1. Diamond Platnumz
Hakuna
ubishi kuwa, mwaka 2013 Diamond Platnumz ndiye msanii aliyeingiza fedha
nyingi zaidi. Pesa nyingi ya Diamond imetokana na malipo ya show zake
za ndani na nje ya nchi. Kwa uhakika, mwaka huu pekee, Diamond
amefanikiwa kuingiza takriban shilingi bilioni 1.
Kwa
show za ndani peke yake, Diamond hutoza si chini ya shilingi milioni 10
ama 15 na kila wiki hufanya show zaidi ya 2. Hivyo tangu mwaka uanze,
Diamond amekuwa akiingiza shilingi milioni 40 kila wiki. Tour za nje
alizofanya mwaka huu ni pamoja na zile za Uingereza ambako alifanya show
kwenye miji mitatu, show ya Burundi na Congo, show mbili za Kenya
(Nairobi na Mombasa), show ya nchini Comoro ambako alilipwa si chini ya
dola 30,000 na show ya Malaysia wiki iliyopita.
Kwa
upande wa show za hapa nyumbani ambazo ni nyingi mno zisizo na idadi,
ukiachana na zile za kawaida, Diamond aliingiza shilingi milioni 40
kwenye show 4 za Kili Music Tour ambapo kila show alilipwa shilingi
milioni 10. Ndiye msanii aliyelipwa fedha nyingi zaidi kwenye ziara
hiyo.
Pia
amefanya show kadhaa za Fiesta 2013, show za promotion za Tigo na
makampuni mengine, Tamasha la Matumaini, show ya Tulizana Tuko Wangapi
ya Leaders Club, show yake na Nay wa Mitego (Dar Live na Maisha Club).
Mwezi February 16 mwaka huu, Diamond alifanya show jijini Arusha ambayo
kiingilio chake kilikuwa ni shilingi 150,000 ndani ya Club Safari na
ukumbi kufurika.
Miezi
kadhaa iliyopita pia hitmaker huyo wa ‘Number 1’ ameshaalikiwa kwenye
show corporate kuburudisha wafanyakazi wa benki na taasisi zingine
pamoja na watu binafsi na zote hizo zimemuingizia fedha nyingi. Pamoja
na show, Diamond amekuwa akiingiza fedha nyingi zaidi kwenye malipo ya
ringtones ambapo kila baada ya miezi mitatu amekuwa akiingiza si chini
ya shilingi milioni 20. Kwa mujibu wa Push Mobile, akaunti ya Diamond
kwenye kampuni hiyo ndio inayoingiza fedha nyingi kuliko msanii mwingine
yeyote wa Bongo Flava.
Mkataba
exclusive alioingia na kampuni ya simu ya Vodacom kuuza wimbo wake mpya
My Number One kama muito wa simu, umezidi kumpandisha juu na ikidaiwa
kuwa mkataba huo ni wa mamilioni ya shilingi.
Ikumbukwe
pia, Diamond ni balozi wa Cocacola. Mkataba huo ambao haijajulikana
umemuingizia shilingi ngapi, lakini ni fedha inayoweza kuwa si chini ya
shilingi milioni 100.
Diamond ni miongoni mwa wasanii wengine 23 wa Afrika akiwemo Lady Jaydee kwenye mradi mkubwa wa Cocacola wa Coke Studio Africa.
2. Lady Jaydee
Huwezi
amini, vuguvugu la Anaconda limemsaidia Jaydee si tu kukusanya
mashabiki wengi zaidi, bali pia limempa fedha nyingi mno. Zaidi ya
tiketi 3,500 zilinunuliwa kwenye show yake ya mwezi June ya Miaka 13 ya
Muziki na kuingiza takribani shilingi milioni 100. Haikuishia hapo,
albam yake Nothing But The Truth ilinunuliwa kwa kiasi kikubwa na
kumfanya kuwa msanii pekee wa Bongo Flava anayeendelea kufurahia mauzo
ya albam zake.
Hits
zake mbili, Joto Hasira na Yahaya kutoka kwenye albam yake hiyo,
zimebadilisha maisha yake na kumfanya kuwa mwanamuziki mwenye show
nyingi zaidi pia. Lady Jaydee ametumbuiza kwenye karibu show zote za
Kili Music Tour ambako ameingiza shilingi milioni 25.
Mwaka
huu pia Lady Jaydee amefanya show nyingi kubwa ikiwemo ile ya uzinduzi
wa filamu ya Lulu, Foolish Age, show yake kwenye Miss Tanzania 2013,
Family Day Show ya Arusha iliyofanyika Eid Pili, Anaconda Show
iliyofanyika Triple A na nyingine iliyofanyika Snow View Hotel. Akiwa
Arusha pia, Lady Jaydee aliuza kopi za albam yake kama njugu pamoja na
tiketi za Anaconda zilizouzwa kwa shilingi 15,000 kila moja.
June
mwaka huu pia, Lady Jaydee alitumbuiza kwenye semina ya kuwezesha
wanawake kuondokana na njaa na umaskini, iliyofanyika chini ya mfuko wa
fursa sawa kwa wote chini ya mama Anna Mkapa. Biashara yake ya Nyumbani
Lounge, imeendelea kufanya vizuri pia kwa kupata wateja wengi wanaoenda
kupata chakula, vinywaji na burudani kutoka kwa bendi yake ya Machozi.
Bado
anaingiza fedha kupitia udhamini wa Airtel kwenye show yake ya TV ya
Diary of Lady Jaydee. Msanii huyo ambaye jina lake ni Judith Wambura pia
miongoni mwa wasanii 24 wa bara la Afrika waliochukuliwa kwenye mradi
wa Coke Studio Africa wa kampuni ya Cocacola unaoendelea jijini Nairobi
Kenya.
Coke Studio Africa – the new, exciting music show featuring incredible live performances by the very best in Africa
3. AY
Humsikii
sana rapper huyu kwenye show za Tanzania. Tofauti na wasanii wengine,
fedha anazoingiza AY zinatokana zaidi na endorsements na biashara zake
anazofanya. Pesa nyingi alizoingiza zimetokana na mkataba wa mwaka mmoja
na Airtel wa ubalozi uliokamilika mwezi May mwaka huu.
Katika
ubalozi huo wa Airtel Africa, AY aliungana na wasanii wengine watatu wa
Afrika ambao ni pamoja na Papa Wemba, Tuface na Daddy Owen wa Kenya.
Katika mkataba huo AY alilipwa dola za Kimarekani 80,000 ambazo ni zaidi
ya shilingi milioni 129.
Rapper
huyo wa ‘Machoni Kama Watu’ ni balozi pia wa bia ya Peroni ya Italia na
kupitia mkataba huo, AY ameingiza mkwanja mwingi. AY pia ni mwanzilishi
mwenza wa kipindi cha Mkasi kinachoendeshwa na Salama Jabir. Kipindi
hicho kina wadhamini wawili, Cocacola na Airtel na hivyo kupitia
mgawanyo wa mapato, AY amekuwa akiingiza pia fedha ya kutosha.
AY
ni CEO wa kampuni ya Unity Entertainment inayojihusisha na kuandaa
show, matangazo, kuleta wasanii wa nje na mambo mengine. Mwaka huu
pekee, ikishirikiana na kampuni ya SK Entertainment, kampuni yake
imeandaa show kibao zikiwemo zile zilizofanyika Elements Lounge ambapo
Avril, Prezzo, Huddah Monroe na J-Martins wamewahi kuhudhuria.
Maisha
ya kawaida ya rapper huyu ndio yanayowafanya watu wengi wasijue ukubwa
wa kile anachokiingiza. Macho yake ameyaelekeza zaidi kwenye uwekezaji
na anawekeza haswaa. Kuna tetesi kuwa, AY anajenga ghorofa lake maeneo
ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. Anasemekana kuwekeza pia mkoani
Mtwara alikonunua ardhi ya kutosha. Mungu ndio anajua ni wapi
alikowekeza tena.
4. Ommy Dimpoz
Ommy
Dimpoz ambaye kwa sasa yupo kwenye ziara ya muziki nchini Marekani
ameingiza fedha zake nyingi kupitia show alizofanya. Ziara zake za Ulaya
na Marekani pekee zimemuingizia dola 50,000 ambazo ni sawa shilingi
milioni 81.
Tangu
aachie wimbo wake mpya Tupogo, tayari Ommy ameshaingiza shilingi
milioni 50. Kwenye show yake ya hivi karibuni ya Tupogo Night
iliyofanyika Club Billicanas, Ommy alipeleka nyumbani shilingi milioni
10 baada ya kukata gharama zote. Watu 1,770 walihudhuria show hiyo.
Show
yake ya Burundi ya mwanzoni mwa mwezi uliopita ilimuingizia staa huyo
shilingi milioni 30. Ommy hutoza si chini ya shilingi milioni 7 kwa show
na kwa mwezi, amekuwa na uhakika wa kufanya show tatu ama nne za ndani
bila kusahau show za Kili Music Tour.
Hivi
karibuni kwenye segment ya Tell it All ya Bongo5, Ommy alifunguka kuwa
makampuni mengi yamekuwa yakimfuata kumpa endorsements lakini msimamo
wake wa kutaka kulipwa fedha ya uhakika imemfanya azikatae nyingi lakini
yupo mbioni kupata deal kubwa. Mpaka sasa Ommy anajenga nyumba mbili
kwa mpigo zenye thamani ya shilingi milioni 250 hadi zilipofikia. Tayari
ana viwanja vingine viwili anavyotaka kuangusha mijengo mingine. Hivi
karibuni pia atakuja na clothing line yake ya PKP.
5. Madee
Hii
inaweza kuwa surprise kwa wengi lakini Madee ni mfano tosha wa jinsi
single moja inavyoweza kubadilisha maisha ya msanii. Tangu atoe single
yake, Sio Mimi, Madee ameshaingiza si chini ya shilingi milioni 200.
Mwaka
huu ameshafanya show 10 za kampeni ya Tigo ambapo kila moja alilipwa
shilingi milioni 3, show 15 za Airtel kwa kiwango hicho hicho. Alifanya
show mbili za kampeni za Coca Cola, ile ya uzinduzi wa Coke Zero na
Cocacola Bonanza Mlimani City. Bado ameendelea kufanya show za Fiesta
2013. Madee pia alikuwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye show
ya Fuse ODG iliyofanyika September 7 kwenye viwanya vya ustawi wa jamii
jijini Dar es Salaam.
6. Mwana FA
Mwanzoni
mwa mwaka huu, Hamis Mwinjuma aka Mwana FA alikuwa msanii wa tatu
miongoni mwa wasanii waliongiza fedha nyingi kupitia malipo ya miito ya
simu, RBT ambapo aliingiza shilingi milioni 18. Alifanya show mbili
kwenye Kili Music Tour ambapo aliingiza si chini ya shilingi milioni 7
pamoja na show kadhaa za Fiesta 2013.
Show
yake ya The Finest ilimuingizia shilingi milioni 19. Hivi karibuni
alichukuliwa na kampuni ya Vodacom kuzunguka baadhi ya mikoa kwenye
kampeni yao na CCBRT kuhusiana na kukuza uelewa wa tatizo la Fistula na
kulipwa mkwanja kama balozi wa kampeni hiyo.
Mwaka
huu FA amefanya matangazo kadhaa ya Vodacom. Hivi karibuni pia aliingia
kile kilichoonekana mkataba kama balozi wa simu za Samsung Galaxy
Tanzania japo haijulikani kama ulikuwa mkataba wa ubalozi kama ilivyo
mingine.
Mwana
FA pia amefanya show za nje zikiwemo za Kenya na Afrika Kusini
aliyofanya siku ya Eid mwezi uliopita. Kama wasanii wengine pia, FA
ameingiza fedha nyingi kwa show za kawaida za hapa nyumbani na zile za
promotion.
Mwaka
huu Chege peke yake alifanya show sita nje ya nchi ambazo kila show
alilipwa shilingi milioni 4. Akiwa na Temba ambao kwa pamoja hutoza
shilingi milioni 6, Chege amefanya show zaidi ya 30 zikiwemo zile za
Fiesta, za promotion mbalimbali na zile za kawaida.
Pamoja na hivyo, Chege
ana biashara ya salon.
8.PROFESA J
Profesa
Jay aliingiza shilingi milioni 20 za Kili Music Tour, alifanya show
kubwa ya Jose Chameleone April mwaka huu, show kibao za promotion za
makampuni, show ya kampuni ya IPP kwaajili ya Walemavu, Diamond Jubilee
mwezi January, na show zingine za kawaida za Dar na mikoani. Pia nguli
huyo wa rap ya Tanzania ameingiza fedha nyingi kupitia show nyingi za
Lady Jaydee.
Prof
J amewekeza kwenye biashara ya salon ambayo tayari inafanya vizuri na
ameshafungua studio ya kurekodi muziki iliyopo kwenye hatua za mwisho
kuanza kazi. Jize aliingiza pia fedha kupitia kampeni ya magazeti ya
Mwananchi kwa kufanya matangazo na show za mikoani.
9. Nay wa Mitego
NAY WA MITEGO
Tangu
mwaka uanze, Nay wa Mitego ameshafanya show zaidi 20 zilizomuingizia si
chini ya shilingi milioni 60. Show hizo ni pamoja na zile za promotion
za makampuni ya simu, show mbili za Muziki Gani, show ya Kili Music
Tour, show za Fiesta na zile za kawaida. Pia ana biashara zake ambazo
kwa pamoja humuingizia si chini ya shilingi milioni 4 kwa mwezi.
10.Temba
MH TEMBA
MH TEMBA
0 maoni:
Post a Comment