Zlatan Ibrahimovic atakuwa nyumbani katika mji wa Malmo, Sweden wakati atakapokuwa na timu yake…lakini mashabiki wa nyumbani wameamua kuonyesha heshima kubwa kwake kwa kumkaribisha kwa staili ya aina yake ikiwa ni miaka 14 tangu aihame timu hiyo ya nyumbani.
Moja ya makumbusho ya jengo lililojengwa mwaka 1546 mjini Malmo ambapo kumeandaliwa tafrija ya kumpokea Zlatan.
Zlatan amewaambia mashabiki wa Malmo wanaweza kuimba jina lake kama walivyokuwa wakifanya awali wakati akiitumikia timu hiyo.
Malmo ndiyo ilikuwa timu yake ya kwanza kubwa iliyomkuza kisoka kabla ya kununuliwa na Ajax ya Uholanzi.
0 maoni:
Post a Comment