Monday, June 29, 2015

WENYEJI Chile wametinga fainali ya Copa America 2015 kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Peru usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Taifa mjini Santiago: Kwa ushindi huo, fainali Chile sasa itakutana na mshindi kati ya Argentina na Paraguay zinazomenyana usiku wa kuamkia kesho. Eduardo Vargas aliifungia bao la kwanza akimalizia krosi ya Alexis Sanchez dakika ya 42. Carlos Zambrano alitolewa...
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea akizungumza na wanamichezo (hawapo pichani) kabla ya kuanza fainali ya Kombe la Chikawe katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya Black Fire kutoka Kata ya Marambo na Timu ya Motisha kutoka Kata ya Kilimanihewa zilipambana na Timu ya Black Fire iliibuka mshindi kwa magoli 3...
  Baadhi ya Wanamichezo wa Polisi walioshiriki Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika mwaka 2013 nchini Namibia wakiwa katika picha. Timu za Jeshi la Polisi Tanzania zitakazoshiriki michezo ya Umoja wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO),  mwishoni mwa mwezi julai nchini Swaziland...

Sunday, June 28, 2015

Morgan Schneiderlin atakuwa ni wa pili kusajiliwa na klabu ya Manchester United Msimu 2015/2016 na atajiunga na Mashetani wekundu wiki ijayo Jumatano Dirsha la Usajili litakapofunguliwa rasmi.  Manchester United wamekamilisha usajili huo kwa kutoa kitita cha £25million kwa Morgan Schneiderlin – na taarifa zaidi kutoka Klabuni humo zinadai kuwa usajili unaendelea na ambao wamewaweka...
Mshambuliaji Samuel Eto’o amejiunga na klabu ndogo ya Antalyaspor iliyopanda kucheza Ligi Kuu ya Uturuki msimu huu. Makao makuu ya klabu hiyo ni mji wa Antalya ambao Yanga iliwahi kuweka kambi miaka miwili iliyopita. Kabla ya kutua hapo, Eto’o amewahi kuichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania, kabla ya Inter Milan ya Italia, Chelsea ya England na Everton ya England....
Paraguay wameifunga Brazil usiku huu kwa Mikwaju ya Penati (3-4) kwenye Michezo ya Copa America na Sasa kukutana uso kwa Uso na Argentina Nusu Fainali.Robinho akishangilia bao lake la dakika ya 15 kipindi cha kwanza kwa kuipatia bao 1-0 dhidi ya Paraguay baada ya kupata pasi safi kama kona kutoka kwa Dani Alves.  Mpaka mapumziko Brazil ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Paraguay....
HUKU ikishuhudiwa na  wachezaji wake wa kigeni Donaldo Ngoma na Joseph Tetteh Zutah waliowasili Dar es Salaam leo, Yanga ilijukuta ikitoka sare ya bila kufungana na Sports Club Villa ya Uganda kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kwenye mechi hiyo maalumu kwa ajili ya kupinga mauji ya albino na mgeni rasmi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam...

Saturday, June 27, 2015

Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Moshi vijijini,Godlisen Maramia akipokea fomu kutoka kwa Deogratius Mushi ya kuwania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi vijijini wakati liporudisha katika ofisi za chama hicho zilizopo Majengo. Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Moshi vijijini ,Godlisen Maramia akimpongeza mtia nia Deuogratius Mushi kwa uamuzi wa kuingia katika kinya'ng'anyiri...
Mashindano ya Kombe la Meya Shinyanga 2015 (Pepsi Meya Cup 2015) yamezinduliwa rasmi leo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga. Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam na kudhaminiwa na kampuni ya Vinywaji baridi ya  Pepsi (SBC Tanzania Ltd) yanashirikisha...

waliotembelea blog