
5:07 AM

Unknown
Felipe
Pardo aliipa Olympiakos Bao la kuongoza lakini Theo Walcott
akaisawazishia Arsenal ambao walikwenda Mapumziko wakiwa nyuma 2-1 baada
ya Kipa wao David Ospina kujifunga mwenyewe.
Kipindi
cha Pili, Arsenal walisawazisha Dakika ya 65 kwa Bao la Alexis Sanchez
lakini Dakika 1 baadae Olympiakos walifunga Bao la 3 na la ushindi wa
3-2 kupitia Alfred Finnbogason.
Hii ni Mechi ya pili mfululizo kwa
Arsenal kuchapwa katika Kundi F baada kupigwa 2-1 na Dinamo Zagreb na
sasa wana kibarua kigumu cha kufuzu na kuwa Timu ya kwanza kufanya hivyo
tangu Msimu wa 2012/13 tangu Galatasaray walipofungwa Mechi mbili za
kwanza na kuweza kusonga hatua ya Mrtoano ya UCL.
Ili kufanya hivyo, Arsenal inabidi kwanza washinde Mechi zao mbili zinazokuja na zote ni dhidi ya Bayern Munich.
Arsenal
wakubali yaishe! wapigwa bao 2-1, Wafungaji bao za Olympiakos ni Felipe
Pardo 33' David Ospina 40' OG na Alfred Finnbogason 66. Bao za Arsenal
zilifungwa na Theo Walcott dakika ya 35 na lile la Alexis Sánchez dakika
ya 65 na mtanange kumalizika kwa 3-2 Olympiakos wakiibuka kidedea
Emirates!

Arsenal v Olympiakos
0 maoni:
Post a Comment