Monday, February 24, 2014



Sherehe za kufunga rasmi michezo ya Olimpiki ya Sochi
Michezo ya ishirini na mbili ya Olimpiki ya majira ya baridi, iliyodumu kwa siku 17, imemalizika Jumapili katika mji wa kitalii wa Sochi, kwa wenyeji Urusi kuibuka wa kwanza
Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach alifunga rasmi michezo hiyo katika tafrija iliyodumu kwa dakika 130.
Urusi ilimaliza ya kwanza katika jedwali la medali, ikiwa na medali 13 za dhahabu 11 za fedha na 9 za shaba.
Norway ilimaliza ya pili na medali 11 za dhahabu 5 fedha na 10 za shaba.
Canada ilikamilisha orodha ya tatu bora na jumla ya medali 10 za dhahabu 10 za fedha na 5 za shaba.
Korea Kusini ilikabidhiwa bendera ya Olimpiki ikiwa ni ishara ya kuandaa michezo hiyo mwaka 2018, itakayofanyika katika mji wa Pyeongchang.
Mashindano ya Urusi yaligharimu dola bilioni 30, ambacho ni kitita kikubwa zaidi katika historia ya mashindano ya Olimpiki duniani IOC.
Rais wa shirikisho la Olimpiki duniani (IOC) Thomas Bach ameitaka dunia kuitizama Urusi kwa mtazamo mpya kwani wameonyesha uwezo wa hali ya juu katika kuandaa michezo hiyo na kukidhi matarajio ya washiriki wengi walioshiriki mashindano ya msimu wa baridi Sochi.
Alisema wanaondoka Sochi wakiwa marafiki bila ya kumbukumbu ya changamoto zilizokuwepo awali.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog