
Mkuu
wa wilaya ya mtwara Mh, Wilman Kapenjama akimpongeza mzee Sefu
Namtapika (60) baada ya kumkabidhi gari yake aina ya Toyota IST mpya
aliyojishindia kupitia promosheni ya Airtel Yatosha zaidi na kukabidhiwa
katika viwanja vya Mashujaa mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki hii.

Mkuu
wa wilaya ya Mtwara Mh, Wilman Kapenjama akikabidi funguo ya gari kwa
Mshindi wa Promosheni Airtel yatosha Zaidi mkoani Mtwara bw, Sefu
Namtapika (60) ambae ni mwalimu mstaafu aliyeibuka na ushindi wa Toyota
IST kupitia droo ya kwanza ya promosheni Yatosha zaidi inayoendesha na
Airtel. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni toka kushoto nyuma ni Meneja
mauzo wa Airtel mkoa wa Mtwara Bw, Batlomeo Masatu, Afisa Masoko wa
Airtel Bi Aminata Keita, na Meneja Biashara wa kanda ya Pwani Bw Albert
Majuva.

Meneja
Biashara wa kanda ya Pwani Bw Albert Majuva (wakwanza kulia)
akimpongeza Mshindi wa Promosheni ya Airtel yatosha Zaidi mkoani Mtwara
bw, Sefu Namtapika ambae ni mwalimu mstaafu aliyeibuka na ushindi wa
Toyota IST kupitia droo ya kwanza ya promosheni Yatosha zaidi
inayoendesha na Airtel. Anaefuata ni Afisa Masoko wa Airtel Bi Aminata
Keita na Meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Mtwara Bw, Batlomeo Masatu
wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika mkoani humo kwenye
viwanja vya mashujaa mwishoni mwa wiki.

Meneja
uhusiano wa Airtel bw, Jackson Mmbando akiongoza umati wa wakazi wa
mkoani mtwara waliojitokeza katika viwanja vya Mashujaa kushudia hafla
ya makabidhiano ya gari Toyota IST kwa mshindi wa droo ya kwanza ya
promosheni ya Airtel yatosha Mzee Sefu Namtapika mwishoni mwa wiki hii.

Mshindi
wa gari aina ya Toyota IST mzee Sefu Namtapika akipongezwa na mke wake
Bi… mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya gari alilojishindia kupitia
promosheni ya Airtel Yatosha zaidi. Hafla ya makabidhiano ilifanyika
katika viwanja vya mashujaa mkoani mtwara mwishoni na wiki na
kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Mtwara mjini mh, Wilman Kapenjama.
Kampuni
ya Simu za Mkononi ya Airtel imekabidhi Gari aina ya Toyota IST kwa
mshindi wa Tatu wa droo ya kwanza Promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi
inayofanyika kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo jumla ya magari 60
yatatolewa kwa wateja wanaotumia mtandao huo.
Gari hilo la tatu
limetolea kwa mshindi kutoka mkoani Mtwara ambaye ni mwalim mstaafu
Seif Namtapika Katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya mashujaa.
Namtapika amesema hakuweza kuamini mpaka hapo alipouliza katika ofisi
za Airtel za mkoani hapo.
0 maoni:
Post a Comment