Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro
Premium Lager, kesho inatarajiwa kushuka dimbani kucheza na timu ya
Taifa ya Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainaili za
wachezaji wa ndani CHAN 2016.
Kikosi cha Taifa Stars kimeendelea
na mazoezi katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo
huo utakaopigwa kuanzia majira a saa 2 usiku kwa saa za Afrika
Mashariki.
Stars inahitaji ushindi katika
mchezo huo wa awali ili kujiweka katika mzingira mazuri ya kusonga
mbele, kabla ya mchezo wa marudaino utakaofanyika baada ya wiki mbili
jijini Kampala.
Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart
Nooij amesema vijana wake wako katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo
wa kesho, na kuwaomba watanzania kuwapa sapoti katika mchezo huo.
Endapo Stars itaitoa Uganda katika
hatua ya awali, itafuzu katika hatua ya pili ambapo itacheza dhidi ya
timu ya Taifa ya Sudan, na mshindi wa mchezo huo moja kwa moja atafuzu
kwa fainali za CHAN 2016 nchini Rwanda.
Wakati huo huo, timu ya Taifa ya
Uganda (The Cranes) inatarajiwa kuwasili leo mchana jijini Dar es salaam
kisha kuelekea kisiwani Zanzibar tayari kwa mchezo huo wa kesho dhidi
ya Taifa Stars.
TWFA KUFANYA UCHAGUZI AGOSTI 15
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi
wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA), George Mushumba
ametangaza uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika agosti 15, 2015
kujaza nafasi mbalimbali.
Kwa mamlaka aliyonayo anapenda
kutangaza uchaguzi mkuu wa TWFA leo kwa ajili ya kujaza nafasi
zilizoachwa wazi, uchaguzi huo utafanyika tarehe 15, Agosti 2015 katika
nafasi zifuatazo:
- Mwenyekiti
- Katibu Msaidizi
- Mweka Hazina
- Wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji.
Fomu za kuomba nafasi hizo zitaanza kutolewa tarehe 19-23 Juni 2015 katika ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF
0 maoni:
Post a Comment