Monday, November 25, 2013



Jesús Navas 1' • Sandro 34' OG • Sergio Agüero 41' • Sergio Agüero 50' Álvaro Negredo 55' Jesús Navas 90' +2' •Manchester City leo wameinyuka timu ya Tottenham Hotspurs bao 6-0 kwenye uwanja wa Etihad. City wakitandaza soka safi na wakionesha kiwango chao cha hali ya juu nyumbani kwao ndio walionza kupata bao la mapema dakika ya 1 baada ya mchezaji wao mpya Jesús Navas kufunga bao hilo. City waliongeza bidii zaidi ili wajikwamue watoke nafasi waliokuwa nayo nafasi ya tisa baada ya kufungwa na vibonde Sunderland wiki iliyopita.
Bao la pili la Manchester City limefungwa dakika ya 34 kwa mchezaji Sandro kujifunga bao hilo baada ya kucheza ndivyo sivyo, Bao la tatu likifungwa na Sergio Agüero dakika 41 na akifunga tena bao jingine la pili dakika ya 50, Álvaro Negredo akafunga bao tena kwa City katika dakika ya 55.

Jesús Navas akawafunga bao tena Spurs katika dakika za lala salama dakika ya 90' +2.
Ushindi huu unawapandisha City hadi nafasi ya NNE wakiwa na Alama 22.
Early strike: Jesus Navas put Man City ahead against Tottenham after just 14 seconds
Jesus Navas akiifungia bao  Man City dhidi ya  Tottenham katika dakika ya 1
At the double: Sandro deflects the ball into his own net following Alvaro Negredo's volley
Sandro akijifunga bao hapa baada ya Alvaro Negredo kuachia shuti
Strike: Hugo Lloris watches on as Sergio Aguero extends Man City's lead just before half-time
Kipa wa Spurs Hugo Lloris akianga Sergio Aguero akitupia ndani ya lango lake mpira muda mchache kabla ya mapumziko
Exquisite: Negredo shoots after an excellent turn to get the better of Spurs defender Michael Dawson
Negredo akituliza mpira kwa makini na kuachia shuti kali.
Team effort: Negredo celebrates with team-mates Aguero and Samir Nasri after scoring Man City's fifth goal
Negredo akipongezwa na  Aguero pamoja na  Samir Nasri baada ya kufunga bao la nne
Hit for six: Jan Vertonghan slides in as Navas slots home City's sixth goal in the last minute
Jan Vertonghan akimkaba Navas jambo ambalo halikuwezekana katika dakika za lala salama na shuti kali la Navas kuingia langoni mwao.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog