Thursday, September 10, 2015

Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Rhys Torrington (kulia) akibadilishana mikataba na Rais wa TFF, Jamal Malinzi leo 

RATIBA YA MECHI ZA RAUNDI YA KWANZA 

AFC vs  Polisi Mara Polisi Tabora vs Green Warriors Kariakoo Lindi vs Changanyikeni Dar Mkamba Rangers vs Ruvuma FC ya Kigoma Rhino ya Tabora vs Alliance FC ya Mwanza Panone vs Cocacola Kwanza ya Mbeya Polisi Moro vs Mshikamano Sports Sabasaba Utd vs Abdajalo ya Tabora Magereza Iringa vs Polisi Dar Mirambo vs Town Small Boys Ruvuma Abdajalo Dar vs Transcamp Ruvu Shooting vs Cosmopolitan Singida Utd vs Bulyhanhulu JKT Rwamkoma vs Villa Squad Wenda vs Madini Sports Arusha Pamba vs Polisi Dodoma.
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya Azam Media Limited leo imesaini Mkataba wa miaka minne na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kudhamini michuano ya Kombe la Shirikisho, zamani (FA) wenye thamani ya Sh. Bilioni 3.3.
Katika halfa iloyofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa jengo la Kisenga LAPF, Kijitonyama, Dar es Salaam, Rais wa TFF, Jamal Malinzi, amesema kwamba amefurahia kufanikisha azma ya kurejesha mashindano hayo.
Malinzi amesema kwamba duniani kote maendeleo ya soka yanatokana na kuwepo na mashindano mbalimbali yakiwemo ya Kombe la Shirikisho la nchi, ambayo yanashirikisha na klabu za chini hadi zile zinazoshiriki Ligi Kuu.
“Nitafurahi sana kuona klabu ya Daraja la Pili inashinda Kombe hilo, duniani kote Kombe hili lipo na klabu za chini zimekuwa zikiwapiga ‘visu’ wale wakubwa,” alisema Malinzi.
Aliongeza kuwa bingwa wa mashindano hayo atajinyakulia kitita cha Sh. Milioni 50 wakati kila timu itakayokwenda kucheza ugenini itapata Sh. Milioni tatu za safari na mwenyejii atapewa Sh. Milioni 1 ya maandalizi.
“Tumeona bingwa wa michuano hii apate Sh. Milioni 50 kwa sababu atakuwa amecheza mechi saba na yule wa Vodacom anayecheza michezo 30 anapata Sh. Milioni 70,” Malinzi aliongeza.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya TFF, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ alisema jana kuwa mashindano ya mwaka huu yatashirikisha klabu 64 na yataendeshwa kwa njia ya mtoano.
Kaburu, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Simba SC, amezitaja timu hizo kuwa ni pamoja klabu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Bara, timu 24 za Daraja la Kwanza na idadi kama hiyo za Daraja la Pili.
Alisema kwamba mshindi wa kombe hilo atapata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) mwaka 2017.
Torrington (kulia) wakitiliana saini Mkataba na Malinzi 
Malinzi akichezesha droo ya kuchagua timu za Raundi ya kwanza 
Meneja Masoko wa TFF, Peter Simon akitaja timu za kumenyana katika Raundi ya kwanza




ORODHA YA MABINGWA WA KOMBE LA FA: 

1967 Yanga SC (Dar es Salaam)
1985 Maji Maji (Songea)   
1995 Simba SC (Dar es Salaam)
1996 Sigara (Dar-es-Salaam)
1997 Tanzania Stars (Dar es Salaam)
1998 Tanzania Stars (Dar es Salaam)
1999 Yanga SC (Dar-es-Salaam)
2000 Mtibwa Sugar
2001 Simba SC (Dar-es-Salaam) 
2002 JKT Ruvu Stars (Pwani)
Alieleza kuwa timu 16 za Ligi Kuu ya Bara zenyewe zitaanzia raundi ya pili itakayoshirikisha klabu 32 na kuongeza kwamba wiki ya mechi za Kombe la FA hakutakuwa na michezo ya Ligi ya Bara.
Hii ni mara ya kwanza kihistoria michuano ya Kombe la FA kuwa na udhamini na miaka ya imekuwa ikiibuka na ‘kuyeyuka’ tangu mwaka 1967 kabla ya kupotea moja kwa moja mwaka 2002. Mara ya mwisho Kombe la FA lilifanyika mwaka 2002 na JKT Ruvu Stars ya Pwani ikaibuka bingwa baada ya kuifunga Baker Rangers ya Magomeni kwenye fainali. Bingwa wa kwanza wa Kombe la FA enzi hizo likiitwa Kombe la FAT ilikuwa Yanga SC mwaka 1967, na michuano hiyo haikufanyika tena hadi 1985 Maji Maji ya Songea ilipotwaa Kombe. Kombe la FAT likayeyua tena kabla ya kurejea miaka 10 baadaye, 1995 na Simba SC ikatwaa ubingwa kabla ya kupokonywa na Sigara mwaka 1996, ambao nao walilitema kwa Tanzania Stars mwaka 1997 iliyofanikiwa kulitetea 1998 kabla ya kupokonywa na Yanga SC 1999. Ubingwa wa FA mwaka 2000 ulikwenda kwa  Simba SC, waliopokonywa na Yanga SC mwaka 2001 kabla ya JKT Ruvu kuwa bingwa wa mwisho wa mashindano hayo mwaka 2002.
Klabu ya Tottenham Hotspur ambayo makao makuu yake ni jiji la London imemzuia winga wa kimataifa wa Korea Kusini Son Heung-Min kununua gari lenye rangi nyekundu. Spurs ambao wanajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu weekend hii dhidi ya Sunderland wametoa sharti hilo kwa Son Heung-Min.
Kwa mujibu wa mtandao wa mirror.co.uk Son Heung-Min anatajwa kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya soka kutokea bara la Asia, lakini amethibitisha kuzuiwa na viongozi wa Spurs kununua gari lenye rangi nyekundu kwa sababu ni rangi ambayo inatumiwa na wapinzani wao Arsenal.
Son-Heung-Min-signs-for-Tottenham
“Viongozi wa Tottenham tayari wameniambia siruhusiwi kununua gari lenye rangi nyekundu, nina furaha kucheza mechi yoyote ile dhidi ya Arsenal  na ninapenda kushinda kwa sababu mimi ni mshambuliaji, rekodi yangu ya ufungaji itaongea kwa ajili yangu”>>> Son Heung-Min
Heung-Min-Song
Son Heung-Min alisajiliwa na klabu ya Tottenham Hotspur kwa dau la pound milioni 22 akitokea klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani na kusaini mkataba wa miaka mitano, Son Heung-Min amecheza mechi 87 na kufunga magoli 29 akiwa na klabu ya Bayer Leverkusen.



.
.
Kazi yangu ni kuhakikisha nakusogezea kila stori inayonifikia na hapa ninayo stori iliyochukua headlines Sept 9,2015 ya msanii wa Hip Hop kutokea 96.0 (Tanga) Roma Mkatoliki ambaye single yake mpya ilizuiliwa kwenye baadhi ya vituo vya radio nchini.
Msanii huyo alipokutana na ripota wa millardayo.com aliweza kuelezea sababu zilizopelekea kuzuiliwa kwa single yake mpya iitwayo Viva Roma na kusema..’Kiukweli jana ndio ilikuwa tarehe 9 mwezi wa tisa ambayo nilitoa ahadi kwa watu kuwa nitaachia wimbo wangu mpya unaoitwa Viva Roma na asubuhi mapema kabisa kwenye ukurasa wangu wa instagram nilipost picha ikionesha napaki CD zangu nikiwa tayari kuisambaza kazi yangu mpya mimi na timu yangu nzima ya Tongwe Records; – Roma Mkatoliki
.
.
‘Ilikuwa saa saba nianze na Eatv Radio kwenye kipindi cha Planet Bongo, saa nane nitaenda XXL ya Clouds FM, halafu nitaenda Times FM, halafu nitaenda E FM, na Magic FM so nilikuwa natoa ratiba ya kuitambulisha wimbo wangu katika vituo mbalimbali vya radio’ – Roma Mkatoliki
‘Ila mpaka sasa tunavyoongea tumeshaisambaza katika vituo vyote mbalimbali sehemu ambayo bado ni kwenye mitandao tu kama blogs, website na nchi za jirani ila jibu nililopewa na baadhi ya vituo vya radio ni kwamba wameikataa kuicheza ngoma yangu kwasababu wanachodai kwamba ina maneno makali huku vituo vingine vikiwa vinacheza verse moja tu kiukweli imenisikitisha lakini kwa upande wa mashabiki wanasema wimbo ni mzuri na sio kama ninalaumu vituo vya radio ila ndio maamuzi yao


Kila siku team ya Hekaheka kutoka Clouds FM imekua ikituletea matukio mbalimbali yanayotokea ndani ya familia zetu.
Hekaheka ya leo inatokea Kahama ambapo mtoto wa miezi mitano aling’atwa na punda na kisha kukimbia naye umbali wa mita kama 300.
Shuhuda wa tukio hilo amesema mtoto huyo alikua amelala pembeni ya kibanda cha mama yake ambaye alikua anapika mara ghafla punda mmoja akaja kisha akamng’ata, akaanza kukimbia naye.
Mama wa mtoto amesema alikuwa amemkalisha chini huku yeye anapika, lakini akashangaa punda amemchukua mtoto wake na kuanza kukimbia naye.
Anasema baada ya mwendo mrefu yule punda alikutana na mtu mwenye fimbo ndipo akamuachia yule mtoto lakini akiwa tayari na majeraha mbalimbali na mpaka sasa amelazwa katika hospitali ya Kahama.
Daktari wa mifugo amesema punda pia anaweza kupata kichaa cha mbwa hivyo ni vyema wananchi wakajua hilo, pia anaweza kufanya hivyo akiwa katika wakati wa kutaka kujamiana.
Baada ya tukio lile wananchi wenye hasira waliwakamata wale punda wote wawili na kuwachoma moto.



Cristiano Ronaldo ni staa mkubwa kwenye soka, YES… Dunia inamjua, hii ni kumaanisha kwamba hata wasio na ushabiki kwenye soka jina lake wanalijua !!
1900832
Mastaa kama Michael Jordan wamestaafu kwenye Michezo lakini majina yao yako juu bado kutokana na kujiingiza pia kwenye biashara kubwakubwa Duniani… Ronaldo anahitaji hata ikitokea leo anaachana na soka, jina lake likumbukwe pia tena kwenye uzito wake !!
Ni dili juu ya dili kwa Cristiano Ronaldo… baada ya kuingia Mikataba mingi ikiwemo ya kutengeneza nguo na viatu vyenye jina lake, safari hii amezindua perfume zenye jina la ‘Legacy‘ na tayari zimesogezwa sokoni kuuzwa.
Hapa nimekuwekea Pichaz na Video, Ronaldo na watu wake wa karibu wakati wa uzinduzi huo…
ron
ron2
ron3
ron4
ron6
Hiki ni kipande cha Video ambacho ni tangazo la perfume yenyewe, sekunde 31 tu mtu wangu hiki hapa..

Wednesday, September 9, 2015


Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney, siku kadhaa nyuma alifikia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Uingereza Sir Bobby Charlton, usiku wa September 8 alivunja rekodi ya Sir Bobby Charlton kwa kufunga goli la 50.
2C1693CD00000578-3226944-image-a-70_1441746439612
Wayne Rooney alifunga goli la 50 kwa mkwaju wa penati  akiwa na timu yake ya taifa ya Uingereza wakati wa mchezo dhidi ya Switzerland wa kuwania kufuzu kucheza EURO 2016, mechi ilimalizika kwa Uingereza kuibuka na ushindi wa jumla wa goli 2-0.
2C16903E00000578-3226944-image-a-71_1441746470439
Baada ya mechi hiyo Rooney aliingia katika chumba cha kubadilishia nguo huku akipigiwa makofi na wachezaji wenzake pamoja na kocha na kukabidhiwa jezi namba 50 ambayo ni jumla ya magoli aliyofunga katika timu ya taifa ya Uingereza.
2C16911600000578-3226944-image-a-77_1441746577925
22
Hii video ya Rooney na wachezaji wenzie wakiwa dressing room.



Msanii wa Bongo Flava Diamond Platnumz anazidi kuipeperusha bendera ya Tanzania, Tuzo nyingi sana zinazidi kutambua juhudi na kazi ya Diamond  kwenye muziki wa Tanzania.
Good news kwako mtu wangu, mtu wetu Diamond Platnumz amepata nafasi nyingine kubwa ya kuiwakilisha Tanzania kwenye tuzo za kimataifa.
mtvema
Tuzo za MTV Europe Awards maarufu kama MTV EMA kwa mwaka huu wa 2015 zimemtaja Diamond Platnumz kuwa miongoni mwa wasanii kutoka Africa wanaowania kipengele cha ‘Best African Act’,  wasanii wengine waliobahatika kuingia kwenye kipengele hicho ni; Davido, AKA (South Africa) na Yemi Alade (Nigeria).
yemimtv
Yemi Alade ni msanii pekee wa kike kwenye kipengele hiki cha Best African Act.
davidoema
Davido kutoka Nigeria
akaema
AKA kutoka South Africa.
MTV EMA 2015 inahitaji mtu wa tano kukamilisha orodha ya ‘Best African Act’ mtu wangu na kama wewe ni mdau mkubwa sana wa muziki mzuri basi MTV EMA 2015 inakupa wewe nguvu na kibali cha kumchagua mtu wa 5 unaehisi atafaa kuchuana na Diamond Platnumza na wengine kwenye kipengele hiki..
ema2
kwenye wale watano waliopendekezwa wapo; Wizkid, KO (South Africa), Stone Bwoy (Nigeria), Cassper na DJ Arafat.
EMA
Kumpata mmoja kati ya watano hapo juu, utaratibu wa kuwapigia kura upo hivi… unaandika #MTVEMA ikifuatiwa na hashtag (#Nominate) na jina la msanii na kisha unatweet mara nyingi uwezavyo kwenye Twitter ili kumpata yule unayeona anastahili kufunga kipengele hiki.
EMA1
Tuzo za MTV EMA Awards 2015 zinafanyika tarehe 25 October jijini Milan, Italy. Mwisho wa kupiga kura ni tarehe 14 September 2015.

waliotembelea blog