Siku
chache baada ya kuachia video ya wimbo wake - ‘NINGEFANYAJE’, muimbaji
wa R&B kutoka Tanzania, Bernard Paul maarufu kama Ben Pol ameeleza
sababu zilizopelekea muimbaji Avril kutoka Kenya aliyeshirikishwa
kwenye wimbo huo, kutoonekana kwenye video hiyo anayoitaja kuwa kubwa
kuliko video zote alizowahi kufanya.
Katika
video hiyo iliyoongozwa na Justin Campos wa Afrika Kusini, Ben Pol
anaonekana akiimba na Rossie M ambaye pia ameshirikishwa kwenye wimbo
huo huku mashabiki wakiisikia sauti ya Avril bila kumuona mwimbaji huyo
mrembo.
Ben
Pol amewaomba radhi mashabiki wake kwa kuwapa video ambayo
haijakamilisha wahusika wote hususan kutokuonekana kwa Avril, na kwamba
sababu zilizopelekea hivyo zilikuwa nje ya uwezo wa pande zote katika
utayarishaji wa video hiyo.
Ben
amesema kuwa baada ya yeye na Rossie M kuwasili Afrika Kusini
ilikoshutiwa video hiyo, zilijitokeza changamoto muda mfupi kabla ya
kuanza zoezi hilo. Ben Pol ameeleza kuwa pamoja na kuwa na maandalizi
makubwa, video ya ‘Ningefanyaje’ ilikumbwa na changamoto nyingi tangu
awali zilizopelekea kuahirishwa mara tatu.
“Kwa
kweli hii video tokea mwanzo ilikuwa na changamoto, kwanza tuliisogeza
mbele karibu mara tatu tena tukiwa tayari tumeshafika Afrika Kusini mimi
na Rossie,” alisema Ben Pol. “Mara ya kwanza ni kutokana na ‘delay’ ya
viza upande wa Avril. Si unajua Wakenya wao wanaenda South kwa viza
tofauti na sisi Tanzania hatuendi kwa viza so kwetu ni rahisi zaidi muda
wowote tu ukiamua fasta unaenda,” aliongeza.
Mkali
huyo alieleza kuwa baada ya terehe mpya kupangwa na muongozaji
aliyeshuti video hiyo, Justin Campos, siku moja kabla ya kushuti, AVRIL
alipata tatizo lingine ambalo lilimzuia kusafiri kwa siku iliyofata
kwenda Afrika Kusini.
Wakati
huo huo, Campos naye alimueleza Ben Pol kuwa kwa jinsi ratiba yake
ilivyo endapo ataahirisha tena kushuti video hiyo, ratiba yake
isingemruhusu kushuti video hiyo hadi Januari au Februari 2016, kitu
ambacho Ben Pol amesema kisingewezekana kwasababu ingeendelea
kumgharimu zaidi kifedha na kuvuruga ‘timing’ yake.
“Kutokana
na hali hiyo, sikuwa na jinsi nyingine zaidi ya kukubali matokeo
kwasababu mwisho wa siku si mimi wala Avril wala director aliyekwamisha
bali ni ‘situation’ ambayo ilikuwa nje ya uwezo wa kibinadamu.” Ben Pol
anaeleza.
Ameongezea
kuwa pamoja na kwamba angeweza kuamua kushuti video kwa kutumia version
nyingine ya wimbo huo isiyokuwa na sauti ya Avril ili video isionekane
na upungufu wake, lakini hakupenda kufanya hivyo kwa kuwa lengo kuu la
wimbo lilikuwa kumshirikisha mwimbaji huyo. Pia, mashabiki wangekosa
ladha nzuri na kazi nzuri aliyoifanya Avril. Hivyo, aliamua kufanya
video hiyo bila Avril na kukusudia kuwaeleza mashabiki wake
kilichosababisha hali hiyo kwa kuwa aliamini mashabiki wataelewa magumu
aliyopitia katika kuwapa video hiyo waliyokuwa wakiisubiri.
“Namshukuru
sana Avril kwa kukubali kufanya kazi na mimi kwasababu imetimiza moja
kati ya malengo yangu ya 2015, ambayo ilikuwa kuanza kufanya kazi na
wasanii wa nje ya Tanzania na yeye ndiye alikuwa chaguo langu la kwanza.
Ni imani yangu tutafanya tena project nyingine ya pamoja na
kuikamilisha kama tulivyoikusudia,” alimaliza Ben Pol na kuwashukuru
mashabiki wake kwa kuupokea kwa mtazamo chanya wimbo na video yake.
0 maoni:
Post a Comment