Mapema
wiki hii millardayo.com iliandika stori ya ajali ya lori la mafuta kuua
zaidi ya watu 90 Nigeria ikiwa ni baada ya kuwa kwenye mwendo mkali na
kugonga watu na magari yaliyokuwa kwenye kituo cha abiria.
Lakini
leo Ghana nayo imeingia kwenye headlines baada ya kituo cha mafuta
kulipuka na kuua watu wanaokadiriwa kuzidi 90 katika mji mkuu wa nchi
hiyo Accra.
Mlipuko
huo umetokea baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko katika maeneo
mengi ya mji huo ambapo pia imewaacha watu wengi bila makazi huku sehemu
kubwa ya mji ikiwa gizani kutokana na kukatika kwa umeme.
Idadi
ya watu waliofariki huenda ikaongezeka kwani watu wengi wamepoteza
maisha baada ya kuwepo kituoni hapo wakijikinga na mafuriko yaliyotokea
na huenda idadi ikaongezeka kutokana na baadhi ya miili kuwa bado
haijapatikana.
0 maoni:
Post a Comment