Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya Forward Formidable Enterprises (FFE) inayoandaa
tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” Johnson Lujwangana
akifafanua jambo kuhusiana na tamthilia hiyo itakayoanza kurushwa kwenye
vituo vya televisheni kuanzia mwezi septemba. Wengine katika picha
kutoka kulia ni Jesca haule na Aisha bakari.
Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya Forward Formidable Enterprises (FFE) inayoandaa
tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” Johnson Lujwangana katikati
akifafanua jambo kuhusiana na tamthilia hiyo itakayoanza kurushwa kwenye vituo
vya televisheni kuanzia mwezi septemba. Wengine katika picha kutoka kushoto ni
Brian daniel, Neema Mung'anya, Samuel katabazi, Jesca haule, Aisha bakari na
Victor Casmir.
Waigizaji wa tamthilia ya “A boys mission” inayoandaliwa na kampuni ya Forward Formidable Enterprises katika picha ya pamoja.
Kampuni
mpya katika utengenezaji wa filamu nchini, Forward Formidable Enterprises (FFE)
inayoandaa tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” inahitaji kiasi cha
Sh milioni 800 ili ikamilike.
Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya FFE, Johnson Lujwangana alisema kuwa kwa sasa wameweza
kutengeneza toleo la utangulizi "pilot episode' kwa ajili ya kuonyesha
nini wanakifanya huku kila kitu kikiwa tayari kwa ajili ya kurekodiwa. Johnson
alisema kuwa tamthilia yao inazungumzia changamoto na suluhisho mbalimbali kwa
maisha ya vijana nchini na fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kughalimia
gharama mbalimbali za kuzalisha rasmi tamthilia hiyo.
Baadhi
ya gharama hizo kwa mujibu wa Johnson ni kulipa mtayarishaji bora, kuwalipa
wasanii fedha kutokana na ubora wa kazi zao, kulipia vifaa vya kisasa, kulipa
sehemu bora ya kurekodi tamthilia, usafiri, chakula na gharama nyinginezo.
“Kama
msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond anatengeneza video ya dakika tatu kwa
Sh Milioni 60, kwa nini tamthilia ambayo kila sehemu (episode) inatumia si
chini ya dakika 45 hisifikia kiwango hicho cha fedha? Alihoji Johnson. Alisema
kuwa wao wanataka kuwafaidisha wasanii wao kwa kuwalipa vizuri na kuendelea
kudumu katika fani na kuwataka wadhamini kujitokeza kwa wingi kusaidia mradi
huo.
“Hakuna
hata msanii mmoja maarufu katika tamthilia hii, lengo si kama kuwatupa wasanii
hao, bali ni kupanua wigo na kuwapa nafasi wasanii wengine, nataka kizazi kipya
zaidi katika tasnia ili kuendeleza kuzalisha mastaa,” alisema. Alisema
kuwa katika tamthilia imeonyesha na kutoa majibu ya nini vijana wanatakiwa
kufanya hapa nchini na kuachana na fikra za kukimbilia nje ya nchi kwa kudhani kuwa ndiko kutakuwa suluhisho la
matatizo yao.
Alifafanua
kuwa mara baada ya kufika huko, hali inakuwa tofauti na kukutana na changamoto
nyingi zaidi za maisha na kuwaza kurejea nchini. “Tamthilia
ni ya kisasa zaidi kwani lengo letu pia ni kuonyeshwa nje ya nchi na kuonyesha
madhari ya kuvutia ya jiji letu la Dar es Salaam na kupromoti mji wetu tofauti
na hali iliyozoeleka kwani tamthilia nyingi uonyesha maisha ya vijijini,”
alisema Johnson.
Alifafanua
kuwa kwa kuonyesha usafi wa mji, maeneo mbalimbali ya starehe ya hapa nchini,
kutawavutia hata wasanii watayarishaji wa tamthilia nje ya nchi kuja
kutayarishia kazi zao hapa nchini. Alisema
kuwa tamthilia hiyo ina jumla ya sehemu 12 ambapo katika kila sehemu, muigizaji
mkuu ma maudhui ya tamthilia pia yanabadilika.
0 maoni:
Post a Comment