NA KUANZIA LEO CHEGE ANA SHOOT MUSIC VIDEO YA CHAPA NYINGINE, CHINI YA DIRECTOR ADAM JUMA WA VISUAL LAB AMBAYE SIKU HIZI KWENYE VICHUPA ANAVYO VISIMAMIA HUWA ANATUMIA SIGN YA AJ BADALA YA VISUAL LAB, HII NI TANGU ATANGAZE KUACHA KUFANYA VIDEOZ MIEZI KADHAA ILIYOPITA,
Wednesday, December 18, 2013
8:05 PM
Unknown
NA KUANZIA LEO CHEGE ANA SHOOT MUSIC VIDEO YA CHAPA NYINGINE, CHINI YA DIRECTOR ADAM JUMA WA VISUAL LAB AMBAYE SIKU HIZI KWENYE VICHUPA ANAVYO VISIMAMIA HUWA ANATUMIA SIGN YA AJ BADALA YA VISUAL LAB, HII NI TANGU ATANGAZE KUACHA KUFANYA VIDEOZ MIEZI KADHAA ILIYOPITA,
8:01 PM
Unknown
Abiria zaidi ya mia mbili waliokuwemo kwenye ndege hiyo wamenusurika kifo, wanasubiri msaada ngazi waweze kushushwa.
8:23 AM
Unknown
- Hata hivyo, Waingereza ni watu makini na ambao linapokuja suala kama hilo, huweza kutumia baadhi ya nguvu kulisukumiza mbali kana kwamba haliwahusu kabisa.
KAMA siku 10 zilizopita kuliibuka habari kuhusu kashfa ya upangaji matokeo katika soka la England.
Mambo haya yamepokewa kwa mtikisiko na hisia
tofauti kwa sababu yanaweza kuathiri ile hadhi ya soka la hapa, hasa
ikizingatiwa kwamba England ndiyo nchi yenye ligi maarufu zaidi duniani.
Hata hivyo, Waingereza ni watu makini na ambao
linapokuja suala kama hilo, huweza kutumia baadhi ya nguvu kulisukumiza
mbali kana kwamba haliwahusu kabisa.
Hata katika hili, wengi niliozungumza nao wamesema
kwamba kwanza si kitu kipya katika historia ya soka, lakini wengine
wanakazia kwamba wanaohusishwa na kashfa hiyo ni wachache hivyo
washughulikiwe kikamilifu. Kuna jamaa mmoja ambaye amepata kufanya kazi
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ambaye anasema haya ni mambo sawa
na ndoto za mchana na yapuuzwe tu.
Katika madai yaliyotolewa wiki iliyopita, baadhi
ya wachezaji (bahati mbaya ni Waafrika au wana asili ya Afrika na
Singapore), wanadai kwamba walizoea kupanga matokeo kwa namna ya
kuziathiri timu zao.
Mnigeria mmoja, Sam Sodje, anasema alikuwa
akitengeneza mambo kwa kupewa fedha hadi Pauni 70,000 ili acheze faulo
mpaka aonyeshwe kadi za njano au hata nyekundu.
Lakini pia aliwashawishi wachezaji wengine ndani
na nje ya timu yake akiwa wakala wa rushwa na upangaji matokeo kisha
wakapata kulipwa, yote hayo aliyafanya katika soka la England.
Hili ni jambo linalowaumiza sana watu wa hapa, hivyo kuna wanaoshauri wote waliohusika wafungiwe maisha.
Haya mambo husanuka katika hali ya ajabu, kwa vile
awali huwa ni siri kubwa kati ya ‘wakala’ na mchezaji anayefikiwa kwa
ajili ya kuisaliti timu yake ili ifungwe.
Hata hivyo, kwa kuwa wanasema za mwizi ni 40,
mazungumzo yangu na baadhi ya wadau yanaonesha kwamba siri hii
hushindikana kufichwa kwa sababu mbalimbali.
Moja ni utoto au ulevi wa wachezaji wanaohusishwa
na kashfa hizo, ambapo hushindwa kuhifadhi vifuani mwao siri husika
wanapokuwa kwenye maeneo ya starehe.
Lakini pili, kwa hapa England suala la kamari ni kubwa japo mizizi yake mikubwa ipo kule barani Asia.
0inShare
8:08 AM
Unknown
Jaquar is one of Kenya’s highest earning
musicians and with good reason. The lad has been releasing hit after hit
and he has honestly displayed lasting power. So it comes as no surprise
that when he wants to treat himself, he spends sufficiently to by a
state of the art luxury vehicle and as I told you earlier in the year,
he settled for a Jaguar XJ
Source: Gafla Kenya
7:02 AM
Unknown

Mbunge wa Iramba Magharibi, mh. Mwigulu Nchemba leo asubuhi aliomba mwongozo wa Spika wa bunge akimtuhumu Mh. Mbowe kwamba amekuwa akitumia madaraka yake vibaya kwa kuchanganya mapenzi na kazi, hali inayolichafua bunge la Tanzania katika tawsira za kimataifa.....
Mwigulu ameliambia bunge kuwa , Mbowe alipiga simu kutaka kusitishwa kwa safari ya mbunge wa viti maalumu Chadema mkoa wa Arusha Joyce Mukya (inasemekana ni mpenzi wake) aliyekuwa ametumwa na bunge kwenda Dominica Republic kwa ajili ya kazi za bunge....

Kwa
mujibu wa Mwigulu, Joyce akiwa huko alipigiwa simu na Mbowe
akimtaka akatishe safari hiyo na badala yake aelekee Dubai kula
bata na Mbowe, kitu ambacho amedai kuwa ni matumizi mabaya ya
pesa za bunge ( posho) ...
Aidha , Mwigulu ameliomba bunge lifanye uchunguzi kuhusu posho zilizotolewa kwa mbunge huyo ambaye alikatisha safari halali ya bunge na kumfuata mpenzi wake ( Mbowe ) Dubai.
6:37 AM
Unknown
Kivuko
kikubwa cha Mv Magogoni kinachofanya safari zake kati ya Kivukoni na
Kigamboni jijini Dar es Salaam kimekosa muelekeo majini katika bahari ya
Hindi kikiwa na abiria na magari baada ya injini zake kushindwa kufanya
kazi,Mpaka sasa sababu ya injini kushindwa kufanya kazi hazijatoka.
Shuhuda anasema ‘Tulikua wanatoka Dar kwenda Kigamboni,hatua chache
kabla ya kufika Kigamboni injini zilizima,baada ya kuzima zikaja Tag kwa
ajili ya kutuvuta mpaka ng’ambo ya pili ambayo ni Kigamboni,na
ilituchukua dakika 45 mpaka kuvutwa ng’ambo ya Kigamboni’Taarifa kamili zinafata endelea kufatilia kupitia millardayo.com
6:35 AM
Unknown
USIKU huu Jumanne ni Leicester City, Timu inayocheza Daraja la Championship, kuwa Wenyeji wa Vigogo wa Ligi Kuu England, Manchester City, na Mechi ya pili ni ya Timu za Ligi Kuu England huko Stadium of Light kati ya Sunderland na Chelsea.
Edin Dzeko ameifungia bao la pili dakika za lala salama dakika ya 41 nakufanya 2-0 na kwenda mapumziko City wakiwa vifua wazi kwa bao 2.
Dakika ya 53 Edin Dzeko akafunga tena bao jingine la tatu.
Lloyd Dyer akifunga bao lao la pekee kipindi cha pili dakika ya 77 na mpira kumalizika kwa 3-1
Lee Cattermole alipojifunga dakika ya 46 na chelsea kuzawadika kwa bao hilo lililodumu kwa muda
Askari akianguka chini baaja ya kushindwa kukamata jamaa aliyeingia kifua wazi uwanjani
Shabiki alishangilia kama vile yeye kafunga bao...
Jose Mourinho na Gus Poyetwakabaki wanacheka kwa muda!! baada ya kushuhudia shabiki hilo likishangilia na kuona kama linamwongezea giza mzee Mourinho...
Dakika za majeruhi dakika ya 88 Fabio Borini akaisawazishia bao Sunderland na mtanange kuwa 1-1 na mpira kumalizika na kuongezewa muda wa dakika 30.
ROBO FAINALI
Jumanne Desemba 17
Leicester 1 v Man City 3
Sunderland 2 v Chelsea 1
LEO Jumatano Desema 18
Stoke City v Manchester United
Tottenham v West Ham United
Subscribe to:
Posts (Atom)
RSS Feed
Twitter