Mashindano
ya maarufu ya urembo duniani, Miss Universe, sasa yatakuwa chini ya
kampuni ya kusaka, kuendeleza vipaji na masoko ijulikanayo kwa jina la
WME/IMG.
Awali
mashindano hayo yalikuwa yakiendeshwa kwa ushirika baina ya kampuni
hiyo na kampuni inayojishughulisha na masuala ya habari na burudani ya
NBCUniversal na mtangazaji maarufu wa vipindi vya televisheni,
mwanasiasa na mfanyabiashara, Donald J Trump.
Akizungumza
jijini jana, Mwandaaji wa mashindano ya Miss Universe Tanzania, Maria
Sarungi Tsehai alisema kuwa wamepokea taarifa kuhusiana na kampuni mpya
hiyo ambayo pia inaandaa mashindano ya Miss USA na Miss Teen Usa.
Maria
ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Compass Communications
alisema kuwa wamepokea mabadiliko hayo na wataendelea kufanykazi na
mmiliki huyo mpya ili kuendeleza vipaji vya wasichana nchini.
Alisema
kuwa mashindano ya Miss Universe ni moja kati ya matukio makubwa ya
burudani duniani ambayo usaidia wasichana kutoka nchi zaidi ya 190
zinazoshiriki kila mwaka na watu zaidi ya nusu bilioni kufuatilia
mashindano hayo kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao na televisheni.
“Kwa
sasa tupo katika maandalizi ya kufanya mashindano ya Miss Universe
Tanzania, tunaamini kuwa mabadiliko haya yatatupa changamoto zaidi kwa
lengo la kufika mbali na zaidi kuhakikisha tunatwaa taji baada ya
matokeo mazuri ya Flaviana Matata ya mwaka 2007 ambapo aliingia hatua ya
10 bora,” alisema Maria.
Afisa
Mkuu wa kampuni ya WME/IMG, Mark Shapiro ameahidi kuyaendeleza
mashindano hayo kufika ngazi ya juu kabisa ikiwa pamija na washindano
bora.
"Najisikia
faraja kuendshs mashindano haya, tutayaendeleza kwa kiwango kikubwa na
kuhakikisha umaarufu wake unaongezeka, naamini mashabiki wengi zaidi kwa
sasa watafuatilia mashindano yetu kwa njia ya mbalimbali,” alisema
Shapiro.
Maria Mwandaaji wa mashindano ya Miss Universe Tanzania, Maria Sarungi Tsehai alizungumza katika mashindano yaliyopita.
Miss Universe Tanzania 2014 Caroline Bernard akitoa elimu ya afya kwa wanafunzi wa kike katika shule ya msingi Msimbazi Mseto
0 maoni:
Post a Comment