Msanii Juma Nature ‘Kiroboto’ akizungumza katika mkutano na waandishi
wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu tamasha kubwa la kuadhimisha
miaka 16 ya kazi zake za muziki nchini pamoja na hitimisho la sherehe
za mwaka mmoja za Kituo cha Redio cha EFM linalofahamika kwa jina la
Komaa Concert litakalofanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi Ukumbi wa Dar
Live Mbagala kuanzia saa 12 jioni.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara
ya Mahusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo,
ambao ni waandaaji wa tamasha hilo. Kulia ni Meneja wa Maendeleo ya
Biashara wa Kampuni ya Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo
wa dhamini wa tamasha hilo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha
EFM, Denis Ssebo (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka
kulia ni Msanii Said Christopher ‘Mucky), Meneja wa Maendeleo ya
Biashara wa Kampuni ya Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo
wa dhamini wa tamasha hilo,Msanii Juma Nature, Msanii, Semani Jabiri
‘Msagasumu’ na Msanii Snura Mushi.
Wasanii watakaotoa burudani la nguvu siku hiyo ya tamasha. Kutoka
kulia, Fredy Felix ‘Fredwayne’ Juma Nature, Snura Mushia, na Said
Christopher ‘Mucky)
Ofisa Habari wa Kituo cha Redio cha EFM, Lydia Moyo (kushoto), akiperuzi simu yake katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua tukio hilo.