FIFA
imesema Uchaguzi wa Rais wa Shirikisho hilo utaendelea Ijumaa licha ya
Maafisa wao 7 kukamatwa na Polisi kwa tuhuma za kupokea rushwa ya zaidi
ya Dola 150 Milioni. Ijumaa Kongresi ya FIFA inapiga Kura za Uchaguzi wa Rais ambapo Rais wa sasa, Sepp Blatter, anawania kiti hicho kwa mara ya 5 huku akikabiliwa na Mpinzani mmoja, Mwana wa Mfalme Ali bin al-Hussein kutoka Jordan.
Maafisa waliobambwa Leo kwa tuhuma za rushwa ni pamoja na Makamu wa Rais wa FIFA, Jeffrey Webb, na Eduardo Li, Julio Rocha, Costas Takkas, Eugenio Figueredo, Rafael Esquivel na Jose Maria Marin.

Hata hivyo, Rais wa FIFA, Sepp Blatter, hajahusishwa na Mashitaka hayo.
RSS Feed
Twitter
2:15 AM
Unknown
0 maoni:
Post a Comment