Licha ya kutotwaa Taji lolote Msimu uliopita, Man United imeiengua Bayern Munich na kukamata Nafasi ya Kwanza kwa kuwa ndio Bidhaa ya Biashara yenye thamani kubwa ikikadiriwa kuwa ni Dola Bilioni 1.2 na hii ni kwa mujibu wa takwimu za Washauri mahsusi wa Bidhaa na Fedha, Brand Finance.
Katika Listi iliyotolewa na Washauri hao wa Bidhaa na Fedha, Klabu 6 katika 10 Bora Duniani ni za England.Barcelona, ambao Juzi Jumamosi walitwaa Kombe la UEFA CHAMPIONS LIGI, wameporomoka Nafasi 2 na sasa wapo Nafasi ya 6.
Msimu 2014/2015 Klabu ya Barcelona imetwaa makombe matatu(Treble) na hapa ni jana wakati wanatembeza makombe hayo Mtaani!Ingawa Magazeti ya Spain yamekuwa yakivutia upande wa Klabu zao na kudai Man United, kwa kukosa Mataji, imepoteza Mashabiki wengi Duniani, Ripoti ya Brand Finance imesema: "Hata kama ripoti hizo za kupoteza Mashabiki itaaminika, Man United bado ina Maelfu ya Washabiki huko India, Kusini Mashariki ya Asia na China, ikijumuisha zaidi ya Nusu Bilioni ya Watu na habari hizo hazijawakimbiza Wadhamini."
Brand Finance imesema kuwa kwa kusaini Dili na Wadhamini kama Chevrolet na Adidas, ambao walisaini nao 2014 kwa Dau la Pauni Milioni 750 kwa Miaka 10, ni vitu tosha kuthibitisha thamani ya Klabu hiyo na kwamba thamini yao itapanda zaidi kama ilivyopanda kwa Asilimia 63 tangu 2014.
KLABU 20 BORANA THAMANI YAKE!
1. Manchester United (England): $1206 Milioni
2. Bayern Munich (Germany): $933 M
3. Real Madrid (Spain): $873 M
4. Manchester City (England): $800 M
5. Chelsea (England): $795 M
6. Barcelona (Spain): $773 M
7. Arsenal (England): $703 M
8. Liverpool (England): $577 M
9. Paris Saint-Germain (France): $541 M
10. Tottenham Hotspur (England): $360 M
0 maoni:
Post a Comment