ALIEKUWA Meneja wa Southampton Mauricio Pochettino ameteuliwa kuwa Meneja mpya wa Tottenham Hotspur kwa Mkataba wa Miaka Mitano. Pochettino,
mwenye Miaka 42, aliteuliwa kuwa Meneja wa Southampton hapo Januari
2013 alipombadili Nigel Adkins na Msimu huu amewafikisha Nafasi ya 8
kwenye Ligi Kuu England iliyomalizika Mei 11, na kabla uteuzi huu wa Leo
wa kwenda Tottenham, alijiuzulu...
Wednesday, May 28, 2014


UEFA imewafungulia Mashitaka Kocha wa
Atletico Madrid Diego Simeone na Kiungo wa Real Madrid Xabi Alonso kwa
kuwatuhumu kufanya Utovu wa Nidhamu kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONS
LIGI iliyochezwa Jumamosi iliyopita huko Lisbon, Ureno na Real Madrid
kuichapa Atletico Madrid Bao 4-1. Wote hao wawili wameshitakiwa kwa makosa ya kuvamia Uwanja. Mara
mbili Diego Simeone aliingia Uwanjani...


Cardiff City imemsaini Straika wa Manchester United Federico Macheda kwa Mkataba wa Miaka Mitatu. Macheda,
mwenye Miaka 22, anakuwa Mchezaji wa 3 kusainiwa na Cardiff kwa ajili
ya Msimu ujao na atahamia bila malipo kuanzia Julai 1 wakati Mkataba
wake na Man United utakapoisha. Macheda aliwahi kufanya kazi huko Man United chini ya Bosi wa Cardiff, Ole Gunnar Solskjaer, alipokuwa Kocha...
Tuesday, May 27, 2014


Mbeya
City Usiku huu imefungwa Bao 2-1 na AFC Leopards ya Kenya katika Mechi
yao ya Pili ya KUNDI B la Mashindano ya CECAFA NILE BASIN CUP
iliyochezwa huko Khartoum, Sudan. Hadi Mapumziko, Mbeya City walikuwa nyuma kwa Bao 2-0 zilizofungwa na Mudde Musa katika Dakika ya 30 na Were Paul, Dakika ya 35.Bao la Mbeya City lilifungwa na Deus Kaseke katika Dakika za Majeruhi. Kwenye
Mechi ya...


Mratibu
Mtendaji wa tamasha hilo la ‘Love Concert –Kumbukumbu ya Mangwea’,
Kareeem Omary ‘KO’ (kushoto) akiwa na familia ya marehemu Albert
Mangwea ‘Ngwair’ Mama mzazi wa Mangwea (Katikati) na kaka wa Mangwea,
Keneth Mangwea (kulia).
Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo la ‘Love Concert –Kumbukumbu ya Mangwea’, Kareeem Omary ‘KO’ .
Bana...


Fungua sana domo kaka: David Luiz akipimwa afya katika uwanja wa mazoezi wa Granja Comary.
Imechapishwa Mei 27, 2014, saa 9:14 asubuhi.
WAKATI homa ya fainali za kombe la dunia
ikizidi kupanda kwa mataifa shiriki, timu mwenyeji, Brazil, inaendelea
kujiwinda vikali mno ili kubeba ndoo ndani ya ardhi yake ya nyumbani.
Wachezaji wa Brazil wanaonekana...


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TIMU ya Taifa ya Tanzania chini
ya kocha mkuu, Mholanzi, Mart Nooij inatarajia kujipima ubavu katika
mechi ya kimataifa ya kirafiki jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi (The Flames)
kuanzia majira ya saa 11:00 jioni.
Taifa Stars iliyopiga kambi yake
mjini Tukuyu jijini Mbeya inatarajia kuwasili asuhubi...
Sunday, May 25, 2014



Mkutano kuonyeshwa moja kwa moja na Star TV
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikagua jukwaa la wageni waalikwa kwenye uwanja wa People's Singida.
Katibu wa NEC
itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikagua jukwaa la kuhutubia ,wengine
pichani ni Maafisa wa Chama Makao Makuu Nyakia Ally (kushoto) na
Octavian Kimario(kulia)
Magari ya kurushia matangazo yakiwa...
Wednesday, May 21, 2014



Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein
akizungumza na Balozi mteule wa Tanzania nchini Sweden Mhe,Dora Msechu ,
aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo,[
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein
akifuatana na Balozi mteule wa Tanzania nchini Sweden Mhe,Dora Msechu ,
aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo,baada...


Shirika
la kutetea haki za binadamu Human rights watch limeishutumu serikali ya
Somalia kwa kuwanyima wafungwa haki za uakilishi wa wakili na
kuwashitaki raia wa kawaida chini ya mahakama za kijeshi.
Shirika
hilo limesema kuwa mamia ya raia wanahukumiwa kwa sheria kali
wasizoelewa. Human rights watch pia imesema kuwa raia wengi wamejikuta...


Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
akizungumza na ujembe wa watu kutoka Congo hawapo pichani waliomtembelea
ofisini kwake kuwaalika wasanii kutoka Tanzania kushiriki katika
sherehe za fiesta nchini Congo kwa lengo la kudumisha amani na
mshikamano katika nchi za maziwa makuu. Kulia ni Mwenyekiti wa sherehe
za fiesta kutoka Congo Bi. Anne...



Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu Kiongozi wa Japan, Yoshihiro
Suga, wakati alipofika ofisini kwake Jijini Tokyo Japan leo Mei 21,
2014, akiwa katika ziara ya kikazi. Picha na OMR
Serikali
ya Japan imeelezea nia yake ya kuendelea kuchangia bajeti ya Tanzania
na kufafanua kuwa, inafanya...



Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2014/2015) unaanza Juni 15 hadi
Agosti 3 mwaka huu wakati kipindi cha kutangaza wachezaji walioachwa au kusitishiwa
mikataba ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu.
Kipindi cha kwanza cha uhamisho wa wachezaji ni kuanzia Juni 15 mwaka huu hadi Julai
30 mwaka huu. Kupitia majina na kutangaza pingamizi ni kati ya Agosti 4 na 11 mwaka
huu. Kuthibitisha...



Kikosi cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20
(Ngorongoro Heroes) chenye watu 25 kinaondoka kesho alfajiri kwenda
Nigeria kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Nigeria (Flying
Eagles).
Mechi hiyo itachezwa Jumamosi (Mei 24 mwaka huu) katika Jiji la Kaduna
kwenye Jimbo la Kaduna ambalo lipo katikati ya Nigeria. Msafara wa timu
hiyo unaoongozwa na Mjumbe wa Kamati...


Mechi
ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini
Morocco kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe iliyochezwa Jumapili
katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 63,345,000.
Mapato
hayo katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Taifa Stars kuibuka na ushindi
wa bao 1-0 yametokana na washabiki 11,079 waliokata tiketi kushuhudia...
Subscribe to:
Posts (Atom)