Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 19
kesho (Februari 22 mwaka huu) kwa mechi tano zitakazochezwa katika miji ya Dar
es Salaam, Bukoba, Morogoro, Tanga na Arusha.
Yanga
itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting ya mkoani Pwani katika mechi itakayofanyika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Nayo Kagera Sugar inaikaribisha Rhino Rangers
ya Tabora katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Uwanja
wa Manungu uliopo Turiani mkoani Morogoro ndiyo utakaotumika kwa mechi kati ya
Mtibwa Sugar na Ashanti United, wakati Coastal Union itaumana na Mbeya City
katika mechi itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kutoka Uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga.
Maafande
wa Oljoro JKT watakuwa nyumbani kupambana na Mgambo Shooting katika mchezo
utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini
Arusha.
Jumapili
(Februari 23 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa ni Simba dhidi ya JKT Ruvu,
mechi ambayo pia itaoneshwa moja kwa moja na Azam Tv. Mechi kati ya Azam na
Tanzania Prisons iliyokuwa ichezwe kesho (Februari 22 mwaka huu) Uwanja wa
Chamazi sasa itachezwa Jumapili (Februari 23 mwaka huu) ambapo na itakuwa ‘live’.
Ligi
hiyo itaendelea Jumatano (Februari 26 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Ashanti
United na Azam itakayochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex (Chamazi).
0 maoni:
Post a Comment