Sunday, February 9, 2014

140208110255 sochi sage kotsenburg 304x171 reuters nocredit1 326e5
Mwanariadha wa Marekani Sage Kotsenburg amekuwa mwanariadha wa kwanza kunyakua medali ya kwanza ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi inayofanyika katika mji wa Sochi nchini Urusi.

Sage Kotsenburg, amenyakua medali hiyo katika mchezo wa kuteteleza katika barafu kwa kwa kutumia ubao kwa upande wa wanaume, ukiwa ni mmoja katika michezo 12 mipya iliyoingizwa katika michuano hiyo, ili kuwavutia vijana.
Mwanamke wa kwanza kushinda medali ya dhahabu ni Marit Bjoergen wa Norway,katika mbio za marathon za kilomita 15. Umati mkubwa wa mashabiki wa Uholanzi wanatarajiwa kumshangilia bingwa mtetezi wa mchezo wa kuteleza katika barafu, Sven Kramer, akijaribu kutetea taji lake kwa upande wa wanaume mita elfu tano.
Rais Vladmir Putin wa Urusi alifungua rasmi jana(Ijumaa), mashindano ya Olimpiki ya majira ya baridi katika mji wa utalii wa Sochi katika sherehe zilizofana.
Waliokuwa wanariadha mashuhuri nchini Urusi waliubeba mwenge wa Olimpiki kabla ya kuwashwa na aliyekuwa mlinda lango wa mchezo wa magongo Vladislav Tretiak pamoja na mchoraji wa barafu Irina Rodnina.
Katika siku 16 zijazo,karibia wanariadha 3000 watashiriki katika michezo mbalimbali 98 katika mashindano hayo yaliodaiwa kugharimu takriban dola billioni 50. Chanzo: bbcswahili

Mark Harper
Waziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Mark Harper, amejiuzulu baada ya kujulikana kuwa amemuajiri mtu asiyekuwa na kibali cha kubaki nchini.
Alieleza kuwa alidanganywa na mwanamke mmoja aliyemuonesha nyaraka za bandia, alipomuajiri kusafisha nyumba yake.
Bwana Harper alisema kwa sababu alichangia kupitisha bungeni sheria ngumu kuhusu uhamiaji, alihisi inambidi kuwajibika zaidi kushinda wengine.
Chama cha Conservative kimeahidi kupunguza idadi ya watu wanaohamia Uingereza kutoka malaki na kuwa elfu kadha tu.

bale 32a22
REAL Madrid imeifumua mabao 4-2 Villarreal katika mchezo wa La Liga usiku wa jana na kupanda kileleni mwa ligi hiyo, Cristiano Ronaldo akikosekana kutokana na kuanza kutumikia adhabu yake ya mechi tatu.
Mabao ya Real jana yamefungwa na mchezaji ghali duniani, Gareth Bale dakika ya saba, Karim Benzema dakika ya 25 na 76 na Jese dakika ya 64.
Ushindi huo unaifanya Real itimize pointi 57 sawa na Atletico Madrid baada ya kila timu kucheza mechi 23, lakini inapanda kileleni kwa wastani wake mzuri wa mabao.
Barcelona yenye pointi 54 baada ya kucheza mechi 22, inaweza kurejea kileleni ikiifunga Sevilla leo kwa kuwa inawazidi wastani mzuri wa mabao Real na Atletico.Chanzo: binzubeiry

 

Ongeza kichwa

Jana naamini kwamba idadi kubwa wa washabiki wa ligi kuu ya Uingereza walishangaa kuona Arsenal walipata kipigo cha goli tano kwa bila dhidi ya Liverpool. Na Liverpool wamekuwa kileleni mwa dunia ya soka wikendi hii, lakini pia katika msimu huu nzima. Liverpool wamekuwa na msimu mzuri sana!
Hata hivyo, kutoka mwanzo wa msimu huu watu wengi wameamini Liverpool hawana uwezo wa kuchukua nafasi ya nne katika ligi. Liverpool hawajacheza Ligi ya Mabingwa tangu mwaka 2009! Lakini, msimu huu Liverpool wana timu ambayo naamini ina uwezo mkubwa wa kuchukua nafasi ya nne. Bila shaka Luis Suarez ni kati ya wachezaji bora katika Ligi Kuu ya Uingereza, na hata duniani! Lakini, washambuliaji wote Liverpool wameonyesha kiwango kikubwa kimpira msimu huu. Kwa mfano, Daniel Sturidge amefunga magoli 16 katika Ligi Kuu ya Uingereza!
Kitu ambacho naamini kinawasaidia Liverpool ni kwamba hawachezi katika Ligi ya Mabingwa . Kwa hiyo, tofauti na timu kama Chelsea, Manchester United, Arsenal, na Manchester City, Liverpool hawana sababu ya kupumzisha wachezaji katika Ligi ya Uingereza, na wachezaji wao hawachoki kutokana na kucheza mechi nyingi.

Mechi ya jana ilikuwa mechi ambayo niliamini kwamba Arsenal wangeonyesha kwamba kweli wana uwezo wa kushinda Ligi Kuu ya Uingereza. Ni mechi kubwa kama hii ambayo Arsenal wanahitaji kushinda kama kweli wanataka kuchukua taji la mabingwa wa Uingereza! Naamini jana Liverpool walicheza mpira mzuri sana na wa kushambulia. Lakini, sababu nyingine ambayo Arsenal ilifungwa ni ukweli wachezaji wachache walifanya makosa walipojaribu kuwakaba wachezaji wa Liverpool. Kwa mfano, Koscielny hakumkaba Skrtel vizuri wakati Liverpool walipopiga faulo katika dakika ya kwanza, na kwa hiyo, mchezaji huyu aliweza kuwafungia Liverpool goli la kwanza. Vile vile, Koscielny hakumkaba Skrtel kabisa katika corner ambayo Liverpool waliipata katika dakika ya kum, na Skrtel alifanikiwa kufunga goli lake la pili. Kocielny ni kati ya mabeki bora katika ligi kuu ya Uingereza, lakini, jana makosa yake yalisababisha Arsenal kupoteza pointi tatu.
Lakini , Arsenal bado wana nafasi nzuri ya kushinda ligi ya Uingereza. Kwa sasa wameshika nafasi ya pili nyuma ya Chelsea. Jumatano wanakutana na Manchester United. Arsene Wenger anajua, kwamba timu yake haiwezi kushinda ligi bila kushinda mechi kubwa!
Olle Bergdahl Mjengwa,
Stockholm.

KMchezaji wa Norwich City Bradley
 
Johnson akichuana vilivyo kuutafuta mpira na Alvaro NegredoKocha wa Manchester City Manuel PellegriniMMcM MMM w
 
Mchezaji wa Manchester City Pablo Zabaleta na Mchezaji wa Norwich City Bradley Johnson wakikabana huku Pablo akimbana vilivyo kwa nyuma mchezaji huyo hatari wa Norwich.
 
 
 



Mzee Wenger akiwasili  kwenye mtaa wa Liverpool Lime baada ya kibano!

 
 
 
 



 
 
 
.




Eden Hazard akishangilia..moja ya bao lakeo


MSIMAMO ULIVYO KWA SASA TIMU ZA JUU.
2013-2014 BARCLAYS PREMIER LEAGUE TABLE

OVERALL
HOME
AWAY

POS
TEAMPWDLFA
WDLFA
WDLFA
GDPts
1Chelsea2517534720
1120289
6331911
2756
2Arsenal2517444826
921226
8232620
2255
3Manchester City2517356827
1101429
6342618
4154
4Liverpool2515556330
1111389
4442521
3350

waliotembelea blog