Thursday, July 17, 2014


Hands off: Juventus are keen on keeping hold of star midfielder Arturo Vidal (left)
Hang`oki: Juventus wamesema hawatamuuza Arturo Vidal (kushoto).

Imechapishwa Julai 16, 2014, saa 2:39 usiku

KIUNGO wa Juventus, Arturo Vidal hauzwi majira haya ya kiangazi, mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo, Giuseppe Marotta amesisistiza.
 Marotta alikuwa anaongea jana mchana wakati Juventus alikuwa inamtangaza kocha mpya wa klabu hiyo,  Massimiliano Allegri kufuatia kuondoka kwa Antonio Conte. 
Kumakuwepo tetesi nyingi wiki za karibuni zikimhusisha nyota huyo kujiunga na  Manchester United.
Key target: Chile international Vidal had been on Louis van Gaal's summer wish-list
Kwenye rada: Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile, Vidal amekuwa katika rada za kocha wa Man United Louis van Gaal.


Greet: Van Gaal (centre) meets assistant manager Ryan Giggs (left) and executive vice-chairman Ed Woodward
Salamu: Van Gaal (katikati) amekutana na msaidizi wake  Ryan Giggs (kushoto) na makamu mwenyekiti Ed Woodward.

Imechapishwa Julai 16, 2014, saa 2:14 usiku

KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal amewasili katika uwanja wa mazoezi wa Carrington leo jumatano kuanza kazi yake mpya.
Mholanzi huyo alipigwa picha akiwa geti kubwa, lakini baadaye klabu iliposti picha katika mtandao wake wa Twita akiwa na msaidizi wake Ryan Giggs na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo,  Ed Woodward.
Van Gaal alitaka kuonana na wachezaji wake baada ya kombe la dunia pamoja na viongozi wa klabu hiyo.
Underway: The Dutchman has returned from Brazil after leading Holland to a third-place finish
Van Gaal amerudi baada ya kuiongoza Uholanzi kushika nafasi ya tatu ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil. 
Discussions: Giggs, Van Gaal and Clive Woodward have work to do to return United regular success
Majadiliano: Giggs, Van Gaal na Clive Woodward wana kibarua kikubwa cha kuirudisha United katika hadhi yake.

Van Gaal ametua kazini siku nne tu tangu aiongoze Uholanzi kushika nafasi ya tatu na kwa maana hiyo amejinyima mapumziko.
Kocha huyo mwenye miaka 62, ni kocha wa kwanza kuiongoza Man United kutoka nje ya British,na hatakuwa na muda wa kupoteza katika harakati zake za kuijengga United.
Kesho alhamisi, atatangazwa rasmi katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari kabla ya kuanza safari ya kwenda nchini Marekani kuweka kambi ya maandilizi ya kabla ya msimu.
United itacheza mechi dhidi ya Los Angeles Galaxy, Roma, Inter Milan na  Real Madrid, wakati mechi ya kwanza ya Van Gaal katika dimba la Old Trafford itakuwa ya kirafiki dhidi ya Valencia  Agosti 12 mwaka huu.
Siku nne baadaye United wataanza ligi kuu kwa mchezo wa nyumbani dhidi ya Swansea.
Pairing: United will embark on a US tour in the coming days, and Giggs is happy with training so far
Watu wa kazi: Giggs (kushoto) na Van Gaal watafanya kazi pamoja kufuta majanga ya David Moyes msimu uliopita.

Wednesday, July 16, 2014


On the move: Chelsea midfielder John Obi Mikel has been linked with a transfer to an Italian club
Anatimka zake: Kiungo wa Chelsea, John Obi Mikel anahusishwa kuhamia klabu za Italia.

Imechapishwa Julai 16, 2014, saa 12:08 asubuhi

KLABU ya Chelsea wanatarajia kumuuza kiungo wao raia wa Nigeria, John Obi Mikel, huku kukiwa na taarifa kuwa klabu za Italia zimekubali kutoa ofa ya paundi milioni 5.
Mikel alianza katika mechi 11 tu za ligi kuu msimu uliopita   na alipata upinzani mkubwa kutoka kwa Nemanja Matic, Willian na Ramires.
Kitendo cha kiungo Cesc Fabregas kujiunga na klabu hiyo kutokea katika klabu ya Barcelona kwa dau la paundi milioni 30 kunazidi kufinya nafasi ya Mikel msimu ujao.
New boy: Cesc Fabregas has joined Chelsea from Barcelona in a £30million move this summer
Kijana mpya: Cesc Fabregas amejiunga na Chelsea majira haya ya kiangazi kutokea klabu ya Barcelona.

Mikel, aliyecheza katika mechi zote za Nigeria katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 nchini Brazil na kufika hatua ya pili na kupigwa na Ufaransa, amesema kuondoka kwake si kwasababu ya kuwasili kwa Fabregas.
Alisema: "Sina tatizo na kusajiliwa kwa Fabregas," alisema. "Tulikutana mara kwa mara. Hata hivyo hatuchezi nafasi moja".
Wakatai huo huo, beki wa Chelsea, Patrick van Aanholt amethibitisha kuondoka klabuni hapo na anaweza kurithi nafasi ya mchezaji aliyesajiliwa na Newcastle Daryl Janmaat katika klabu ya Feyenoord.
Mholanzi huyo mwenye miaka 23 alijiunga na akademi ya Chelsea mwaka 2009 akitokea PSV Eindhoven, lakini amecheza mechi mbili tu na alitumia msimu uliopita kucheza kwa mkopo katika klabu ya Vitesse.
Van Aanholt ameichezea Uholanzi katika mechi mbili na ameiwakilisha nchi hiyo katika ngazi zote kuanzia miaka 16.
On his way: Patrick van Aanholt has been linked with a move to Feyenoord in Holland +
Anasepa zake: Patrick van Aanholt  anahusishwa kujiungga na  Feyenoord ya nchini Uholanzi.

1951Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
KOCHA wa Simba sc, Mcroatia, Dravko Logarusic ameanza kazi kukinoa kikosi chake kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara katika uwanja wa Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM).
Loga ameamua kuanza kambi mapema kwa lengo la kurejesha heshima ya Simba iliyopotoea kwa miaka mitatu mfululizo.
Katika mazoezi hayo, wachezaji wa zamani ambao hawapo katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania,  Taifa Stars kinachojiandaa na mechi ya Julai 20 dhidi ya Msumbiji wanahudhuria pamoja na wachezaji wapya.
Mshambiliaji wa zamani wa Supersport United ya Afrika kusini, Dani van Wyk amekuwa akihudhuria mazoezi hayo kama sehemu ya kujaribiwa na Loga kabla ya kufanya maamuzi ya kumsaininisha mkataba.
Mchezaji huyo amekuwa akijitahidi kuonesha uwezo wake, lakini Loga anasema anahitaji muda kumtazama kabla ya kufikia makubaliano.
Mlinda mlango bora wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu uliopita, Hussein Sharrif `Iker Casillas` amesharipoti kuanza mazoezi na Simba baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea Kagera Sugar.
Wachezaji wengine wapya walioanza mazoezi ni pamoja na Michael Mgimwa kutoka Thailand, Mohammed Hussein maarufu kama Tshabalala kutoka kwa `wanankulukumbi`, Kagera Sugar.
1
Wakati Simba wakiendelea na mazoezi hayo, nao watani wao wa jadi, Yanga sc wanaendelea kunoa makali katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola chini ya kocha mkuu, Mbrazil Marcio Maximo akisaidiwa na Leonardo Neiva.


Straika wa Atletico Madrid Diego Costa amekamilisha Uhamisho wake kwenda Chelsea na kusaini Mkataba wa Miaka Mitano.
Inaaminika Dau la Uhamisho la Straika huyo Mzaliwa wa Brazil lakini anachezea Spain ni Pauni Milioni 32.
Costa anakuwa Mchezaji wa 3 kuchukuliwa na Chelsea kwa ajili ya Msimu mpya na wengine ni Cesc Fabregas na Mario Pasalic.

Msimu uliopita akiwa na Atletico Madrid, Diego Costa alipachika Bao 36 katika Mechi 52 na kuisaidia Klabu yake kutwaa Ubingwa wa La Liga na kufika Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI waliyodundwa 4-1 na Real Madrid.
Costa


MCHEZAJI wa zamani wa Arsenal na Chelsea Ashley Cole amesema Wachezaji wa England ni waoga kwenda kucheza Klabu za Kigeni.Cole, mwenye Miaka 33, amejiunga na AS Roma ya Italy baada kuondoka Chelsea kufuatia kumalizika kwa Mkataba wake ambao haukuongezwa.
Akiongea na Wanahabari kwa mara ya kwanza kama Mchezaji wa AS Roma, Cole alitamka: “Wachezaji wa Kiingereza pengine wanaogopa kwenda nje ya Nchi, wanajisikia vyema kubaki Nyumbani.”
Kwenye Kikosi cha England kilichokwenda huko Brazil kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia ni Kipa Fraser Forster pekee ndie alikuwa hachezei Klabu ya England lakini nae hakwenda mbali kwani alikuwa Scotland akichezea Celtic.


Akiongea kuhusu kuhamia AS Roma, Cole amesema: “Hii ni nafasi kwangu kujaribu lugha nyingine, utamaduni na maisha mapya.”

Aliongeza: “Siogopi presha. Nimeona ari ya Mashabiki na mapenzi yao nilipotua tu. Nitasikia raha hapa!”
Ingawa Chelsea walikataa kumpa Mkataba mpya, Cole amesisitiza bado anao uhusiano mzuri na Meneja wa Klabu hiyo, Jose Mourinho.
Cole amesaini Mkataba wa Miaka Miwili na AS Roma na Msimu ujao watashiriki UEFA CHAMPIONS LIGI baada ya kumaliza Ligi ya Serie A wakiwa Nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa Juventus.


Fans greet the Germany teamGermany wamerudi Nyumbani kwao Berlin wakiwa na Kombe la Dunia mkononi baada kuwafunga Argentina 1-0 Juzi na kupokewa kwa shangwe kubwa na maelfu ya Wajerumani.That went well! Philipp Lahm and Thomas Muller pulled off a stunt on stage in Germany on Tuesday
Nahodha Philipp Lahm, akifuatiwa na Bastian Schweinsteiger, aliwaongoza Wachezaji wenzake kushuka toka kwenye Ndege.
Maelfu ya Wajerumani walikuwa wakiisubiri Timu yao katikati ya Jiji la Berlin, huko Brandenburg Gate, kwenye eneo linaloitwa Fan Mile, na Kikosi hicho kikiongozwa na Kocha Joachim Low kilikuwa kikizungushwa Mitaa ya Berlin wakiwa juu ya Basi la wazi na kuishia hapo Brandenburg Gate.
Having a ball: Christoph Kramer pretends to play the guitar as they entertain the huge crowd
Huku Mashabiki wakiimba: "Deutschland, Deutschland, Deutschland!", Kocha Low na Wachezaji wake walipokezana kuinua Kombe la Dunia juu na Basi kupita popole likilakiwa na kusindikizwa na Mashabiki kibao.
Boy band material? (from left) Hummels, Lahm, Durm, Kramer and Muller all get in on the guitar act
Huku wakiwa kwenye msafara huo, Wachezaji kadhaa wa Germany walichukua picha kwenye Simu zao na kuziposti moja kwa moja kwenye Twitter huku wakitoa maneno ya furaha.
Hii ni mara ya 4 kwa Germany kutwaa Kombe la Dunia na mara nyingine zilikuwa Miaka ya 1954, 1974 na 1990.
Pleased: Bastian Schweinsteiger and Lukas Podolski pose with the World Cup trophy in Berlin
Mbali ya sherehe hizo za Mjini Berlin, Kikosi hicho cha Germany kina Wachezaji wengi kutoka Bayern Munich na Klabu hiyo imeandaa sherehe maalum kwenye Mji wao Munich ili kuwapokea Wachezaji wao wa Kikosi hicho.

 Lahm akicheza pembeni mwa Thomas Mullerambaye kabeba kombe la Dunia  2014 waliloshinda huko Brazil siku ya Jumapili kwa kuwatungua Argentina bao 1-0, akiwa amelibeba mbele ya mamia ya mashabiki huko kwao Ujerumani leo hii.

 Podolski, Per Mertesacker, Mesut Ozil, Ron-Robert Zieler, Jerome Boateng na Sami Khedira
Mamia ya Mashabiki leo asubuhi huko Ujerumani wakiwasubiri Mabingwa wao Dunia


Wachezaji wakishusha mizigo yao

Wakipunga mikono kwa Mashabiki!!! Mesut Ozil, Ron-Robert Zieler, Erik Durm, Mats Hummels na Shkodran Mustafi

 Ozil, Benedikt Hoewedes na Per Mertesacker kwenye gari ya wazi na kombe lao.

waliotembelea blog