Meneja wa Mawasiliano Efm, Denis Ssebo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kumpata mshindi wa shindano la kubuni maneno ya Kanga kupitia kipindi
cha UHONDO ambacho huruka hewani kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa
kuanzia saa sita mchana hadi saa tisa alasiri, kikiwa na Matangazaji
mahiri Dina Marios, kikao hicho kimefanika leo jijini Dar es Salaam,
katikati ni mshindi wa shindano hilo Sekela Richard na wakulia ni
Matangazaji wa Efm Radio Dina Marios.
Matangazaji mahiri Dina Marios, akimkabidhi kitita cha shilingi Kitanzania milioni moja. mshindi wa shindano hilo, Sekela Richard kulia ni Meneja wa Mawasiliano Efm, Denis Ssebo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja wa Mawasiliano Efm, Denis Ssebo
Picha na Emmanue Massaka.
MENEJA wa Mawasiliano Efm, Denis Ssebo shindano
hilo halitaishia hapo, kwani baada ya kupata mshindi neno lake la
Ushindi zitatengenezwa kanga zitakazoandikwa neno hilo ikiwa ni hatua
ya pili sasa ya kumwezesha mwanamke kujikwamua kiuchumi.
Zikishatengenezwa kanga hizo, Efm kupitia
kipindi hicho cha Uhondo, itatatoa nafasi kwa wanawake kutengeneza
pesa na kujikwamua kwa kuuza Kanga hizo na Mwanamke yoyote hasa kwa
Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani atachukua kanga hizo na kuziuza ambapo
kwa kila doti moja ya kanga atapata asilimia 30% ya pesa.
0 maoni:
Post a Comment