Tukio hilo la kusikitisha limetokea katika kata ya Mwakata iliyoko katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali na kuathiri watu 3,500.
Katika kata Mwakata iliyoathiriwa
zaidi, kaya 350 zimeathiriwa katika kijiji cha Makata wakati katika
kijiji cha Nhumbi, kaya 100 zimeathirika. Katika kijiji cha Magung'hwa,
kaya 50 zimeathiriwa.
Rais Kikwete amesema msiba huo siyo wa wana-Shinyanga pekee bali ni wa taifa zima ambalo limepoteza nguvu kazi muhimu kwa maendeleo yake na ustawi wa jamii ya watanzania kwa ujumla.
Rais Kikwete amewaomba wafiwa wote wawe na moyo wa uvumilivu, utulivu na subira wakati huu wa majonzi makubwa kwao wanapoomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao.

Aidha amewahakikishia wafiwa wote kuwa
binafsi yuko pamoja nao katika kipindi chote cha kuomboleza msiba huu
mkubwa kwao na kwa taifa.
0 maoni:
Post a Comment