Kwenye mechi hiyo maalumu kwa ajili ya kupinga mauji ya albino na mgeni rasmi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Mecky Sadiki, Yanga ilipoteza nafasi nyingi za kufunga kwenye mchezo huo.
Washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Amisi Tambwe na Simon Msuva walishindwa kufurukuta mbele ya ukuta thabiti wa Sports Club Villa ambao ni mabingwa wa Uganda.
Malimi Busungu alikosa bao la wazi kwenye dakika ya 31 baada ya kupokea pasi nzuri ya winga Goefrey Mwashuiya, lakini mpira aliopiga ulitoka pembeni kidogo ya Yanga la Sports Club Villa na dakika ya 39 Amis Tambwe alikosa bao la wazi akiwa ambeki peke yake na kipa wa Villa Sebweto Nicholaus.
Huku Villa ikiwatoa Kasule Abdulkarim na kumuingiza Dua Abeid na kisha kumtoa Kazibente James na kumuingiza Kamazi Dennis.
Hata hivyo Yanga walipata penalti kwenye dakika ya 79 baada ya Deus Kaseke kuangushwa kwenye eneo la hatari lakini Simon Msuva alipaisha penalti hiyo na kuinyima Yanga ushindi kwenye mechi hiyo ya kujipima nguvu kujiandaa na mashindano ya kombe la Kagame.
Yanga mpaka sasa imecheza michezo miwili ya kujipima nguvu ambapo wiki hii iliifunga klabu ya daraja la kwanza ya Friends Rangers kwa mabao 3-2 kwenye mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
0 maoni:
Post a Comment