Sunday, May 10, 2015


Real leo hali siyo shwari!!! sare yawaangusha! Walitoka nyuma ya bao 2-0 na kusawazisha kuwa 2-2 mpaka dakika 90 zinamalizika, Ronaldo pia akikosa penati katika mtanange huo!Cristiano Ronaldo akiwa hoi baada ya kubanwa leo na Timu ya Valencia CF huku Real wakitoka Nyuma na kusawazisha bao kuwa 2-2, Sare hiyo ikiwaacha nyuma ya pointi nne dhidi ya Vinara Barcelona.

Fowadi wa Valencia CF  Paco Alcacer akishangilia bao lake la dakika ya 19

Wachezaji wa Valencia wakipongezana baada ya Javi Fuego kumfunga kipa wa Real Iker Casillas kwa mpira wa adhabu

Valencia walitangulia kipindi cha kwanza kwa kufunga bao 2-0

Ronaldo leo hoi!!  BernabeuPaco Alcacer dakika ya 19 kipindi cha kwanza anawaandikia bao la kwanza Valencia kwa kufanya 1-0 dhidi ya Real Madrid.
Pepe alianza kurudisha bao  kipindi cha pili dakika ya 56 na Isco dakika ya 84 kusawazisha bao na kufanya 2-2 na mtanange kumalizika.
Sare hii inawafanya Real kugawana pointi moja moja na Valencia huku Barcelona wakiwazidi pointi 4 Kileleni Real ambao wako nafasi ya pili. Barca wako Kileleni wakiwa na pointi zao 90 na Real wametimiza pointi 86. Nafasi ya tatu inashikiliwa na Atletico de Madrid wenye pointi 76.
Valencia CF pamoja na kuwa mbele ya bao 2-0 dhidi ya Real na kulazimishwa sare wao wapo nafasi ya 4 na pointi zao 73.


Chupchupuu!!!Marouane Fellaini aliifungia Manchester United bao la pili na kufanya 2-1 dakika ya 78 na mtanange kumalizika United wakiibuka kidedea kwenye Uwanja wa Selhurst Park, London mbele ya mashabiki 25009. Ushindi huu wa United unawapa Matumaini ya Kucheza Klabu Bingwa Ulaya msimu Ujao kwani wamefanikiwa kupata pointi 68 na wapo ndani nne bora wakiwa pia nafasi ya nne. Ashley Young akishangilia!Jason Puncheon dakika ya 57 kipindi cha pili alisawazisha bao na kufanya 1-1.Jason Puncheon akishangilia bao lake1-1Jason Puncheon baada ya kuweka sare
Juan Mata akichonga penati.Mpaka nyavuni!Mata akishangiliaPongezi kwa MataMchezo huu pia Umemalizika ukimwachia Majeraha Luke Shaw na kulazimika kuondolewa Uwanjani na huku Wayne Rooney akipumzishwa baada ya kuumia Mguu.Luke Shaw kaumia tena na Hapa ni Dokta akimcheki kwa karibu sanaLuke Shaw kaumia tena na kulazimika kuondolewa UwanjaniMeneja wa Newcastle United Alan Pardew alipata muda akateta na wachezaji wake na kuwapa mbinuLuke Shaw akiondolewa Uwanjani huko Ugenini Selhurst ParkRooney nae yale yale!Rooney alipumzishwa!
Wachezaji wa Crystal Palace wakimsimamia Mwamuzi Michael Olivier baada ya kutoa penati kwa UnitedJuan Mata dakika ya 19 kipindi cha kwanza aliifungia United bao kwa mkwaju wa penati nao Crystal Palace walisawazisha kupitia mpira wa adhabu frii kiki iliyofungwa na Jason Puncheon dakika ya 57 kipindi cha pili na kufanya 1-1.Van Gaal akisalimiana na Meneja mwenzie Alan Pardew

Saturday, May 9, 2015


Stoke City XI: Butland, Cameron, Shawcross, Muniesa, Pieters, N'Zonzi, Whelan, Walters, Adam, Arnautovic, Diouf.
Akiba: Sorensen, Bardsley, Ireland, Odemwingie, Sidwell, Crouch, Wollscheid.

Tottenham XI: Lloris; Dier, ChiricheÈ™, Fazio, Vertonghen; Bentaleb, Mason; Lamela, Eriksen, Chadli; Kane.
Akiba: Vorm, Rose, Yedlin, Dembele, Stambouli, Townsend, Soldado.


Timu ya Simba Sports Club imeibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya JKT Ruvu na kushika nafasi ya 3 katika Ligi Kuu ya Vodacom iliyomalizika leo. ‪#‎VPL2015‬
Timu za Polisi Moro na Ruvu Shooting zimeshuka daraja.



Kutoka chini ya kwa chini ni kuhusu Kocha wa Bayern Munich kwenda Ligi Kuu England msimu Ujao wa 2015/2016 kufundisha Timu ya Man City.

 


Jermain Defoe dakika ya 85 kipindi cha pili aliwafungia bao Sunderland na kufanya 2-0 dhidi ya Everton. Ushindi huu umeipandisha Sunderland nafasi ya 14 wakiwa na pointi 36 huku Everton wakiwa nafasi ya 11 na pointi zao 44. Ukumbuke mpenzi wa bukobasports Sunderland wanamchezo wao mkononi hivyo mchezo wao wa leo ni 35, Everton wao wamecheza mchezo wao wa 36.
Danny Graham wa Sunderland  dakika ya 53 anaifungia bao Sunderland na kufanya 1-0 dhidi ya Everton kipindi cha pili.


 Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Tanga, Bw. Gabriel masanja  (wapili kulia) akipeana mkono na Bw. Rajpaul Singh Dhani (kulia) dereva wa gari ya mashindano iliyoiwakilisha benki hiyo katika mchezo wa mashindano ya magari uliyofanyika mkoani Tanga hivi katibuni. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Tanga.

Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Tanga, Bw. Gabriel masanja  (wa kwanza kushoto) pamoja na Bw. Rajpaul Singh Dhani (Wa tatu kushoto) dereva wa gari (iliyopo mbele yao)ya mashindano iliyoiwakilisha benki hiyo katika mchezo wa mashindano ya magari uliyofanyika mkoani Tanga hivi katibuni. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Tanga. 

waliotembelea blog