Wednesday, August 26, 2015


USIKU huu imefanyika Droo ya Raundi ya 3 ya Kombe la Ligi huko England ambalo hujulikana kama Capital One Cup na kujumuisha Vigogo wa England ambao wanaanzia Raundi hii.
Timu hizo kubwa ni Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, Chelsea, Manchester United, Liverpool na Arsenal.
Mechi za Raundi hii ya 3 zitachezwa Wiki ya kuanzia Septemba 21.
Timu nyingine za Ligi Kuu England zilicheza Raundi ya Pili Jumanne Usiku.
DROO KAMILI:
Man United v Ipswich Town
Liverpool v Carlisle
Crystal Palace v Charlton
Middlesbrough v Wolves
Norwich v West Brom
Hull v Swansea
Leicester v West Ham
Aston Villa v Birmingham
Tottenham v Arsenal
Sunderland v Man City
Newcastle v Sheffield Wednesday
Reading v Barnsley/Everton
Preston v Bournemouth
Walsall v Chelsea
MK Dons v Southampton
Fulham v Stoke City

Tuesday, August 25, 2015

Klabu ya Juventus ya Italia bado inaongeza nguvu katika kikosi chake kwa kusajili wachezaji kadhaa ili kuweza kuendana na kasi ya michuano mbalimbali itakayoshiriki msimu huu. Juventus ambayo imeondokewa na nyota kadhaa kikosini mwake ikiwemo Carlos Tevez na Andre Pirlo imeongeza nguvu katika kikosi chake.
2BA4773D00000578-3209576-image-a-1_1440491596620
Juventus August 25 wamekamilisha usajili wa mkopo kwa muda wa msimu mmoja wa aliyekuwa winga wa klabu ya Chelsea Juan Cuadrado ambaye alijiunga na Chelsea mwaka 2015 akitokea katika klabu ya Fiorentina ya Italia.
Pichaz Juan Cuadrado alivyowasili Italia August 24 kabla ya August 25 kutangazwa kusajiliwa

2BA2EA5500000578-0-image-a-83_1440458491736

Mshambuliaji Pape Abdoulaye N'Daw mwenye umri wa miaka 21 anatarajiwa kutua leo usiku kutoka Dinamo Bucuresti ya Romania kufanya majaribio Simba SC 

SIMBA SC imeachana na Msenegali, Papa Niang baada ya kumjaribu kwa dakika 45 tu jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hawajachoka, Simba SC leo wanatarajia kupokea wachezaji wawili wengine wa kigeni kuwafanyia majaribio, ambao ni Msenegali Pape Abdoulaye N'Daw na Mmali.
N'Daw mwenye umri wa miaka 21, kwa sasa anachezea klabu ya Liga I ya Romania, Dinamo BucureÈ™ti, wakati wa Mali bado jina lake halijapatikana na haijulikani anatoka timu gani. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba wachezaji hao watafanyiwa majaribio na atakayevutia zaidi, ndiye atapewa Mkataba. 
Niang alikuja SImba SC baada ya klabu hiyo kushindwa kufikia makubaliano na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Kevin Ndayisenga juu ya dau la usajili.
Niang kutoka klabu ya Alianza F.C. ya El Salvador ambaye ni mdogo wa mshambuliaji wa kimataifa wa zamani wa Senegal, Mamadou Niang jana alishindwa kabisa kuwashawishi wana Simba kwa soka yake.
Papa Niang amerejea kwao baada ya 'kuchemsha' jana katika mchezo wa kiraiki na Mwadui

Mchezaji huyo wa zamani wa CF Mounana ya Gabon, Al Shabab SC ya Kuwait, FC Vostok ya Kazakhstan, FF Jaro, AC Oulu na FC OPA za Finland alitarajiwa kuondoka usiku wa jana kurejea kwao, ikiwa ni baada ya siku tatu za kuwa Dar es Salaam.
Awali Simba SC pi ilishindwa kumsajili mshambuliaji mwingine hatari wa Vital’O, Laudit Mavugo kufuatia klabu mbili za nchini humo kupandisha thamani ya mchezaji huyo na kuwa Sh. Milioni 200, badala 110 walizokubaliana awali.
Aidha, kuibuka pia kwa mzozo mpya kati ya klabu ya Vital’O FC na Solidarity FC, inayodai kumlea Mavugo na kudai ina hakimiliki ya mchezaji huyo nako kuliishitua Simba.
Vital’O ikaikoroga zaidi Simba SC baada ya kudai kiwepo kipengele cha wao kupata asilimia 50 kama mchezaji huyo atauzwa na Wekundu hao wa Msimbazi kwenda klabu nyingine.   


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA kipa wa Simba SC kwa misimu mmoja nusu uliopita, Ivo Philip Mapunda (pichani kushoto) amesema anarejea Kenya, baada ya kuachwa na klabu hiyo mapema mwezi huu.
Ivo aliyewahi kudakia pia Yanga SC, amesema hana kinyongo na Simba SC na anaondoka nafsi yake ikiwa safi kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine.
“Nawashukuru mashabiki wa mpira haswa wa Simba kwa kuwa nami kipindi chote, nilipofanya vibaya na nilipowaudhi mlikuwa nami na ndiyo soka ipo hivyo,”amesema.
Ivo Ameongeza; “Maisha yana changamoto na ndiyo nimezipata kwa sasa Simba baada ya watu fulani kufanya hivyo, ila naamini maisha ni popote na Mungu ndiye kila kitu,”.
Ivo amesema kwamba anarudi Kenya ambako bado anakubalika na anaamini atapata timu.
Ivo alijiunga na Simba SC Desemba 2013 akitokea Gor Mahia ya Kenya katika cha mwaka mmoja na nusu wa klabu hiyo ya Msimbazi, ameidakia jumla ya mechi 39 na kufungwa mabao 25, akiiwezesha timu hiyo kutwaa taji moja, Kombe la Mapinduzi.
Ivo Mapunda akipongezwa na wenzake Januari mwaka huu baada ya kuiwezesha timu hiyo kutwaa Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Amaan, Zanzibar

Zaidi Ivo aliwafurahisha mno wana Simba kwa kulinda vyema lango kwenye mechi dhidi ya mahasimu, Yanga SC na kwa kipindi chake chote Wekundu wa Msimbazi hawajapoteza mechi dhidi ya watani wao hao.
Alianza na mechi ya Nani Mtani Jembe mwaka juzi, Simba ikishinda 3-1, akadaka mechi ya Ligi Kuu, timu hizo zikitoka sare ya 1-1 kabla ya Desemba mwaka jana kuiongoza tena timu hiyo kushinda mechi ya Nani Jembe 2 mabao 2-0 na mechi yake ya mwisho ya watani kudaka, Wekundu wa Msimbazi walishinda 1-0 katika Ligi Kuu.
Ivo Mapunda ameondoka Simba SC baada ya mechi 39, akifungwa mabao 25

REKODI YA IVO MAPUNDA SIMBA SC

Simba 3-1 Yanga (Nani Mtani Jembe, alifungwa moja Dar)
Simba SC 1-0 AFC Leopard (Mapinduzi, hakufungwa Zbar)
Simba SC 0-0 KCC  (Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 2-0 Chuoni (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 2-0 URA (Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 0-1 KCC (Fainali Kombe la Mapinduzi, alifungwa moja)
Simba SC 1-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu Bara hakufungwa)
Simba SC 4-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu Bara, hakufungwa)
Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Bara, alifungwa moja)
Simba SC 0-1 Mgambo JKT (Ligi Kuu Bara, alifungwa moja)
Simba SC 0-1 Coastal Union (Ligi Kuu, alifungwa moja)
Simba SC 1-2 Azam FC (Ligi Kuu, alifungwa mbili)
Simba SC 1-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu, alifungwa moja)
Simba SC 0-1 Ashanti United (Ligi Kuu, alifungwa moja)
Simba SC 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu, alifungwa moja)
Simba SC 0-3 ZESCO United (Simba Day, alifungwa mbili Dar)
Simba SC 2-1 Kilimani City (kirafiki Zanzibar, hakufungwa)
Simba SC 2-0 Mafunzo (kirafiki Zanzibar, hakufungwa )
Simba SC 5-0 KMKM (Kirarfiki, Zanziabr hakufungwa)
Simba SC 3-0 Gor Mahia (Kirafiki, Dar es Salaam, hakufungwa)
Simba SC 0-1 URA (Kirafiki, Dar es Salaam alifungwa moja) 
Simba SC 2-2 Coastal Union (Ligi Kuu, alifungwa mbili)
Simba SC 1-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 2-4 Mtibwa Sugar (Kirafiki Chamazi, alifungwa nne)
Simba SC 2-0 Yanga SC (Nani Mtani Jembe, hakufungwa)
Simba SC 3-1 Mwaduni FC (Kirafiki, Taifa alifungwa moja)
Simba SC 0-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu Taifa, alifungwa moja)
Simba SC 0-0  Mtibwa Sugar (aliingia dakika ya 90 Simba ikashinda penalti 4-3 Fainali Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 2-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu, alifungwa moja)
Simba SC 0-0 Coastal Union (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 2-0 Polisi Moro (Ligi Kuu, alidaka kipindi cha kwanza akaumia na kutoka bila kufungwa) 
Simba SC 0-1 Stand United (alifungwa moja)
Simba SC 5-0 Prisons (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 1-0 Yanga SC (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 1-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 0-2 Mgambo Shooting (Ligi Kuu, alifungwa moja akatolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili)
Simba SC 4-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 3-0 Ndanda FC (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 2-1 Azam FC (Ligi Kuu, alifungwa moja).
Ivo Mapunda wakati anasaini Simba SC Desemba mwaka juzi mjini Nairobi

aiyolacoverfinal (1)
Diamond Platnumz ameamua kumtambulisha msanii wake wa kwanza mtu wangu kutoka kwenye lebo yake ya WCB,msanii huyu anaitwa Harmonize na hii ni singo yake ya kwanza inaitwa Aiyola,ukiisikiliza unaweza kuandika comment hapo chini.
Klabu ya soka ya Simba mwishoni mwa wiki iliyopita ilimleta mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal Papa Niang ambaye ni ndugu wa damu na Mamadou Niang mchezji aliyetamba katika vilabu kadhaa barani Ulaya ikiwemo timu ya taifa ya Senegal.
DSC_9335
August 24 Papa Niang alijaribiwa na wekundu hao wa msimbazi katika mechi ya kirafiki ya Simba dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga inayofundishwa na kocha Jamhuri Kiwelo, taarifa zilizotoka ni  kuwa Niang hajafanya vizuri majaribio ya Simba hivyo August 25 inaleta msenegal mwingine kuja kumfanyia majaribio.
Taarifa zinaeleza Simba inamleta Abdulah Ndow kutoka Senegal ila analetwa na wakala aliyemleta kocha wa Simba Dylan Kerr, msenegal huyo anayekuja Simba inadaiwa ameshawahi kucheza Ulaya katika klabu ya Bucharest ila alivunja mkataba baada ya kutolipwa fedha anazodai.

EL 1Mgombea Urais wa UKAWA 2015 Edward Lowassa alianza ziara ya kuingia mitaani Dar es salaam Aug 24 2015 ili kukutana na Wananchi uso kwa uso na kusikiliza matatizo yao.
 Lowassa amesema atatusaidia, tuna furaha sana leo ametutembelea, hatukutarajia,” alisema mwanafunzi wa Shule ya Nyegulu, Dorcus Wilson baada ya kuzungumza na Lowassa.

Mwanafunzi mwingine wa Shule ya Msingi Maarifa, Grey Issa alisema amefurahi kumuona Lowassa kwa sababu amekuwa akimwona kwenye televisheni. Alisema kero yao kubwa ni unyanyasaji wanaoupata kutoka kwa makondakta wa daladala.

Baadhi ya wananchi walisema Lowassa ndiye rais wao mtarajiwa kwa sababu haijawahi kutokea kwa kiongozi yeyote mkubwa kufika kwenye makazi yao na kuzungumza nao... 

“Lowassa ndiye rais wetu. Ni mtu muhimu sana, amefika kwetu na kuzungumza na sisi. Angekuwa ni kiongozi mwingine angefika hapa na walinzi wengi,” alisema Augustino Nyembo, mkazi wa Gongo la Mboto.

Ilipotimu saa 2.35 asubuhi, waziri mkuu huyo wa zamani, aliingia kwenye daladala lililofika kituoni hapo kupakia abiria na kusafiri nalo kwenda Chanika. Baadhi ya abiria walistaajabu kumuona akiingia kwenye daladala hilo na baadhi yao waliteremka kwa mshangao.

Ndani ya daladala hilo, Lowassa aliketi kiti kimoja na mwanafunzi na muda wa kulipa nauli ulipofika, kondakta alisema; “Kwa kuwa wewe ni rais mtarajiwa sitakutoza nauli, utapanda bure”, ombi ambalo mgombea huyo alilikataa.

Lowassa alitoa noti ya Sh2,000 na kumtaka konda achukue nauli yake, pia akate ya mwanafunzi aliyekaa naye. Kondakta alichukua fedha hizo na hakurejesha chenji ya Sh1,400 wala kudaiwa. Watu wengine waliokuwa wameongozana naye katika daladala hilo walijilipia nauli ya Sh400 kila mmoja kutoka Gongo la Mboto mpaka Chanika.

Kondakta huyo, alimweleza Lowassa kuwa tatizo kubwa wanalolipata katika kazi yao ni kutokuwa na mikataba ya kazi na kwamba wanaweza kufukuzwa muda wowote bila kuwa na utetezi wa namna yoyote.

Mgombea huyo wa urais, pia alizungumza na wananchi eneo la Chanika na kuwasikiliza kisha kuendelea na ziara yake kuelekea Mbagala kwa kutumia gari lake.

Bodaboda wajiunga na msafara
Wakati msafara wa Lowassa ukielekea Mbagala, baadhi ya waendesha bodaboda waliufuata hadi uliposimama kwa ajili ya kujaza mafuta eneo la Kajiungeni.

Mmoja wa vijana hao, Zawadi Mrutu alisema wanampenda mgombea huyo kwa sababu ni mchapakazi na anaweza kuleta mabadiliko. Alisema hawajapewa fedha kujiunga na msafara wa Lowassa, bali ni mapenzi yao.

Alisema kiongozi wa wajasiriamali hao aliyezungumza juzi kwenye mkutano wa CCM hajui shida wanazozipata barabarani kwani kama angezifahamu... “asingezungumza vile. Hatumtaki tena kwenye chama chetu.”

Kijana mwingine, Ali Kasembo alisema wanachotaka ni mazingira mazuri ya kufanya kazi yao ya kusafirisha abiria. Alisema wamekuwa wakinyanyaswa na askari polisi katika kazi yao kwa madai kwamba wanakiuka taratibu.

“Lowassa ni jembe, namkubali sana. Tunataka atusaidie kupata mazingira mazuri ya kazi ili na sisi tuliojiajiri kwa kazi hii tujisikie huru, siyo kila siku tunakimbizana na polisi,” alisema Kasembo, anayefanya shughuli zake za bodaboda Chanika.

Akiwa Mbagala
Msafara wa Lowassa ulipofika eneo la Rangitatu, Mbagala na wananchi kumbaini, walianza kufuata gari lake huku wakiimba; “pisha, pisha, Rais apite…, pisha, pisha, Lowassa apite…”

Ilipotimu saa 4.05 asubuhi, msafara huo uliingia kwenye Kituo cha Daladala Mbagala Rangi Tatu huku watu wakisukumana kutaka kumuona.

Hata hivyo, Lowassa alipojaribu kuzungumza nao hakusikika kutokana na kelele zilizotawala kituoni hapo.

Baada ya spika kufungwa kwenye gari, mgombea mwenza, Juma Duni Haji alisimama na kusema wamepita kuwasalimia wale ambao wameitwa malofa. Alisema hatazungumza zaidi kwa sababu wataambiwa walifanya mkutano usiotambulika rasmi.

“Leo tumepita kuwasalimia maskini wanaoambiwa ni vibaka, malofa, wapumbavu. Tunaomba mtuache tuendelee na safari, tutakutana Jumamosi,” alisema Duni na kurejea kwenye gari na kuendelea na safari yao.

Mwenyekiti Monduli ahamia Chadema
Wakati huohuo; Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Monduli, Arusha, Reuben Ole Kuney ametangaza kujiondoa CCM na kujiunga na Chadema.

Ole Kuney ambaye aliwahi kuwa mkuu wa wilaya mbalimbali kabla ya kustaafu, alisema amejiondoa CCM kutokana na kubaini chama hicho kimeshindwa kusimamia taratibu na kanuni zake.

“Mimi kama mwenyekiti wa wilaya anayotoka Lowassa, waziri mkuu wa zamani na mbunge wetu, siwezi kubaki CCM kwani chama kilishindwa kutenda haki katika mambo mengi ikiwamo mchakato wa urais,” alisema.

Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Elisante Kimaro alisema kamati ya siasa ya chama hicho itakutana Jumatatu kujadili mwenendo wake na kupanga ratiba ya kampeni.

waliotembelea blog