Tuesday, February 25, 2014

Jose Mourinho kocha wa Chelsea

Kocha wa timu ya Chelsea ya England, Jose Mourinho ameshutumu tabia ya kurekodi kwa siri mazungumzo yake kuhusu wachezaji wa timu hiyo.
Mourinho amesema lilikuwa jambo la aibu kuona kwamba mazungumzo binafsi kuhusu wachezaji wa timu yake, yanawekwa hadharani na kampuni moja ya televisheni nchini Ufaransa.
Mourinho amesema alikuwa anatania alipokuwa akilalamika kuwa Chelsea inakosa wachezaji wa nafasi ya ushambuliaji na alimtania Eto'o kuhusu umri wake.
"Yalikuwa mazungumzo ya utani na mtu ambaye hahusiki na masuala ya ulimwengu wa soka," amesema Mourinho.
"Ni fedheha kwa mtu kurekodi mazungumzo binafsi."

G_46334.png
IKIWA imebaki siku moja kabla ya Galatasaray kuikaribisha Chelsea katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, kumezuka vurugu za kupigana na kurushiana viti kati ya mashabiki wa Galatasaray na mahasimu wao Besiktas katika mitaa ya jiji la Istanbul. Kumekuwa na picha za video katika mtandao wa Youtube ukionyesha makundi makubwa ya wahuni wa Galatasaray na Besiktas wakichapana katika mitaa yenye maduka mengi kabla ya mchezo baina ya timu hizo katika Uwanja wa Turk Telekom.
Vurugu hizo ziliendelea pia wakati wa mchezo huo ambao Galatasaray ilishinda kwa bao 1-0. Mashabiki wa Chelsea watakaosafiri kwenda jijini Istanbul kwa ajili ya kuishangilia timu yao wameonywa kuwa makini pindi watakapokuwa huko. (EL)

twiga star by mafoto1 97507
Washabiki wa mpira wa miguu nchini watashuhudia bure mechi ya timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) dhidi ya Zambia (Shepolopolo).
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) itachezwa Ijumaa (Februari 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili alasiri.
Twiga Stars ambayo ilipoteza mechi ya kwanza iliyochezwa Lusaka, Februari 14 mwaka huu kwa mabao 2-1 iko kambini chini ya Kocha Rogasian Kaijage na msaidizi wake Nasra Juma ikijiwinda kuwakabili Wazambia wanaotarajiwa kutua nchini Alhamisi (Februari 26 mwaka huu).
Waamuzi wa mechi hiyo Ines Niyonsaba, Jacqueline Ndimurukundo, Axelle Shikana na Suavis Iratunga kutoka Burundi kutoka Burundi wanatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa (Februari 26 mwaka huu). Kamishna Fran Hilton Smith kutoka Afrika Kusini yeye atatua nchini Februari 27 mwaka huu kwa ndege ya South Africa Airways. Chanzo: TFF

Kocha David Moyes na Wayne Rooney wakizungumza mbele ya waandishi wa habari kuhusu mtanange wao wa leo na Olympiacos. Utakaopigwa usiku leoRooney anataka timu yao ishinde na yeye binafsi anasema yupo fiti na yuko tayari kushirikiana na wenzake kuifunga timu ya Olympiacos.

Fowadi wa United Danny Welbeck, Rooney na Javier Hernandez wakifanya mazoezi jana..jumatatu!
Danny Welbeck akiwa na wachezaji wenzie jana kwenye mazoezi tayari kwa mtanange wao na Olympiacos huko ugenini Chris Smalling, Rio Ferdinand na Marouane Fellaini kwenye mazoezi...
Michuano ya UEFA CHAMPIONS LIGI inaendelea tena leo Jumanne na kesho Jumatano wiki hii kwa Mechi nyingine za kwanza 4 za Raundi hiyo ambapo Timu mbili za England, Mabingwa Manchester United na Chelsea, zitakuwa Ugenini kuanza kampeni zao.
Wiki iliyopita, Timu nyingine mbili za England zilianza vibaya kwa zote kufungwa Mechi zao za Nyumbani wakati Man City walipochapwa kwao Etihad 2-0 na Barcelona na kumaliza Mechi wakiwa Mtu 10 baada ya Beki wao, Martin Demichellis, kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu. 

Monday, February 24, 2014

Mratibu wa Mbio za Uhuru Marathon, Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumzia maandalizi ya uzinduzi wa Mbio hizo kwa Mwaka 2014,ambapo mwaka huu Mbio hizo zitazinduliwa kwenye Kijiji cha Butiama,Mkoani Mara.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Selemani Nyambui akinzungumza kwenye Mkutano huo.

MBIO za Uhuru (Uhuru Marathon) zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi katika kijiji cha Butiama mkoani Mara, Agosti mwaka huu, huku lengo kubwa likiwa ni kudumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, wameamua kuzindulia Butiama ili kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambaye katika uhai wake alipigania mno mambo hayo.

“Tukumbuke Mwalimu Nyerere alipigania mno amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu, pia ndiye muasisi wa Taifa hili, hivyo tuliona bora tukazindulie Butiama ili kumuenzi.”

Alisema, mara baada ya uzinduzi huo wanatarajia kuzunguka nchi nzima kuanzia ngazi ya wilaya, ili kuzitambulisha mbio hizo na kuwakumbusha Watanzania umuhimu wa amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu.

Melleck alisema, kiini cha kuanza kampeni ya kuzindua mbio hizo mapema imekuja, kwani zenyewe zimebeba ujumbe wa amani, umoja na mshikamano, hivyo ni vyema kuwakumbusha Watanzania umuhimu wa kutunza na kuenzi mambo hayo.

“Amani ya nchi yetu katika siku za hivi karibuni inaonekana kwenda vibaya hasa kutokana na baadhi ya vyama vya siasa kufanya siasa kwa visasi badala ya kujenga hoja kukabiliana na changamoto za kisiasa, hivyo ni jukumu letu kuilinda,” alisema.

Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Selemani Nyambui alisema, kuanza maandalizi mapema kwa mbio hizo ni faraja kwao na watahakikisha wanakabiliana na changamoto zote ili ziweze kufana.

Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Desemba 8, mwaka huu na kwa mara ya kwanza zilifanyika mwishoni mwa mwaka jana na kushirikisha wanariadha kutoka nchi mbalimbali.

waliotembelea blog