Mashindano ya CECAFA Kagame Cup ni mashindano makongwe barani Afrika ambayo yalianza mwaka 1967 kwa kushirikisha timu za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, na mwaka huu ni mashindano ya 40 tangu kuanza kwa michuano hiyo
Klabu ya Simba ndio timu inayoongzoa kwa kutwaa ubingwa huo mara sita (6) ikifuatiwa na Yanga, Gor Mahia zilizotwa mara (5), APR ya Rwanda ikiwa imetwaa ubingwa huo mara tatu (3). Yanga na Gor Mahia zina nafasi ya kufikia Simba SC endapo zitafanikiwa kutwaa Ubingwa msimu huu.
Mechi ya ufunguzi ufunguzi siku ya jumamosi uwanja wa Taifa itawaktanisha APR ya Rwanda dhidi ya Al Shandy ya Sudan saa 8 kamili mchana, KMKM kutoka Visiwani Zanzibar watacheza dhidi ya Telecom ya Djibout uwanja wa Karume saa 10 jioni, huku wenyeji timu ya Yanga wakiwakaribisha Gor Mahia kutoka Kenya saa 10 jioni.
Kuelekea kwenye mashindano hayo, waandaji wa michuano hiyo CECAFA kwa kushirikiana na wenyeji Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya michezo hiyo, ambapo Uwanja wa Karume kiingilio kitakua shilingi elfu mbili (2,000) na uwanja wa Taifa kiingilio cha chini kitakua ni shilingi elfu tano (5,000) na kiingilio cha juu ni elfu 20,000 (20,000).
Timu zinazoshiriki michuano hiyo
Kundi A: Yanga (Tanzania Bara), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar), Khartoum-N (Sudan).
Kundi B: APR (Rwanda), Al-Shandy (Sudan),LLB AFC (Burundi), Heegan FC (Somalia).
Kundi C: Azam FC (Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na KCCA (Uganda).
Michuano hiyo ya CECAFA Kagame Cup itaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha Supersport.
0 maoni:
Post a Comment