Good news ninayotaka kukusogezea ni
kwamba Msanii wa Bongo Fleva Ali Kiba, Jacqueline Ntubaliwe , Vanessa
Mdee wameamua kuungana na shiriki la kimataifa liitwalo WildAid ili kupiga vita ya ujangili na biashara ya pembe za ndovu.
Uzinduzi wa kampeni hiyo ulifanyika katika hoteli ya Sea Cliff na kuhudhuliwa na waziri wa Maliasili na Utali, Lazaro Nyalandu na wakiwemo mabarozi wa china na marekani.
Akizungumza na waandishi wa habari Ali Kiba alisema ‘Nashukuru
kwanza nilipata nafasi ya kuishi na tembo porini kwa muda wa siku wa
tatu kwa hiyo kiukweli lazima uogope maana mimi ni muoga nambari moja,
ila nilichokuwa nafikiria ni tofauti na vile nilivyodhani ila tembo ni
wanyama wazuri
Vile
vile nilipata nafasi ya kwendaNairobi kuwatembelea watoto wa tembo
yatima mama zao wameuliwa na watu wasio na imani ukifikiri kibinadamu
wanyama ni viumbe kama sisi, kuna wale ambao tumeruhusiwa kula lakini
sio kwa wale ambao ni fahari kwetu sisi ni vivutio vinaipa nchi yetu
thamani, wageni wanakuja kuona hao hao wanyama wetu lakini watu wanawaua
kwasababu unavyowatoa ndovu zao ni sawa sawa unawatesa wanaumia
kiukweli mimi napiga vita hivi vya ujangili lakini kutokana na imani na
kutaka Tembo hao wanapata watetezi ambao ni sisi, mimi na yoyote kwani
wale ni kama raia na pia wana haki ya kuishi ndio maana tukiwa na
mapenzi nao tunaenda kuwaona, kwa hiyo mimi hili suala nimelipokea kwa
mikono miwili na nimefuraha kuwa balozi wa WildAid, nimetembelea sehemu
nyingi kama Tarangire na bado nitaendelea kutembelea na wengine
mnakaribishwa kutembelea hifadhi za wanyama.
Kwa
hiyo na imani mimi na wasanii wengine ambao tunaweza tukatimia nguvu hii
ya pamoja, Jacqueline Mengi na Vanessa Mdee kwakweli tuko mbele juu ya
suala hili, ningependa sana watanzania tushirikiane katika jambo hilo
unapoona tukio hilo limetokea basi toa taarifa mapema kwani ujangili
unatuumiza sisi sote…..’alisema.
0 maoni:
Post a Comment