Saturday, July 18, 2015


Timu zikiingia Uwanjani asubuhi yale jumamosiKikosi kilichoanza cha Man UnitedVikosi vyote viwili kwenye Line upMtanange ukiendelea kwenye patashika lango la Club America!Mashabiki wakiishangilia Timu ya Man United
Morgan Schneiderlin Anaipachikia bao la mapema la kichwa  na kufanya 1-0 dhidi ya Club America katika dakika ya 5 baada ya kusaidiwa  na Juan Mata aliyeunganisha mpira wa kona na kumpata Morgan.  Schneiderlin anaanza vyema Man United!
Hadi Mapumziko Manchester United 1 Club America 0. Kipindi cha pili kiliendelea vyema na Kocha kabla ya Mechi hii, Meneja wa Man United Louis van Gaal alisema atachezesha Timu mbili na kweli alifanya hvyo baada ya kubadili Wachezaji 11 kwa ajili ya Kipindi cha Pili.Kwa Kipindi cha Kwanza, Man United walianza na Kipa Sam Johnstone, Mabeki Darmian, Phil Jones, Daley Blind na Luke Shaw, Viungo Michael Carrick, Schneiderlin, Juan Mata na Ashley Young huku Mastraika wakiwa Memphis Depay na Wayne Rooney.
Wachezaji 11 walioingizwa Kipindi cha Pili ni Kipa Lindegaard, McNair, Smalling, Evans, Blackett, Schweinsteiger, Herrera, Lingard, Pereira, Januzaj, Wilson.Wachezaji wa Man United wakimpongeza Morgan Schneiderlin
Schneiderlin celebrates his breakthrough goal with Phil Jones and Memphis Depay as United seized the early initiative 
Schneiderlin akipongezwa na  Phil Jones pamoja na  Memphis Depay
Wayne Rooney tries to prevent Pablo Cesar Aguilar from playing the ball down the line during the opening half
Wayne Rooney na Pablo Cesar Aguilar
Club America's Osvaldo Martinez (left) leaves United duo Memphis Depay (middle) and Juan Mata (right) in his wake
Mchezaji wa Club America Osvaldo Martinez akiwachomoka Memphis Depay na Juan Mata na kwenda mbele
Juan Mata akipanga kumchomoka mchezaji wa Club America Paolo Goltz kwenye mchezo wao wa kirafiki huko SeatlleTaswira ya Uwanja huo kwa Upande wa Screen kubwa ilipo Eeeh! Chupuchupu United wapate bao la piliJanuzaj akilindwa kwa karibu na Wachezaji wa Timu ya Club America
KIKOSI CHA MAN UNITED
Man United XI:
Johnstone, Darmian, Jones, Blind, Shaw, Carrick, Schneiderlin, Young, Mata, Memphis, Rooney

Club America: Gonzalez, Mares, Aguilar, Sambueza (c), Goltz, Arroyo, Samudio, Guemez, Quintero, Martinez, Buron
Mashabiki: 48,857


Fabian Delph akitambulishwa huko Manchester City Etihad
Kapewa Jezi No. 18Wakipata picha na ShabikiKaribu Etihad
Delph gives two thumbs up after confirming that he would be leaving Aston Villa to move to Manchester
Delph vipimo vilienda safi

Delph amejiunga na City kwa kitita cha  £8million

Delph akionesha jezi yake

Delph tayari kuiletea Makombe  City

Mike Summerbee alipokutana na  Delph na kumwivishia jezi yake

Kitu cha Delph tayari kwa kuvaliwa


Anatakiwa Old Trafford
Manchester United kwa karibu sana wanafukuzia sahihi ya Fowadi  wa  Barcelona Pedro

 Arda Turan (katikati) na Gerard Pique wakati wa mzoezi

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho nae amekuwa akimwitaji mchezaji huyo Pedro anayeuzwa dau kama la
£22m

Kocha wa Man United  Louis van Gaal bado anaendelea kuwa bize kuboresha Kikosi chake.

Mchezaji wa zamani wa Timu ya  Bayern Munich Bastian Schweinsteiger na sasa Manchester United wakiwa kwenye mazoezi ambapo Kocha huyo ameamua kabla ya Msimu ujao kuanza kuboresha kikosi chake

Friday, July 17, 2015


MABINGWA wa Italy Juventus wamesisitiza Kiungo wao Paul Pogba hauzwi licha ya Ofa kutoka Barcelona.
Joan Laporta, Rais wa zamani wa Barca ambae sasa anagombea tena nafasi hiyo, ameweka kwenye ajenda yake kuwa akichaguliwa Urais basi atamnunua Pogba.
Laporta yupo kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Urais pamoja na Rais wa sasa Josep Maria Bartomeu, August Benedito na Toni Freixa.
Pogba, Kijana wa Miaka 22 wa Kifaransa alietokea Man United kwenda Juve, pia anawindwa na Manchester City na Chelsea.
Mkurugenzi wa Juve, Giuseppe Marotta, amesema: "Yeyote anaemtaka Pogba anapaswa kuongea na sisi na si Wakala Mino Raiola. "

Aliongeza: "Tumezungumza na Barca katika Miezi ya hivi karibuni lakini hauzwi. "
Hata hivyo, hata kama Barca watamnunua Pogba ambae ana Mkataba hadi 2019, hawawezi kumtumia hadi Januari 2016 kutokana na kufungiwa na FIFA kwa kukiuka Kanuni za Usajili wa Wachezaji Chipukizi.
Licha ya Adhabu hiyo, Barca imeshasaini Wachezaji Wawili katika Kipindi hiki cha Uhamisho ambao ni Aleix Vidal kutoka Sevilla na Kiungo wa Uturuki anaetokea Klabu ya Atletico Madrid Arda Turan.



KOCHA wa timu ya APR ya Rwanda, Dusan Dule Suyagic amejigamba kuwa kikosi chake kitafanya vizuri kwenye mashindano ya Kagame inatarajiwa kuanza kutimua kesho jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya mazoezi na timu yake yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dusan alisema msimu uliopita timu yake ilishika nafasi ya pili baada ya kufungwa na El Merreikh ya Sudan hivyo msimu huu wamekuja wakijua kuna ushindani lakini nao watahakikisha wanatoa ushindani.
“Naheshimu kila timu iliyopo kwenye mashindano haya lakini naamini APR tutaonyesha ushindani kwani lengo letu ni kutwaa ubingwa wa CECAFA”, alisema Dusan.
APR itafungua dimba la mashindano ya Kagame ambayo yanashirikisha klabu toka nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa na Al Shandy ya Sudan kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa saa 8 kabla ya Yanga na Gor Mahia kuingia dimbani saa 10.00 kumaliza ubishi wa mashabiki kuwa nani mkali kati ya hizi timu kongwe Afrika Mashariki.


Mashindano ya CECAFA yanashirikisha vilabu 13 toka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambapo APR FC ipo kundi B pamoja na Al Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi na Hegaan FC ya Somalia.
Kundi A lina timu za Yanga na KMKM za Tanzania, Telecom ya Djibout, Gor-Mahia ya Kenya na Khartoum ya Sudan wakati kundi C lina timu za Azam ya Tanzania, Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda.


Arsene Wenger amesema Arsenal wanalenga kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu England Msimu huu unaoanza Agosti 8.
Msimu uliopita Arsenal walimaliza Nafasi ya 3 kwenye Ligi ambayo hawajawahi kutwaa Ubingwa tangu 2003/04 na tangu wakati huo walitoka kapa kila Msimu na kuonja Makombe Mwaka Jana kwa kutwaa FA CUP na kulitetea tena Mwaka huu.
Hadi sasa Arsenal imemsaini Mchezaji mmoja tu, Kipa Mkongwe kutoka Chelsea, Petr Cech, lakini Wenger ana imani kubwa na Kikosi chake.

Amenena: "Ubingwa ni lengo letu na tunaamini tuna nafasi ya kuleta changamoto. Hatuko mbali."
Wenger, alietua Arsenal Mwaka 1996, ameweza kuipa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 3 kwenye Misimu ya 1997/98, 2001/02 na 2003/04.
Kipa mpya wa Arsenal Petr CechArsene Wenger akiwaangalia Vijana wake kwenye mazoeziMtu kati!Cazorla wakati wa mapumziko



Kocha wa Mkuu wa Yanga, Hans Van Pluijm (kulia) akisisitiza jambo kwa kuinua kidole juu na kufanya ukumbi kuzizima kwa kicheko alipokuwa akiongea na wandishi wa habari juu ya mchezo wao dhidi ya Gor-Mahia utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katikati ni kocha mkuu wa Gor Mahia, Frank Nuttal na kushoto ni Katibu Mkuu wa Vyama vya Soka vya nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Nicholaus Musonye. (Picha na Rahel Pallangyo)

MAKOCHA wa timu za Yanga na Gor Mahia ya Kenya wametambiana kila mmoja kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa ufunguzi wa Mashindano ya kombe la Kagame utakaochezwa kesho majira ya saa 10:00 kwa saa za Afrika Mashariki kwenye Uwanja wa Taifa.
Kocha wa mkuu wa Yanga Hans Van Pluijm amesema anawaheshimu wapinzani wake timu ya Gor Mahia lakini haiogopi na ana matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
“Nimefundisha soka Afrika tangu mwaka 1996 hivyo nina uzoefu na soka la timu za hapa kwa muda mrefu, lakini pia tumefanya maandalizi ya kutosha lakini mimi sidharau mpinzani wangu kwa sababu kwenye soka lolote linaweza kutokea na hakuna mtu anayejua matokeo”, amesema Pluijm.
Kocha mkuu wa Gor Mahia, Frank Nuttal amesema hana uzoefu mkubwa kwenye soka la Afrika ukilinganisha na mpinzani wake (Van Pluijm) lakini akasisitiza kuwa vijana wake wako vizuri kuikabili Yanga.
“Yanga ni timu kubwa japo sijawahi kuiona ikicheza lakini naamini ni timu yenye ushindani na mechi ya kesho itakuwa ngumu lakini mwisho wa mchezo tutajua matokeo”, amesema Nuttal.
Mchezo huu ambao mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Ujenzi, John Magufuli ambaye pia ni mteule wa kugombea kiti cha urais kupitia chama tawala (CCM) unatarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake kutokana na timu zote kuwa na historia inayolingana kwenye mashindano haya kwani kila mmoja ametwaa kombe la Kagame mara tano.

waliotembelea blog