Azam inacheza Ligi ya Mabingwa, CAF CHAMPIONS LIGI, na itaanzia Nyumbani Februari 15 kwa kuikaribisha El Merreikh ya Sudan kwenye Uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es Salaam wakati Yanga itacheza michuano ya CAF ya Kombe la Shirikisho na imepangiwa kucheza mechi ya kwanza Nyumbani dhidi ya BDF IX ya Botswana na Mechi hiyo itafanyika Februari 14 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga itarejea kwenye VPL hapo Februari 21 kwa kucheza huko Sokoine, Mbeya dhidi ya Mbeya City na Azam FC watacheza kwao Azam Complex Jijini Dar es Salaam Jumatano hii na Mtibwa Sugar na kisha kutocheza hadi Februari 22 dhidi ya Tanzania Prison pia hapo hapo Azam Complex.
Wikiendi hii ya Februari 14 na 15 zipo Mechi 5 za VPL.
Baada ya Mechi 13, Yanga ndio wanaongoza Ligi wakiwa na Pointi 25 wakifuatiwa na Azam FC wenye Pointi 22 kwa Mechi 12.
LIGI KUU VODACOM
RATIBA:
Jumatano Februari 11
Azam FC vs Mtibwa Sugar
Jumamosi Februari 14
Ndanda FC vs Mtibwa Sugar
Coastal Union vs Mbeya City
Stand United vs Mgambo JKT
Jumapili Februari 15
Polisi Morogoro vs Simba
Kagera Sugar vs JKT Ruvu
0 maoni:
Post a Comment