Akiongea na Wanahabari kwa mara ya kwanza kama Mchezaji wa AS Roma, Cole alitamka: “Wachezaji wa Kiingereza pengine wanaogopa kwenda nje ya Nchi, wanajisikia vyema kubaki Nyumbani.”
Kwenye Kikosi cha England kilichokwenda huko Brazil kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia ni Kipa Fraser Forster pekee ndie alikuwa hachezei Klabu ya England lakini nae hakwenda mbali kwani alikuwa Scotland akichezea Celtic.
Akiongea kuhusu kuhamia AS Roma, Cole amesema: “Hii ni nafasi kwangu kujaribu lugha nyingine, utamaduni na maisha mapya.”
Aliongeza: “Siogopi presha. Nimeona ari ya Mashabiki na mapenzi yao nilipotua tu. Nitasikia raha hapa!”
Ingawa Chelsea walikataa kumpa Mkataba mpya, Cole amesisitiza bado anao uhusiano mzuri na Meneja wa Klabu hiyo, Jose Mourinho.
Cole amesaini Mkataba wa Miaka Miwili na AS Roma na Msimu ujao watashiriki UEFA CHAMPIONS LIGI baada ya kumaliza Ligi ya Serie A wakiwa Nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa Juventus.
RSS Feed
Twitter
2:00 AM
Unknown
0 maoni:
Post a Comment