Wednesday, September 9, 2015


Serena williams ameendelea kuwa bora zaidi duniani baada ya kumshinda dada yake Venus william katika mashindano ya US Open na kuzidi kusonga mbele.
vee

Serena ambaye anashika nafasi ya kwanza kwa rekodi bora duniani ameshinda dada yake kwa seti tatu ya 6-2 1-6 6-3 zilizompa nafasi ya kuweza kuingia kwenye mashindano ya nusu fainali huko New York,Marekani.
Serena Williams, left, hugs Venus Williams after winning their quarterfinal match at the U.S. Open tennis tournament, Tuesday, Sept. 8, 2015, in New York. (AP Photo/Julio Cortez)
Katika hatua ya nusu fainali,serena atachuana na mwanadada wa nchini Italia Roberta Vinci kesho.


Wakati mshambuliaji wa Italia na klabu ya AC Milan Mario Balotelli akiwa na wakati mgumu katika maisha yake ya soka, kwa kutokufanya vizuri msimu uliyomalizika katika klabu ya Liverpool kitu kilichochangia kutoitwa timu ya taifa. Mpenzi wake wa zamani Fanny Neguesha anaendelea kufurahia penzi lake jipya na Cheikhou Kouyate.
2C12498500000578-0-image-a-40_1441710062286
Fanny Neguesha ambaye amewahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Mario Balotelli, sasa yupo katika mahusiano na kiungo wa kimataifa wa Senegal na klabu ya West Ham United Cheikhou Kouyate baada ya muda mrefu kupita toka ameachana na Balotelli.
2C1247E600000578-3226285-image-a-19_1441713709198
Mrembo huyo na Balotelli waliachana na mwezi September mwaka jana, baada ya hapo mrembo huyo aliingia katika mahusiano na Cheikhou Kouyate. Fanny na Cheikhou Kouyate inaripotiwa kwa mara ya kwanza walikutana photoshoot London, hapo ndio mwanzo wa penzi hilo, ila kwa hivi karibuni wamekuwa wakionekana kuweka wazi uhusiano wao.
2C12EECD00000578-3226285-image-a-55_1441711645712
2C124AFB00000578-3226285-image-a-14_1441713616812
2C124B0100000578-3226285-image-m-13_1441713609827
2C13156400000578-3226285-image-a-25_1441714276246
2C1247B900000578-0-image-a-39_1441710013609
2C12479500000578-0-image-a-36_1441709935783
2C1249C100000578-0-image-a-42_1441710110461
2C124A3A00000578-3226285-image-a-24_1441713748006


Wayne Rooney alifunga penati dakika ya 84 na kufanya bao kuwa 2-0 dhidi ya timu ya Switzerland. Wayne Rooney amevunja rekodi ya Sir Bobby Charlton wa England baada ya kuifungia bao timu yake ya Taifa usiku huu kwa mkwaju wa penati.Kane akishangilia bao lake


Embedded image permalinkBarcelona wamezoa Tuzo ya Klabu Bora Ulaya kwa Msimu wa 2014/15 iliyotolewa na Chama cha Klabu za Soka Ulaya, ECA(European Club Association).
Tuzo hiyo kwa Barcelona imekuja baada ya wao kutwaa Trebo, yaani Ubingwa wa La Liga, Copa del Rey na UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu uliopita.

Sherehe za utoaji Tuzo zilifanyika Jana huko Geneva, Uswisi na Tuzo nyingine walitwaa Klabu ya Ukraine FC Dnipro Dnipropetrovsk waliopewa Tuzo ya Maendeleo Bora Mchezoni kwa kufika Fainali ya EUROPA LIGI bila kutarajiwa na kufungwa na Sevilla ya Spain.
Tuzo ya Ubora kwa Jamii na Programu Bora za Kijamii ilikwenda kwa Arsenal ambao wametambuliwa kwa mchango wao mkubwa kwa Jamii ya Jiji la London kukabiliana na tatizo la ajira kwa Vijana.
Tuzo ya 4 iliyotolewa na ECA ni ile ya Mafanikio Bora ambayo ilibebwa na Klabu ya Estonia Levadia Tallinn kwa mpango wao uitwao 'Pamoja Tutasonga' ambao ulilenga kusaidia Walemavu wanaohitaji msaada wa kuongozwa na Mbwa ili kuingia kirahisi Uwanjani kwa ajili ya Mechi.


Mechi za Makundi ya EURO 2016, Kombe la Mataifa ya Ulaya, zinakamilika Leo kwa ile Raundi ya Mechi za Septemba na kubakisha Mechi 2 kwa kila Timu ambazo zitachezwa Mwezi ujao huku tayari Timu 3 zimefuzu kuingia Fainali.
Fainali za EURO 2016 zitachezwa Mwakani huko France na Raundi hii ya Mechi imezifanya England, Iceland na Czech Republic waungane na Wenyeji France kwenye Fainali.
Bado zipo nafasi 20 kukamilisha idadi ya Timu 24 kwenye Fainali ambazo huchukuliwa na Washindi 9 wa Makundi, Washindi wa Pili 9, Mshindi wa 3 Bora mmoja pamoja na Timu 4 zitakazoshinda Mechi za Mchujo zitakazoshitikisha Washindi wa 3 Wanane.

Leo England wanacheza Mechi ya kukamilisha Ratiba ya Kundi E dhidi ya Switzerland Uwanjani Wembley Jijini London na macho yote yapo kwa Kepteni wao Wayne Rooney kama ataweza kuvunja Rekodi ya Ufungaji Bora England baada Juzi kwenye Mechi na San Marino kufunga Bao moja na kumfikia Mfungaji Bora Sir Bobby Charlton mwenye Bao 49 kwa Mechi 106.

Hii Leo ataichezea England Mechi yake ya 106.


RATIBA:
Jumanne Septemba 8

21:45 Belarus vs Luxembourg
21:45 Macedonia vs Spain
21:45 Slovakia vs Ukraine
21:45 England vs Switzerland
21:45 Slovenia vs Estonia
21:45 Lithuania vs San Marino
21:45 Liechtenstein vs Russia
21:45 Sweden vs Austria
21:45 Moldova vs Montenegro



.
.
Unakumbuka ile ishu ya bondia wa ngumi Francis Cheka ya kumpiga na kumuumiza meneja wa baa yake akimtuhumu kusababisha hasara?
Sasa good news ninayotaka kukusogezea ni kwamba bondia huyo wa mchezo wa masumbwi akiwa anatumikia kifungo cha nje kwa sasa anatarajia kwenda nchini Uingereza tarehe 15 mwezi huu kwenye mchezo wa masumbwi.
Leo sept 8 alikuta na ripota wa millardayo.com na kuzungumza machache kuhusiana na taratibu za safari yake pamoja na kifungo anachotumikia nje…’Kwanza namshukuru mwenyezi mungu niko katika hali ya salama kesi yangu katika ustawi wa jamii inaendelea vizuri na ustawi wa jamii niko nao katika hali ya kawaida sababu wao wanajua umuhimu wangu na kuweza kujua mimi Francis Cheka nahitaji nini kwa mashabiki wangu, mimi ni mtanzania ambaye ninawajenga umma wa watanzania kwenye michezo ya boxer’ – Francis Cheka
‘Ustawi wa jamii wamenipa ruksa ya kwenda kupigana kwenye pambano hilo nchini Uingereza nategemea kwenda tarehe 15 mwezi huu na mkurugenzi wa ustawi wa jamii ameweza kuniambia mawili matatu kuhusiana na taratibu au kitu gani ninachotakiwa kukifanya ili niweze kufanikisha safari yangu ya Uingereza’ – Francis Cheka

Tuesday, September 8, 2015




RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA 

Septemba 12, 2015
Ndanda FC Vs Mgambo JKT
African Sports Vs Simba SC
Majimaji FC Vs JKT Ruvu
Azam FC Vs Prisons
Stand United Vs Mtibwa Sugar
Toto Africans Vs Mwadui
Mbeya City Vs Kagera Sugar
Septemba 13, 2015
Yanga SC Vs Coastal Union
Septemba 16, 2015
Yanga SC Vs Prisons
Mgambo JKT Vs Simba SC
Majimaji FC Vs Kagera Sugar
Mbeya City Vs JKT Ruvu
Stand United Vs Azam FC
Toto Africans Vs Mtibwa Sugar
Ndanda FC Vs Coastal Union
Septemba 17, 2015
Mwadui FC Vs African Sports
Septemba 19, 2015
Stand United Vs African Sports
Mgambo JKT Vs Majimaji FC
Prisons Vs Mbeya City
Yanga SC Vs JKT Ruvu
Septemba 20, 2015
Mwadui FC Vs Azam FC
Mtibwa Sugar Vs Ndanda FC
Simba SC Vs Kagera Sugar
Coastal Union Vs Toto Africans
Septemba 26, 2015
Simba SC Vs Yanga SC
Coastal Union Vs Mwadui FC
Prisons Vs Mgambo JKT
JKT Ruvu Vs Stand United
Mtibwa Sugar Vs Majimaji FC
Kagera Sugar Vs Toto Africans
Septemba 27, 2015
African Sports Vs Ndanda FC
Azam FC Vs Mbeya City
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
LIGIi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2015/2016 inatazamiwa kuanza kutimua vumbi jumamosi Septemba 12, 2015 kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja tofauti nchini.
Ndanda FC ya Mtwara watakua wenyeji wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Nagwanda Sijaona mjini Mtwara, Wana kimanumanu African Sports watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Wana Lizombe Majimaji wakiwa wenyeji wa maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Azam FC watakua wenyeji wa Tanzania Prisons kaika uwanja wa Chamazi Complex, Stand United FC chama la wana watawakaribisha Mtibwa Sugar katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Toto Africans watawakaribisha Mwadui FC uwanja wa CCM Kirumba na Mbeya City watacheza na Kagera Sugar katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Jumapili Ligi Kuu itaendelea kwa mchezo mmoja tu utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo mabingwa watetezi wa kombe hilo Yanga SC watawakribisha wagosi wa kaya Coastal Union.
Katika hatua nyingine klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera itatumia  Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kwa mechi zake za nyumbani dhidi ya Toto Africans (Sept 26), JKT Ruvu (Sept 30), Tanzania Prisons (Oct 4) na Yanga (Oct 31).
Mabadiliko hayo yamefanyika kupisha shughuli ya uwekaji nyasi bandia inayoendelea kwenye uwanja wao wa Kaitaba mjini Bukoba unaofanywa na wataalamu kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

waliotembelea blog