David
Moyes alimsaini Juan Mata kutoka akiwa na matumaini na mategemeo
makubwa. Juan Mata alionekana kama mtu atakayekuja kuleta mageuzi ya
kuisadia timu hiyo kuingia hata kwenye Top 4. Hata hivyo hali imekuwa
tofauti na matarajio, Manchester United ikishinda mchezo mmoja tu kati
ya minne Mata aliyocheza. Moja ya vitu vinavyoachangia matatizo haya ni
mbinu za kiufundi, hivyo je inafaa kwa Moyes kuangalia upya mbinu zake
ili kupata matokeo mazuri kutoka kwa mchezaji wake wa gharama zaidi -
Juan Mata?
Mahala aambapo amekuwa akichezeshwa Mata.
Baadhi
ya watu walihisi Moyes angebadili mfumo kwenda kutumia 4-2-3-1 ili
kuweza kupata matokeo mazuri kutoka kwa Wayne Rooney, Mata na Adnan
Januzaj nyuma ya mshambuliaji wa mbele Robin van Persie, ingawa hilo
halijawezekana mpaka sasa. Mata amekuwa akichezeshwa kama kiungo wa
kulia au kushoto. Dhidi ya Arsenal alichezeshwa kama kiungo wa kushoto,
ingawa alijaribu kuingia ndani ili kuwa karibu na washambuliaji wawili
wa mbele
Kama
mchoro wa picha unavyoonesha hapo juu, United walikuwa wanacheza na
Arsenal inayogombea ubingwa ugenini, lakini hapo juu tunaona Mata
alitumia muda mwingi katika maeneo ya ulinzi, akikaa sana nyuma katika
eneo la kulinda zaidi lango la timu yake (kutokea kushoto pia). Huu
mfumo kwa hakika huwezi kukupa matunda mazuri kutoka Mata ambaye anakuwa
bora zaidi anapokuwa na mpira miguuni mwake. Ndio maana haishangazi
kuona Mata hakuwa na mchezo mzuri siku hiyo, akitengeneza nafasi mbili
tu kwa Van Persie.
Dhidi
ya Fulham alicheza vizuri kiasi na kuwa na mpira muda mwingi, ingawa
alifanya hivi akicheza kwenye winga ya kulia katika mchezo ambao
ulitawaliwa na krosi kutoka kwa wachezaji wa kikosi cha Moyes. Man
United ilijaribu kupiga krosi 82, staili ambayo sio tu imepitwa na
wakati lakini pia ni staili ambayo ndani yake huwezi kuona ubora wa Juan
Mata, ambaye hufanya vizuri kazi yake anapocheza katikati ya mistari ya
safu ya ulinzi na kiungo, na sio pembeni.
Mahala kwa kubadilisha
Mata
hakufanya vibaya dhidi ya Fulham, alitengeneza nafasi tano za kufunga
kwa wachezaji wenzie na katika mechi nne alizocheza ametengeneza jumla
ya nafasi 13 (namba ya nafasi alizotengeneza Ashley Young msimu mzima).
Lakini angeweza kufanya vizuri zaidi. Dhidi ya Fulham alikuwa na mpira
kwa muda mwingi na alikamilisha 96% ya pasi zake zote.
Lakini
tatizo pekee la hizo pasi zilikuwa katika maeneo ya pembeni, hasa
upande wa kulia. Haya sio maeneo ya kupata ubora wa Mata. Mata anahitaji
kuchezeshwa kati kati ya safu ya ulinzi ya wapinzania na kiungo, mahala
ambapo anaweza kutumia jicho lake la pasi nzuri kwenda kwa
washambuliaji. Kama tunavyoona kwenye picha hapo juu, hakuwa na mamalka
ya mchezo kwenye eneo hilo.
Wazo
la kwanza mbadala na kumuondoa mshambuliaji mmoja na kumchezesha Mata
namba 10, jambo litakalomfanya awe na mpira muda mrefu na kuutumia
katika maeneo ambayo anataka, sio kurudi nyuma kama ambavyo alivyokuwa
akifanya dhidi ya Arsenal. Alicheza kwenye eneo hili katika mchezo pekee
wa ushindi wa United katika mechi nne zilizopita - mechi dhdi ya
Cardiff, ambapo alitengeneza nafasi nne.
Moyes
anaonekana hataki au anasita kuwatumia Januzaj, Mata na Rooney katika
kikosi kimoja na Van Persie. Hii inawezakana inatokana kwamba wachezaji
wake wote watatu wa zamani wana uwezo wa kuingia ndani nyuma ya
mshambuliaji wa kati. Njia pekee ya kufanya mfumo huu kufanya kazi ni
kuachana na mfumo wa krosi na kuachia mpira wa pasi zaidi kuelekea ndani
utumike zaidi.
Hitimisho
Hivi
sasa David Moyes hapati matunda bora ya Juan Mata. Mfumo wa kutumia
krosi ambayo Mata anatumika katika winga sio mzuri katika kutaka kupata
matunda ya Juan Mata. Mata anahitaji uhuru wa kufanya kazi yake katika
maeneo yake ya kati ya uwanja, hasa kwenye eneo la nyuma ya
mshambuliaji. Ikiwa Moyes atabadili mfumo kwenda 4-2-3-1 ambao unamfiti
Mata, Januzaj na Rooney wakicheza nyuma ya Van Persie. Jambo pekee la
kuzingatia ni kuhakikisha mabeki wa pembeni wanakuwa na uwezo wa kutoa
msaada mkubwa wakati timu inaposhambuliwa. Moyes hana cha kupoteza hivi
sasa - hasa baada ya mfumo wa sasa wa 4-4-2 kutokuwa na matunda kwa timu
na kupelekea matokeo mabaya.
0 maoni:
Post a Comment