MSHAMBULIAJI
Carlos Tevez amepata mapokezi mazuri akirejea klabu yake iliyoumuibua
kisoka nchini Argentina, Boca Juniors baada ya kulakiwa na mashabiki
zaidi ya 40,000 akiwemo gwiji mwingine wa klabu hiyo, Diego Maradona
Uwanja wa Bombonera
Akiwa
amevalia jezi namba 10 aliyokuwa anavaa kabla ya kuondoka Boca kuhamia
Corinthians mwishoni mwa mwaka 2004, ambako nyota yake iling'ara zaidi
na kuwa mchezaji mkubwa duniani akitamba klabu za West Ham United,
Manchester United, Manchester City na Juventus, Tevez aliwafurahisha mno
Boca.
Aakitazama
kutoka jukwaani juu katika boksi, Maradona alining'iniza bango
lililoandikwa 'Asanye kwa kurejea, Carlitos", kabla ya kumfuata chini
Tevez na kusalimiana naye. Tevez baadaye alipiga magoti kubusu Uwanja
ambako aliukanyaga kwa mara ya kwanza mwaka 2001 akiwa ana umri wa miaka
18 tu.
Tevez waves to a selection of the 40,000 supporters who turned up to welcome the Argentina international back to the club
0 maoni:
Post a Comment