Saturday, August 9, 2014
Friday, August 8, 2014
7:16 AM
Unknown
KIKOSI cha
pili cha mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc kitakabiliana
na Mtibwa Sugar katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa leo katika
Tamasha la Usiku wa Matumaini , uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Hii itakuwa mechi nzuri kwa timu zote kuangalia uwezo wa wachezaji waliowasajili na wale waliopandishwa kutoka timu za vijana.
Afisa
habari wa Azam fc, Jafar Idd Maganga alisema wanauchukulia mchezo huo
kwa uzito wa hali ya juu kwasababu ni nafasi nzuri kwa wachezaji wao
kuonesha uwezo mbele ya timu bora ya Mtibwa Sugar.
7:14 AM
Unknown
Manchester City wanamtaka Sergio Aguero asaini mkataba mpya kabla ya kuanza msimu mpya.
MANCHESTER
City wanatumaini kuwa Sergio Aguero atasaini mkataba mpya utakaomfanya
alipwe paundi laki mbili na elfu 10 kwa wiki kabla ya kuanza kwa msimu
mpya.
Mabingwa
hao wa England wameweka wazi kuwa mshambuliaji huyo wa Argentina yupo
katika mipango yao ya baadaye pamoja na nahodha Vincent Kompayn na
mazungumzo yanaendelea vizuri.
Barcelona
na Real Madrid wameweka wazi siri ya kuvutiwa na mshambuliaji huyo
mwenye miaka 26, lakini City wanafanya haraka ili kumuongezea mkataba wa
miaka mitano.
7:08 AM
Unknown
Mwimbaji
wa Injili, Upendo Nkone akiwapa matumaini wananchi waliohudhuria Usiku
wa Matumaini muda huu ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Upendo Nkone akiwapa burudani wapenzi wa Gospel ndani ya Tamasha la Matumaini 2014.
Umati wa watu ndani ya Tamasha la Matumaini 2014.
Nkone akizidi kufanya yake pamoja na vijana wake.
Baadhi ya wanahabari na wadau wakifuatilia tamasha hilo.
7:04 AM
Unknown

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Hussein Shariff, Manyika Peter Manyika, Mohammed
Hussein, Abdi Banda, Elius Maguli, Saad Kipanga watatambulishwa kesho katika
Tamasha la ‘ Simba Day’ katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Tamasha hilo la kila mwaka ambalo hufanyika tarehe
8, Agosti ya kila mwaka lilianza kufanyika kwa mara kwanza msimu wa kiangazi
mwaka 2009 chini ya waasisi, Mzee Hassani Dalali na aliyekuwa katibu mkuu wa
klabu hiyo, Mwina Kaduguda kwa lengo la kutambulisha wachezaji wapya, jezi mpya
za klabu huku pia lengo kiuchumi likiwemo .
Wachezaji hao wazawa wataungana na wachezaji wapya
wa kigeni, Paul Kiongera raia wa Kenya, Mrundi, Pierre Kwizera, na washambuliaj
raia wa Botswana, Jerome Ramathakwane na
Ousainou Manneh kutoka nchini Gambia katika mchezo maalumu dhidi ya Zesco ya
Zambia. Ambao watajaribiwa kwanza na kocha Zdravko Logarusic kabla ya
kusajiliwa.
Hussein Sharrif 'Casillas' naye atambaulishwa kesho
Tamasha hilo litafanyika kesho Agosti 9, kufuatia
siku ya leo kuwa na Tamasha la Matumaini na mashabiki wa Simba watapata fursa
ya kuona na kununua jezi mpya za klabu hiyo ambazo watazitumia msimu ujao.
Simba imejipanga kuhakikisha inaimarisha zaidi kikosi chake ndiyo maana
wamekuwa ‘ busy’ kusaka wachezaji wakati huu dirisha la usajili likikaribia
kufungwa.
WACHEZAJI SABA WA KIGENI
Donald Musoti, Amis Tambwe, Joseph Owino,
Kiongera, Kwizera, Jerome, na Manneh watakuwepo uwanjani siku ya kesho.
Wachezaji hao wote ni raia wa kigeni na wamekuja kwa ajili ya kuifufua Simba
baada ya kuwa na misimu miwili mibaya katika ligi kuu ya Tanzania Bara. Simba
inaweza kuwasaini wachezaji wote hao kama mwalimu Logarusic ataridhika na
viwango vyao kwa sababu sheria ya wachezaji wa kulipwa itabadilishwa na kufikia
wachezaji saba.

Abdi Banda atatambulishwa kesho 'Simba Day'
Hii ni mara ya kwanza kwa Tamasha la Simba Day
kuwa na wachezaji saba wa kigeni na ni wakati mwafaka kwa mashabiki wa klabu
hiyo kujitokeza uwanjani siku ya kesho kwa lengo la kwenda kuitazama timu yao
mpya ambayo inasukwa katika mtindo wa kimataifa.
Ligi kuu inataraji kuanza kutimua vumbi lake,
Septemba 20, hivyo baada ya Tamasha hilo timu itakuwa na muda mrefu wa
kujiandaa na kutengeneza timu kabambe ambayo itaweza kutoa ushindani kwa timu
za Yanga SC, Azam SC, Mbeya City ambazo zimeoneka kufanya usajili makini zaidi
licha ya kumaliza katika nafasi tatu za juu msimu uliopita.
Wachezaji kama nahodha Nasorro Masoud ‘ Collo’,
Amri Kiemba, Issa Rashid, William Lucian, Jonas Mkude, Said Ndemla, Miraji
Adam, Abdallah Seseme, Ibrahimu Twaha, Ramadhani Singano, Haroun Chanongo,
Uhuru Suleimani, Ivo Mapunda wataungana na wachezaji wapya waliosajiliwa
klabuni hapo siku ya kesho huku mwanamuziki nyota nchini, Diamond Platnumz
akitaraji kutumbuiza kabla ya zoezi la utambulisho wa wachezaji kuanza. Itakuwa
siku ya aina yake kwa wapenzi wa klabu hiyo.

NI SIKU NZURI KWA KUSAIDIA UJENZI WA UWANJA WA
KLABU
Wiki iliyopita Simba ilianza kufanya mazoezi
katika uwanja wake wa wazi huko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, na
juzi wanachama wa tawi la ‘ Home Boys Wazo Hill’ waliahidi kutoa tani 10 za
mifuko ya saruji ili kusaidia uendelezaji wa ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo
ambao unaendelea. Simba inaweza kutumia Tamasha hilo kuwaunganisha wanachama
wake ambao walikuwa katika tofauti miaka ya karibuni kutokana na uongozi mbaya
wa utawala uliopita. Kila mwanachama wa Simba anaweza kujitolea kwa namna
anavyoweza kwa sababu wanachama ndiyo sehemu muhimu ya kuijenga klabu hivyo ushirikiano ni muhimu kuanzia kwa
viongozi, wanachama, wachezaji na benchi la ufundi. Simba Day ina maana kubwa
na wanachama wanaweza kutumia nafasi yao kusaidia kwa hali na mali klabu yao.
Kila la heri Tamasha la Simba Day…..
7:01 AM
Unknown
Wasiwasi: Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger alikiri kuwa kuna timu hatari katika droo ya UEFA iliyofanyika leo ijumaa.
ASERNAL watakabiliana na Besiktas katika mchezo wa raundi ya pili ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA).
Arsene Wenger alikwepa kukutana na Athletic
Bilbao, Lille , FC Copenhagen, Standard Liege, lakini sasa atachuana na
timu hiyo ya Uturuki ambayo siku za karibuni ilimsajili Demba Ba kutoka
Chelsea kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 4.7.
Besiktas ilimaliza katika nafasi ya tatu
msimu uliopita, lakini imefuzu kucheza UEFA baada mabingwa Fenerbahce
kufungiwa kucheza mechi za michuano ya ulaya kwa kosa la kupanga matokeo
ya mechi ya nyumbani.
Arsenal atacheza michuano ya ulaya kwa mwaka wa 17 mfululizo
Amefungiwa: Beki Bartosz Bereszynski alitolewa dakika za mwisho katika kipigo cha Celtic
Wachezaji wa Legia Warsaw wakishangilia baada ya dakika tisini, huku Stefan Johansen akiacha hoi.
Arsenal watasafiri kwenda Uturuki
kucheza mechi ya kwanza Agosti 19 au 20 mwaka huu na mechi ya marudiano
itapigwa Emirates Agosti 26 au 27.
Kiungo wa Asernal mwenye asili ya Uturuki, Mesut Ozil alifurahishwa na droo na kuandika kwenye mtandao wa Twita akisema: 'Droo nzuri! tayari tunaangalia mbele kuelekea mechi dhidi! @Besiktas! #Turkey #İstanbul #Arsenal #AFC #UCLdraw'.
Wakati huo huo, leo asubuhi, Celtic wamepewa nafasi ya kusonga mbele baada ya kubainika kuwa klabu ya Legia Warsaw ilimchezesha mchezaji asiyekuwa na vigezo.
Kamati ya nidhamu ya UEFA ilikutana na
kutoa maamuzi kabla ya droo mjini Nyoni na kuamua kuwa Celtic wanatakiwa
kupewa ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa pili na inamaanisha
wamesonga mbele kwa magoli ya ugenini.
DRAW NZIMA HII HAPA
FULL CHAMPIONS LEAGUE PLAY-OFF ROUND DRAW
Maribor vs Celtic
Red Bull Salzburg vs Malmo
Aalborg vs APOEL
Steaua Bucharest vs Ludogoret
Slovan Bratislava vs BATE
Besiktas vs Arsenal
Standard Liege vs Zenit
Copenhagen vs Bayer Leverkusen
Lille vs Porto
Napoli vs Athletic Bilbao
Ties to be played on the 19/20 and 26/27 August
Subscribe to:
Posts (Atom)
RSS Feed
Twitter