Tuesday, February 25, 2014


Iringa. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa amesema tatizo la umaskini linalowakabili Watanzania, linatokana na viongozi walioko madaraka kutokuwa waadilifu.
Alisema Tanzania ni nchi iliyojaaliwa rasilimali nyingi ambazo kama zikisimamiwa vyema taifa haliwezi kuwa na watu maskini kama ilivyo hivi sasa.
Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwenye mikutano ya kampeni iliyofanyika katika Vijiji vya Igula katika Kata ya Luwota na Magulilwa mkoani Iringa.
“Nchi hii siyo maskini, imejaliwa rasilimali nyingi ambazo kama zikisimamiwa ipaswavyo, taifa lisingekuwa na umaskini kama ilivyo sasa,” alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Leo hii viongozi wa CCM wamekosa uadilifu ndiyo maana magogo kutoka katika misitu yetu yanaibiwa na kupelekwa nje ya nchi.
Dk Slaa alisema hayo yanatokana taifa kuongozwa na watu wasio waadilifu, huku Amiri Jeshi Mkuu ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete akishindwa kukabiliana na hali hiyo. Katika mikutano hiyo, Dk Slaa aliwataka wakazi wa Kalenga kumchagua mbunge wao ili kuongeza idadi ya wabunge wake

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog