Marais wengi wa Afrika wamekuwa wakikaa kwa muda mrefu madarakani
hali inayochangia baadhi ya nchi kuingia katika machafuko wa kisiasa.
Ukongwe wao kwenye siasa umewafanya wengi wao kujikuta wakikaa miaka
mingi zaidi na kuvunja rekodi ya kukaa madarakani kwa muda mrefu.
Hapa nimekuwekea list ya Marais wa Afrika wenye umri mkubwa zaidi ya wengine…
1. Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ana miaka 91, ndiye Rais mzee kuliko wote, ameshinda urais kwa muhula wa saba
2. Beji Caid Essebsi-Ana miaka 88, amekua Rais wa Tunisia tangu Desemba 31 2014
3. Rais Paul Biya wa Cameroon ana miaka 82,ameingia madarakani tangu mwaka 1982
4. AbdelAziz Boeteflika ni Rais wa Algeria toka April 1999, ana miaka 78
5. Rais wa Guinea Alpha Conde ana miaka 77, amekua madarakani tangu Desemba 2010
6. Rais wa visiwa vya Sao Tome Manuel Pinto da Costa ana miaka 77, aliingia madarakani tangu mwaka 2011
7. Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ana miaka 76, aliingia madarakani tangu Januari 2006
8. Rais wa Malawi Peter Mutharika ana miaka 74, aliingia madarakani May 2014
9. Rais wa Ivory Coast Alassane Quattara ana miaka 73, aliingia madarakani tangu mwaka 2011
10. Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ana miaka 73, aliingia madarakani tangu May 9, 2009
0 maoni:
Post a Comment