Saturday, February 28, 2015
6:04 AM
Unknown
2:59 AM
Unknown
Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na mmiliki wa Blog ya The Habari.com Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi. Kutoka kushoto ni mjumbe wa TBN Mkala Fundikira, Afisa wa kampuni ya mawasiliano na matangazo ya AIMS, Shafiq Mpanja wa AIM, Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale na mjumbe wa TBN Khadija Kalili.
Katika mkutano huo TBN imesema kesho Jumamosi jioni Bloggers takriban 100 kutoka sehemu mbalimbali Nchini watakutanika katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es salam kwa ajili ya hafla ya mwaka mpya itayohudhuriwa pia na wadhamini na marafiki wa Bloggers.
Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano.
Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano.
Father Kidevu (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano.
2:48 AM
Unknown
Meneja Louis van Gaal amezungumza ila hakuweka wazi juu Robin van Persie atakaa nje muda gani ila amesema ni wiki kadhaa
Van Gaal

Robin van Persie aliumia wiki iliyopita wakati wa Mchezo wao na Swansea City huko kwenye Uwanja wa Liberty, Aliumia Enka.
Michezo mitano ijayo ya MANCHESTER UNITED
February 28: Sunderland (nyumbani)
March 4: Newcastle (Ugenini)
March 9: Arsenal (Nyumbani)
March 15: Tottenham (Nyumbani)
March 22: Liverpool (Ugenini)
Van Gaal akiteta kwenye Vyombo vya Habari juu ya mchozo wao na Sunderland kesho jumamosi 28
Makipa: David de Gea na Victor Valdeswakiteta jambo hii leo wakati wa mazoezi
Luke Shaw na Juan Mata wote wanategemewa kucheza mchezo wao wa kesho Old Trafford dhidi ya Sunderland
Van Pesrsie aliumia wakati wa Mchezo na Swansea City walipopewa kichapo cha bao 2-1
Friday, February 27, 2015
Thursday, February 26, 2015
6:38 AM
Unknown
Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya Forward Formidable Enterprises (FFE) inayoandaa
tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” Johnson Lujwangana
akifafanua jambo kuhusiana na tamthilia hiyo itakayoanza kurushwa kwenye
vituo vya televisheni kuanzia mwezi septemba. Wengine katika picha
kutoka kulia ni Jesca haule na Aisha bakari.
Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya Forward Formidable Enterprises (FFE) inayoandaa
tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” Johnson Lujwangana katikati
akifafanua jambo kuhusiana na tamthilia hiyo itakayoanza kurushwa kwenye vituo
vya televisheni kuanzia mwezi septemba. Wengine katika picha kutoka kushoto ni
Brian daniel, Neema Mung'anya, Samuel katabazi, Jesca haule, Aisha bakari na
Victor Casmir.
Waigizaji wa tamthilia ya “A boys mission” inayoandaliwa na kampuni ya Forward Formidable Enterprises katika picha ya pamoja.
Kampuni
mpya katika utengenezaji wa filamu nchini, Forward Formidable Enterprises (FFE)
inayoandaa tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” inahitaji kiasi cha
Sh milioni 800 ili ikamilike.
Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya FFE, Johnson Lujwangana alisema kuwa kwa sasa wameweza
kutengeneza toleo la utangulizi "pilot episode' kwa ajili ya kuonyesha
nini wanakifanya huku kila kitu kikiwa tayari kwa ajili ya kurekodiwa. Johnson
alisema kuwa tamthilia yao inazungumzia changamoto na suluhisho mbalimbali kwa
maisha ya vijana nchini na fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kughalimia
gharama mbalimbali za kuzalisha rasmi tamthilia hiyo.
Baadhi
ya gharama hizo kwa mujibu wa Johnson ni kulipa mtayarishaji bora, kuwalipa
wasanii fedha kutokana na ubora wa kazi zao, kulipia vifaa vya kisasa, kulipa
sehemu bora ya kurekodi tamthilia, usafiri, chakula na gharama nyinginezo.
“Kama
msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond anatengeneza video ya dakika tatu kwa
Sh Milioni 60, kwa nini tamthilia ambayo kila sehemu (episode) inatumia si
chini ya dakika 45 hisifikia kiwango hicho cha fedha? Alihoji Johnson. Alisema
kuwa wao wanataka kuwafaidisha wasanii wao kwa kuwalipa vizuri na kuendelea
kudumu katika fani na kuwataka wadhamini kujitokeza kwa wingi kusaidia mradi
huo.
“Hakuna
hata msanii mmoja maarufu katika tamthilia hii, lengo si kama kuwatupa wasanii
hao, bali ni kupanua wigo na kuwapa nafasi wasanii wengine, nataka kizazi kipya
zaidi katika tasnia ili kuendeleza kuzalisha mastaa,” alisema. Alisema
kuwa katika tamthilia imeonyesha na kutoa majibu ya nini vijana wanatakiwa
kufanya hapa nchini na kuachana na fikra za kukimbilia nje ya nchi kwa kudhani kuwa ndiko kutakuwa suluhisho la
matatizo yao.
Alifafanua
kuwa mara baada ya kufika huko, hali inakuwa tofauti na kukutana na changamoto
nyingi zaidi za maisha na kuwaza kurejea nchini. “Tamthilia
ni ya kisasa zaidi kwani lengo letu pia ni kuonyeshwa nje ya nchi na kuonyesha
madhari ya kuvutia ya jiji letu la Dar es Salaam na kupromoti mji wetu tofauti
na hali iliyozoeleka kwani tamthilia nyingi uonyesha maisha ya vijijini,”
alisema Johnson.
Alifafanua
kuwa kwa kuonyesha usafi wa mji, maeneo mbalimbali ya starehe ya hapa nchini,
kutawavutia hata wasanii watayarishaji wa tamthilia nje ya nchi kuja
kutayarishia kazi zao hapa nchini. Alisema
kuwa tamthilia hiyo ina jumla ya sehemu 12 ambapo katika kila sehemu, muigizaji
mkuu ma maudhui ya tamthilia pia yanabadilika.
6:33 AM
Unknown
Miss Universe Tanzania 2014-2015 Nale Boniface akikata keki na wanafunzi wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) wakati alipotembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Salvatrion Arm jijini Dar es Salaam ikiwa ni madhimisho ya siku yake ya kuzaliwa ambapo aliamua kuwapelekea zawadi watoto hao.
Miss Universe Tanzania 2014-2015 Nale Boniface akiwalisha Keki na wanafunzi wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) wakati alipotembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Salvatrion Arm jijini Dar es Salaam ikiwa ni madhimisho ya siku yake ya kuzaliwa ambapo aliamua kuwapelekea zawadi watoto hao.
Miss Universe Tanzania 2014-2015 Nale Boniface akigawa madaftari kwa wanafunzi wenye mahitaji wakati alipotembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Salvatrion Arm
jijini Dar es Salaam ikiwa ni madhimisho ya siku yake ya kuzaliwa ambapo aliamua kuwapelekea zawadi watoto hao.
jijini Dar es Salaam ikiwa ni madhimisho ya siku yake ya kuzaliwa ambapo aliamua kuwapelekea zawadi watoto hao.
Zawadi
Picha ya pamoja
Wednesday, February 25, 2015
9:42 PM
Unknown
Kipindi cha pili dakika ya 53 Dimitar Berbatov aliwachoma bao la pili Arsenal na kufanya 2-0 dhidi ya Arsenal. Dakika ya 90 kwenye dakika za najeruhi Alex Oxlade-Chamberlainaliwapachikia bao lao la pekee lakini Yannick Ferreira Carrasco aliyeingia kipindi cha pili alimaliza mchezo kwa kufunga bao la tatu na kufanya 3-1 na mtanange kumalizika.
Prince Albert nae alikuwemo kipenzi cha Monaco..kwenye uwanja wa Emirates usiku huu!
Mashabiki walisafiri kuja kuipa kampani ya Nguvu timu yao As Monaco kwenye Uwanja wa Emirates!!
VIKOSI:
Arsenal: Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Coquelin, Cazorla, Sanchez, Ozil, Welbeck, Giroud.
Akiba: Szczesny, Gabriel, Rosicky, Walcott, Oxlade-Chamberlain, Monreal, Chambers.
Monaco: Subasic, Toure, Wallace Santos, Abdennour, Echiejile, Dirar, Kondogbia, Fabinho, Joao Moutinho, Martial, Berbatov.
Akiba: Stekelenburg, Kurzawa, Matheus Carvalho, Bernardo Silva, Carrasco, Alain Traore, Diallo.
Refa: Deniz Aytekin (Germany)
Subscribe to:
Comments (Atom)
RSS Feed
Twitter

