
4:18 AM

Unknown
KIUNGO
wa zamani wa Arsenal Ray Parlour amesema Msimu huu Klabu yake hiyo ya
zamani isiwe na matumaini yeyote zaidi ya kumaliza Nafasi ya 3 au ya 4
kwenye Ligi Kuu England. Matokeo hayo yamewaacha Arsenal wakiwa Nafasi
ya 6 wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara Chelsea na Pointi 6 nyuma ya Timu
ya Pili, Manchester City, ambao ni Mabingwa Watetezi.
Hivi
sasa huko England ipo dhana kubwa kuwa mbio za Ubingwa kwa Msimu huu ni
kati ya Timu mbili tu, Chelsea na Man City, huku Arsenal, Man United,
Liverpool na Tottenham zikitajwa kuwa ndizo zitakazogombea Nafasi za 3
na 4.
Ray
Parlour, akiongea kwenye Kipindi cha Weekend Sports Breakfast cha
talkSPORT, amesema: “Nadhani Arsenal wanapigania Nafasi ya 3 au ya 4.
Ukiwatazama Chelsea na City wapo Ligi tofauti na Arsenal. Wako juu ya
Timu zote Arsenal, Man United, Liverpool na Tottenham. Hizi ndio
zinapigania Nafasi mbili, wanapigania Nafasi za 3 na 4!”
0 maoni:
Post a Comment