0712461976
KOCHA wa Simba sc, Mcroatia,
Dravko Logarusic ameanza kazi kukinoa kikosi chake kwa ajili ya
maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara katika uwanja wa
Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM).
Loga ameamua kuanza kambi mapema kwa lengo la kurejesha heshima ya Simba iliyopotoea kwa miaka mitatu mfululizo.
Katika mazoezi hayo, wachezaji wa
zamani ambao hawapo katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa
Stars kinachojiandaa na mechi ya Julai 20 dhidi ya Msumbiji wanahudhuria
pamoja na wachezaji wapya.
Mshambiliaji wa zamani wa
Supersport United ya Afrika kusini, Dani van Wyk amekuwa akihudhuria
mazoezi hayo kama sehemu ya kujaribiwa na Loga kabla ya kufanya maamuzi
ya kumsaininisha mkataba.
Mchezaji huyo amekuwa akijitahidi
kuonesha uwezo wake, lakini Loga anasema anahitaji muda kumtazama kabla
ya kufikia makubaliano.
Mlinda mlango bora wa ligi kuu
soka Tanzania bara msimu uliopita, Hussein Sharrif `Iker Casillas`
amesharipoti kuanza mazoezi na Simba baada ya kusaini mkataba wa miaka
miwili akitokea Kagera Sugar.
Wachezaji wengine wapya walioanza
mazoezi ni pamoja na Michael Mgimwa kutoka Thailand, Mohammed Hussein
maarufu kama Tshabalala kutoka kwa `wanankulukumbi`, Kagera Sugar.
Wakati Simba wakiendelea na
mazoezi hayo, nao watani wao wa jadi, Yanga sc wanaendelea kunoa makali
katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola chini ya kocha mkuu, Mbrazil
Marcio Maximo akisaidiwa na Leonardo Neiva.
0 maoni:
Post a Comment