Tuesday, March 10, 2015



Mchezaji wa Liverpool  Philippe Coutinhowakati wa Mchezo wao wao na Timu ya  Blackburn
Bradford waliwaondosha  Chelsea na wanategemea kati yake na  Reading kucheza na Arsenal kutokana na Droo iliyochezeshwa punde..-BRADFORD/ READING vs ARSENAL
-ASTON VILLA vs BLACKBURN/LIVERPOOL


Dakika 90 zimemaliza Arsenal wakiwa na Ushindi wa bao 2-1, bao la Ushindi likifungwa na Danny Welbeck mchezaji wa zamani wa Timu ya Manchester United katika dakika ya 61 baada ya Valencia kufanya makosa ya kurudisha mpira nyuma.2-1Ushindi!!Umetupa bao!!Umerudi na kuua!!.Danny Welbeck baada ya kutupia nyavuni bao la pili.
Arsenal walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 25 la Nacho Monreal na Wayne Rooney kusawazisha Dakika ya 29 lakini Welbeck kuipa ushindi Arsenal katika Dakika ya 61. Nje!! Di MariaMan United walimaliza Mechi hii Mtu 10 baada ya Angel Di Maria kulambwa Kadi za Njano mbili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Huu ulikuwa Usiku mwema kwa Arsenal ambao wameendelea kutetea vyema Kombe la FA CUP ambalo wao ni Mabingwa Watetezi na pia wamekuwa wakiteswa na Man United kwa kufungwa Mechi 11 kati ya 15 zilizopita.
Unamvuta Mwamuzi jezi???Mhhh !! Hii ni La Liga EPL??Kaa mbali kwanza!Unakosea Di Maria ...tulia!! Rooney akituliza Jazba!!Pia kwenye Droo ya Nusu Fainali ya FA CUP, iliyofanyika maraa baada ya Mechi hii, Arsenal watacheza na Mshindi kati ya Bradford City au Reading ambao Juzi walitoka 0-0 kwenye Mechi yao ya Robo Fainali.
Nusu Fainali nyingine itakuwa kati ya Mshindi wa Liverpool na Blackburn Rovers, ambao nao walitoka 0-0, dhidi ya Aston Villa.
Kipindi cha pili Danny Webeck mchezaji wa zamani wa Man United aliipa bao la pili Arsenal katika dakika ya 61 na kufanya 2-1. Rooney akisawazisha bao kipindi cha kwanzaRooney  baada ya kuisawazishia United bao kwa kufanya 1-1 dhidi ya Arsenal katika kipindi cha kwanza. Mpaka mapumziko kipindi cha kwanza Manchester United 1-1 Arsenal.1-1Nacho Monreal dakika ya 25 kipindi cha kwanza kaifungia bao Arsenal nao Man United walifufuka na dakika ya 29 Wayne Rooney aliisawazishia bao Manchester United kwa kichwa na kufanya 1-1.Mzee Ferguson akishuhudia kipute Old TraffordMhh!!VIKOSI:
Man United 11: De Gea, Valencia, Smalling, Rojo, Shaw, Blind, Herrera, Di Maria, Fellaini, Young, Rooney
Akiba: Valdes, Rafael, Jones, Carrick, Januzaj, Mata, Falcao


Arsenal 11: Szczesny, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Cazorla, Oxlade-Chamberlain, Ozil, Sanchez, Welbeck
Akiba: Martinez, Gibbs, Chambers, Ramsey, Giroud, Walcott, Akpom 
Man United vs Arsenal

Monday, March 9, 2015


Jumatatu Usiku saa 10:45 huko Old Trafford Manchester United watacheza na Mabingwa Watetezi Arsenal katika mchezo wa Robo Fainali FA CUP.Nani kuondoka na pointi tatu leo kati ya Van Gaal na Wenger?

Saturday, March 7, 2015


Baada ya kuliteka na kulikamata vyema soko la muziki wa jana na hata leo, Mwanamuziki mwenye mafanikio kutoka nchini Uganda Jose Chameleone ameachia hewani mkwaju wake mpya na safari hii akivuka mipaka hadi nchini Nigeria, na sasa ana mshirikisha msanii toka pale anaitwa Pato Ranking.


Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki kwa viwanja sita kutimua vumbi, michezo mitatu ikifanyika siku ya jumamosi na michezo mingine mitatu kufanyika siku ya jumapili.
Katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya Polisi Morogoro watawakaribisha maafande wa Ruvu Shooting kutoka Mlandizi, Coastal Union watakua wenyeji wa Kagera Sugar kwenye dimba la Mkwakwani, huku JKT Ruvu wakiwakaribisha Azam FC katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Jumapili Mgambo JKT watakua wenyeji wa timu ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Mtibwa Sugar wakiwa wenyeji wa wagonga nyundo timu ya Mbeya City katika Uwanja wa Manungu Turiani.
Katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam watani wa jadi Simba SC watakuwa wenyeji wa Young Africans, mchezo unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Friday, March 6, 2015


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.
 
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa fundi mitambo Mkuu wa Azam TV Bw. Mehdoub al Hadad juu ya namna gari la kurusha matangazo nje ya studio (OB Van) linavyofanya kazi wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara wakitmbezwa sehemu mbali mbali za Azam TV na mwenyeji wao Bw. Saidi Salim Bakhressa wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Bw. Saidi Salim Bakhressa wakati alipohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Bw. Saidi Salim Bakhressa wakati alipohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015. 


 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa pole wanafamilia wa MzeeZakaria  Limbe ambao wamepoteza wototo wane katika mafa ya mvua kubwa yenye upepo na  mawe iliyonyesha katika eneo la Mwakata Machi  3 usiku. Alikwenda katika maeneo yaliyoathirika leo  kuwapa pole wananchi. 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipa pole Shoma Petro  ambaye ni mmoja wa majeruhi wa maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa yenye upepo na mawe iliyonyesha kwenye  eneo la  Mwakata wilayani Kahama Machi 3, 2015 usiku. Mheshimiwa Pinda alikwenda kwenye hospitali a wilaya ya Kahama kuwapa pole  majeruhi waliolazwa hospitalini hapo.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Mzee  Donald Lubunda ambaye  amepoteza watoto wane katika maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha  katika  eneo la Mwakata wilayani Kahama Machi 3 usiku. Mheshimiwa Pinda alikwenda kuwapa pole waathirka leo
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Waziri wa Nchi Ofisi yaWaziri Mkuu, Jenista Mhagama  (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa ShinyangaDr Rufunga kukagua maeneo yalyoathiriwa na mvua kubwa iliyoambatana  na upepo mkali na mawe katika eneo  Mwakata wilayani Kahama usiku Machi 3, 2015. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametembelea baadhi ya familia zilizopoteza wapendwa wao pamoja na majeruhi waliolazwa kwenye hospitali ya wilaya ya Kahama kutokana na maafa ya mvua ya mawe iliyonyesha usiku wa kuamkia jana.

Akizungumza na wafiwa katika vijiji vya Mwakata na Magugung’hwa katika kata ya Mwakata wilayani Kahama leo mchana (Alhamisi, Machi 5, 2015) Waziri Mkuu alisema Serikali haitawaacha katika kipindi hiki kigumu walichonacho.

Waziri Mkuu pia alitumia fursa hiyo kuwafikishia wafiwa na waathirika wa maaafa hayo salamu kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye aliwaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.

Akiwa katika shule ya msingi Mwakata ambako watu 250 wanahifadhiwa hapo kwa muda, Waziri Mkuu aliwaambia wakazi hao pamoja na wananchi waliofika kumsikiliza kwamba Serikali imepanga kuleta vyakula, mahema, mablanketi na madawa ya hospitali ili kuwasaidia waathirika hao. “Serikali haitaacha mtu afe kwa njaa,” alisema.

waliotembelea blog