KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mart Nooij, amesema atatumia kambi ya Ethiopia kujiandaa na mchezo wa Misri kwani vijana wapo katika hali nzuri na wameahidi kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo.
Mart Nooij aliyasema hayo leo wakati ametangaza kikosi cha wachezaji 23 walioondoka jana jioni kuelekea Addis Ababa Nchini Ethiopia kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri
“Nitatumia kambi ya Ethiopia kujiandaa na mchezo wa Misri, kwani wachezaji wapo katika hali nzuri na wameahidi kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo na baadae kufuzu katika fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017”, alisema Nooij
Mchezo kati ya Misri na Tanzania wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017
unatarajiwa kuchezwa Juni 14, katika uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria.
Kikosi cha Stars kiliondoka jana saa 11 jioni kwa Shirika la ndege la Ethiopia ambapo kitawasili jiji la Addis Ababa majira ya saa 1 jioni kwa saa za Afrika Mashariki kina wachezaji 23, benchi la ufundi la watu wanne na wajumbe wawili wa kamati ya Utendaji ya TFF ambao ni Vedastus Lufano na Geofrey Irick Nyange “Kaburu”.
0 maoni:
Post a Comment