Friday, July 12, 2013

.

Jay Msangi ambae anaonekana katikati ameshawahi kucheza ngumi akiwa anaishi Marekani.
Taarifa ikufikie kwamba yule bondia mkongwe ambae ni mmoja kati ya waliowahi kumiliki headlines za dunia sana Evander Holyfield anatarajiwa kuja Tanzania. PromotaMtanzania Jay Msangi kutoka Hall of Fame Boxing and Promotions Company  ameongea na jovinbachwa na kumwambia hiyo game imepangwa kuchezwa Uwanja wa Taifa April 27 2014 Uwanja wa Taifa ambapo Evander atapigana na Francois Botha wa South Africa aliewahi kuwa bingwa mara mbili.





.
Evander na Francois
Jay amesema haijawa ngumu kumpata Evander kwa ajili ya pambano kwa sababu kampuni yake ina uzoefu wa miaka mingi na imeshaandaa mapambano zaidi 30 kwenye jimbo la Ohio Marekani, ni kampuni ambayo iko Marekani na hapa Tanzania. Hata hivyo kwa mara ya kwanza hii kampuni August 30 2013 itamkutanisha bondia Francis Cheka na Mmarekani Derrick atakaekua bondia wa kwanza Mmarekani kuja kupigana Tanzania. Siku hiyohiyo ya August 30 pia mabondia Mada Maugo na Thomas Mashari watashuhudiwa wakizichapa live.
 .


Maskini Irene Uwoya wetu...!!!! Inatia huzuni sana, soma hapa alichokiandika, daaah!


Kufuatia kuripotiwa kwa habari "kali" sana iliyopewa kichwa "DIAMOND AFICHUA KISA CHA KULALA NA UWOYA!" leo kuhusu mwanadada Irene uwoya na Msanii wa kizazi kipya Diamond platnumz leo na mtandao wa Global publishers, hatimaye Irene Uwoya alichukua dakika kadhaa kuandika hichi alichokiandika hapa chini....
“Kuna saa najiuliza kwanin ukimwamin mtu ndio anageuka...kwanin ukiwa muwaz watu wanakuchukulia vbaya? Leo nimeumia sanaaa kuliko skuzote...sijaamini mtu niliye mwamini kumuona kama rafiki yangu anaweza kuongea shit kuhusu mim...au najiuliza siruhusiwi kuwa na rafik wa kiume? Lakin sa nyingine nakaa chin nasema God ...u know me better”
MCHUNGUZI wa mambo anasema maneno hayo ni kutokana na kile alichokiona kama ni usaliti wa namna fulani toka kwa rafiki yake wa karibu (Jina kapuni) kuamua kumuanika hadharani mdada huyo wa bongo movies
Kama hukupata nafasi ya kuisona habari hiyo toka kwenye mtandao wa global publishers basi isome hapa kama tulivyoinukuu toka mtandao huo....

""SIRI nje! Lile skendo la Rais wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kudaiwa kulala na mwigizaji Irene Uwoya ambaye ni mke wa ndoa wa mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ limevuja.
KISA KAMILI
Huku akijua kabisa kuwa ataibua zogo kwa kuwa Uwoya ni mke wa ndoa wa mtu, kwa mara ya kwanza, Diamond ameamua kuanika kisa kilichomfanya kujiweka kwa muda kwa Uwoya.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika cha gazeti hili, kilichomfanya Diamond kufikia hatua ya kumtongoza na kutoka naye kimapenzi, ni kitendo cha Uwoya kutoa  maneno ya kumponda huku akionesha waziwazi hali ya kumchukia kila walipokutana.

UWOYA ALIKUWA HAMPENDI DIAMOND
“Unajua Irene (Uwoya) alikuwa hampendi Diamond hata siku moja na mara nyingi alikuwa kila akimuona lazima amponde. Habari hizo zilikuwa zikimfikia mwanamuziki huyo kupitia mashoga wa mwigizaji huyo ambazo ndiyo zilichochea.
“Kufuatia hali hiyo, Diamond naye kila alipofikishiwa taarifa na mashosti wa Uwoya, alikuwa akijisikia vibaya mno ndiyo maana ‘Sukari ya Warembo’ alilazimika kumvizia Uwoya kwa hali na mali ili kumfanya ampende.

CHIKOKA ATAJWA
“Nakumbuka kwa mara ya kwanza Diamond alimtuma (Juma) Chikoka ‘Chopa’ kwa Uwoya ili amfikishie ujumbe wa yeye kumtaka.
“Chikoka hakufikisha taarifa hizo, kitendo ambacho kilimuuma sana lakini siku moja Diamond alikutana na Uwoya akiwa na Chikoka, maeneo ya Sinza-Mori (Dar), akamuomba tena Chikoka namba, akampa, hapo ndipo uhusiano ulipoanzia.
 “Siku mbili baadaye Diamond alizungumza vizuri na Uwoya.

GLOBAL NOMA
“Diamond aliomba ahadi ya kukutana na mwigizaji huyo, bila kuchelewa, Uwoya aliiva na kukubali ambapo walikutana kwenye ile hoteli mliyoandika (Global) kule Mbezi Beach (Dar) wakamalizana.
“Unajua Diamond alifanya hivyo kwa sababu ya kupondwa na washikaji zake kuwa anatamba kutembea na mastaa lakini hamuwezi Uwoya.
“Kwa hiyo utagundua chanzo cha yote ni mdomo wa Uwoya kutangaza kutompenda Diamond kwani alikuwa akimsema vibaya sana kwa watu wake wa karibu,” kilidai chanzo chetu.
BOFYA HAPA KUMSIKIA DIAMOND
Baada ya kujazwa habari hizo, mwanahabari wetu alilazimika kumtafuta Diamond ili kuhakikisha kama alichoelezwa kina ukweli ndani yake ambapo bila kinyongo, mkali huyo wa wimbo wa Kesho alifunguka:
“Dah! Japo yalishapita ila ni kweli Uwoya nilikuwaga nikipata taarifa kutoka kwa marafiki zangu kuwa alikuwa ananichukia sana.
“Nilikuwa nikijiuliza sababu za yeye kunichukia lakini nikawa sizipati hata kidogo na hata nilipochunguza niligundua kweli alikuwa hanipendi kabisa.
“Sipendi sana kuzungumzia ishu hiyo ila naweza kukubali kweli kuwa marafiki zake na wangu ndiyo walionichochea sana kukutana na Uwoya na sasa hatuna tatizo na tunaishi kwa amani na upendo ingawa mengi yamepita na yaliyosemwa sina sababu ya kuyashikilia, kikubwa tumuombe Mungu.”

KAMA KAWA UWOYA HAPOKEI SIMU
Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilimwendea hewani Uwoya lakini kama kawaida, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.

TUJIKUMBUSHE
Miezi kadhaa iliyopita, gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda liliripoti habari ya Uwoya na Diamond kunaswa usiku katika moja ya vyumba vya hoteli maarufu kwenye Ufukwe wa Bahari ya Hindi huko Mbezi Beach, Dar ambapo habari hiyo iliibua maneno lakini sasa mwanamuziki huyo amemaliza utata kwani nguzo na sifa kuu ya Global Publishers ni kuandika ukweli siku zote....""

http://4.bp.blogspot.com/-uWuH_yP6DAA/Ud-rDUX3WOI/AAAAAAAAi7o/JnALffiLZB4/s1600/1.png


 SERIKALI imesisitiza kuwa itatoza Sh 1,000 kwa kila kadi ya simu inayotumika lakini pia inaangalia utaratibu wa kufanya makato hayo kwa njia ambayo haitamuumiza mtumiaji wa simu.


Akizungumza jana jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa alisema kuwa kupitia tozo hizo wanatarajia kukusanya Sh bilioni 160 kwa mwaka.

“Kupitia wawakilishi wenu na sisi serikali kuwa sikivu, tulishauriwa na ikaonekana kwamba kuna uwezekano wa kupata chanzo kingine cha mapato kupitia kadi za simu”alisema.



Alisema katika mapendekezo yaliyokuwa yametolewa serikali ilishauriwa kutoza Sh 1,450 katika kila kadi ya simu lakini baada ya kukaa na kushauriana serikali iliona ni vyema ikatoza Sh 1,000 ili kila mwananchi aweze kumudu gharama ambapo kwa mwaka kila mmiliki wa kadi ya simu atatozwa sh 12,000.


Alisema baadae serikali ilipokea mapendekezo mbalimbali ili kuangalia kama hilo linaweza kutekelezeka na walipita ngazi zote kabla halijapelekwa katika kamati za Bunge na kushauriwa kwamba tozo hilo linaweza kufanyika kwa lengo la kukuza uchumi hasa maeneo ya vijijini.

 
“Tathmini zote zimefanyika kikamilifu na baadae suala hilo likafikishwa Bungeni ambapo pia napo lilikubalika... inawezekana watu wanalalamika lakini ngazi zote suala hilo lilipopita lilikubalika na ikaonekana ni sawa kutozwa sh 1,000 kwa kila kadi ya simu” alisema.



Alisema kutokana na hilo kwa kutwa nzima kadi ya simu itatozwa Sh 33.35 au Sh 100 kwa siku tatu ambapo serikali inaangalia utaratibu mzuri ambao hautamuumiza mtumiaji wa simu.


Dk Mgimwa alisema fedha hizo zitakazokusanywa zitaongeza upatikanaji wa maji vijijini, umeme pamoja na kuboresha miundombinu katika maeneo ya vijijini.

 
HUKU skendo ya kunaswa akiwa na madawa ya kulevya ikiendelea kumtesa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ anatarajiwa kupandishwa kortini nchini Afrika Kusini leo kujibu shitaka ambalo mwenyewe hajaliweka wazi.
Kwa mujibu wa habari ya mjini, wawili hao walinaswa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oriver Tambo uliopo Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania wakiwa na ‘mzigo’ wa kilo nyingi aina ya ‘crystal methamphetamine’ wenye thamani ya shilingi za Kitanzania bilioni 6.8!
Mtu mmoja wa karibu na Masogange alipoulizwa kuhusu ukweli au uongo wa habari hiyo alikuwa na haya ya kusema:
Ni kweli Agnes amekamatwa akiwa na madawa ya kulevya kule Sauzi. Lakini si yenye thamani hiyo ya bilioni sita bali ni milioni arobaini tu. Hata hivyo, ameachiwa kwa dhamana ila paspoti yake imezuiliwa.
“Nadhani kuna mambo yanawekwa sawa ikiwezekana atarudi nyumbani.”
 

KAMANDA WA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA ANENA
Jumatatu iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliviambia vyombo vya habari kuwa, Watanzania wawili walikamatwa nchini Afrika Kusini na mamlaka ya mapato wakiwa na madawa ya kulevya kutoka Tanzania yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Kamanda Nzowa aliwataja Watanzania hao kuwa ni Agnes Gerald ambaye ana miaka 25 na Melisa Edward mwenye miaka 24. Alisema wawili hao baada ya kukamatwa na chombo hicho walikabidhiwa kwa polisi ambapo mahojiano yanaendelea. 

 
 Mpaka hapo, timu nzima iliyokuwa ikifuatilia habari hiyo haikuona ukweli wa Agnes Gerald kuwa ni Masogange na kwa vile siku zote Global Publishers inasimamia utafiti kabla ya kuandika habari iliamua kuiweka pembeni kwanza ili kuendelea kuichimba.
Saa 2:14 usiku wa siku hiyo, Ijumaa lilipokea simu yenye kuashiria wito (code number) ni ya nje na kabla haijapokelewa, ilibainika ni ya Afrika Kusini.
Ijumaa: Haloo.
Sauti: Haloo, mimi Masogange.     
Ijumaa: Mambo Agnes, pole sana na mkasa uliokupata bwana, pole sana.
Agnes: Kwanza naumizwa sana na maneno ambayo watu wanazidi kuyaeneza sehemu mbalimbali bila kuwa na uhakika wowote, mimi sikukamatwa kwa sababu ya madawa ya kulevya.
“Mkasa nilioupata siyo ambao watu wanaueneza kwenye mitandao mbalimbali na katika vyombo ya habari.”

Ijumaa: Kwa hiyo madai ya kukutwa na madawa ya kulevya si ya kweli?
Agnes: Kweli nilikamatwa huku kwa matatizo f’lan ila siyo ishu ya madawa kama watu wanavyosambaza.
Ijumaa: Ni tatizo gani sasa?
Agnes: Unajua sipendi tena kuwapa watu faida ila lilikuwa ni tatizo la kawaida, nilikamatwa na baada ya hapo nilitoka na niko huru. Nasubiri tu kwenda mahakamani Ijumaa (leo) mara moja kisha n’tarudi Bongo.
Ijumaa: Mh! Sasa Egg, mbona huku mpaka viongozi wa polisi wamesema ni madawa?
Agnes: Hapana, siyo, ipo ishu ndogo tu.
Ijumaa: Haya pole sana kwa misukosuko.
Agnes: Asante sana, nitakuja huko siku si nyingi.
Habari hii imeandikwa na Imelda Mtema, Haruni Sanchawa na Musa Mateja.

 
 






 
 
Kuna saa najiuliza kwanin ukimwamin mtu ndio anageuka...kwanin ukiwa muwaz watu wanakuchukulia vbaya? Leo nimeumia sanaaa kuliko skuzote...sijaamini mtu niliye mwamini kumuona kama rafiki yangu anaweza kuongea shit kuhusu mim...au najiuliza siruhusiwi kuwa na rafik wa kiume? Lakin sa nyingine nakaa chin nasema God ...u know me better” alifunguka Uwoya. Sababu kubwa iliyodaiwa kumfanya Diamond atembee na Uwoya ni kitendo cha muigizaji huyo kudaiwa kumponda mara kwa mara na alikuwa hampendi Diamond ambaye alikuwa anafikishiwa habari hizo na marafiki zake Irine.

  
Emmily Omari akiwa selo.


 MREMBO mwenye ulemavu wa ngozi, Emmily Omari, 23, mkazi Buguruni, Dar anayedaiwa kujihusisha na biashara haramu ya uchangudoa, hivi karibuni alipandishwa kizimbani kwa madai ya kufanya kosa hilo.

Emmily ambaye amekuwa akiwatesa askari polisi ambao wamekuwa wakimkamata mara kwa mara na kumfikisha mahakamani lakini haachi tabia hiyo, alipandishwa katika Mahakama ya Jiji na kusomewa mashtaka yake.
Hakimu aliyekuwa akiendesha kesi hiyo, Timothy Lyon alipigwa butwaa kumuona mrembo huyo ambaye aliwahi kumhukumu zaidi ya mara tano kwa kosa la kujiuza na kumuachia huru baada ya kulipa faini.
Pilato huyo baada ya kumuona tena Emmily mbele yake akikabiliwa na shitaka lilelile, alimuuliza alikuwa na tatizo gani lililosababisha mara kwa mara afikishwe mahakamani hapo, mrembo huyo hakujibu chochote.
“We Emmily sasa unatuletea utani, kila siku unaletwa hapa tunakupiga faini unalipa unatoka na kwenda kurudia hiyo biashara yako… sasa tunaona kama unatufanyia masihara  sasa leo hakuna cha faini wala dhamana uende Segerea ukale dona la bure labda utajifunza,” alisema Hakimu Lyon na kuwaamuru askari wampandishe kwenye Karandinga kwa ajili ya safari ya gerezani.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana juzikati zinaeleza kuwa mrembo huyo baada ya kukaa Segerea kwa wiki mbili, alipewa dhamana wakati mahakama ikiendelea kumjadili.






























Dar es Salaam. Serikali imetangaza viwango vipya vya chini vya mishahara kisekta ambavyo vinatofautiana kati ya sekta moja na nyingine ambavyo ni kuanzia Sh40,000 hadi Sh400,000 kwa mwezi kuanzia Julai Mosi mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema, watakaolipwa kima kidogo zaidi cha Sh40,000 ni wafanyakazi wa nyumbani ambao wameajiriwa na watu wa kawaida huku wakiishi kwenye nyumba za waajiri wao.
Kwa upande mwingine, katika viwango hivyo, kima kikubwa katika viwango hivyo cha Sh400,000 kitalipwa kwa wafanyakazi wa sekta za mawasiliano zikiwamo kampuni za simu, kampuni za kimataifa za nishati, madini na taasisi za fedha.
Katika viwango hivyo, mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na watu wa kawaida lakini ambao hawaishi kwenye nyumba za waajiri wao itakuwa Sh80,000.
“Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na mabalozi wa kigeni na wafanyabiashara maarufu wanatakiwa kulipwa Sh150,000 kwa mwezi,” ilisema taarifa hiyo.
Wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na maofisa wa Serikali watalipwa Sh130,000 kwa mwezi.
Kima cha chini cha mshahara katika huduma za kilimo ni Sh100,000 na huduma za afya Sh132,000.
Kwa upande wa wafanyakazi wa vyombo vya habari, posta na usafirishaji wa vifurushi ‘courier services’, kima cha chini kitaanzia Sh150,000.
Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa hoteli za kitalii kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ni Sh250,000, wakati kwa hoteli za kati ni Sh150,000 na migahawa, nyumba za wageni na baa ni Sh130,000.
Kampuni za ulinzi za kimataifa zitapaswa kulipa kiwango cha chini cha mishahara cha Sh150,000 kwa wafanyakazi wake sawa na kampuni ndogo za huduma za nishati.  Kampuni ndogo za ulinzi zitatakiwa kulipa Sh100,000.
Kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga kitakuwa Sh300,000, sawa na wale wa utoaji na uingizaji wa mizigo. Wafanyakazi wanaofanya katika sekta ya usafirishaji wa majini, uvuvi na nchikavu wakitakiwa kulipwa Sh200,000.
Kima cha chini kwa kampuni za makandarasi daraja la kwanza kitakuwa Sh325,000, makandarasi daraja la pili hadi la nne Sh280,000 na makandarasi daraja la tano hadi saba Sh250,000.

waliotembelea blog