Friday, August 21, 2015


Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesema haikuwa nia ya Chelsea kuipiku Manchester United ili kumsaini Pedro kutoka Barcelona.
Man United walikuwa tayari wameshakubaliana na Barcelona kuhusu Uhamisho wa Pedro ambae nae alishaafika maslahi binafsi na Man United lakini Dakika za mwisho Chelsea ikaingia na kumsaini.
Habari toka Old Trafford zilitoboa kuwa Meneja Louis van Gaal ndie alieamua kutomsaini Pedro baada kubainika uhusiano wake wa karibu na Mchezaji mwingine wa zamani wa Barcelona, Kipa Victor Valdes, ambae yuko Man United lakini sasa ana bifu kubwa na Van Gaal kiasi cha kutimuliwa toka Timu ya Kwanza na sasa kuwekwa kwenye Listi ya Wachezaji wanaouzwa.
RATIBA:
Jumamosi Agosti 22

1445 Man United v Newcastle
1700 Crystal Palace v Aston Villa
1700 Leicester v Tottenham
1700 Norwich v Stoke
1700 Sunderland v Swansea
1700 West Ham v Bournemouth

Jumapili Agosti 23

1530 West Brom v Chelsea
1800 Everton v Man City
1800 Watford v Southampton

Jumatatu Agosti 24

2200 Arsenal v Liverpool



Klabu ya Manchester United ambayo msimu huu imedhamiria kupata saini za wachezaji mahiri watakaoweza kurejesha heshima ya kikosi chao kwani toka aondoke Sir Alex Ferguson, klabu hiyo imekuwa na wakati mgumu wa kurudisha makali yake ya awali.
manchester_united_logo_1280x1024
Njia pekee Man United walioamua kuitumia kukijenga upya kikosi chake ni kufanya usajili pekee ndio utakaoweza kuirudisha Man United katika ubora wake, kwa hivi siku za karibuni klabu ya Man United ilikuwa ikihitaji kuipata saini ya beki wa Real Madrid Sergio Ramos na kutumia kigezo cha Real Madrid kumtaka De Gea ili iweze kuwashawishi Real Madrid kumuachia beki huyo.
1420198841_extras_noticia_foton_7_2
Baada ya klabu ya Real Madrid kuweka ngumu na kugoma kumuuza beki huyo kwenda Man United na kumpa mkataba mpya, Man United waliamishia mawazo kwa beki kutokea Ureno anayeitumikia Real Madrid ya Hispania Pepe wakiwa na matumaini ya kumpata, August 21 Real Madrid wametangaza kumsainisha mkataba mpya beki huyo.
Jose Mourinho ni miongoni mwa makocha wanaopenda wachezaji wenye asili ya Afrika August 19 2015 habari za kumsajili beki wa kimataifa wa Ghana aliyekuwa anaichezea klabu ya FC Augsburg ya Ujerumani Baba Rahman na kujiunga na klabu ya Chelsea kwa ada ya uhamisho ya pound milioni 21.7.
2B78503700000578-3202562-image-a-28_1439923425179
Beki huyo wa Ghana mwenye umri wa miaka 21 huenda atapangwa kucheza beki ya kushoto namba ambayo ilikuwa ikichezwa na beki wa kihispania Cesar Azpiliceuta ambaye baada ya ujio wa Baba, Stamford Bridge Cesar Azpiliceuta ataenda kucheza upande wa  kulia.
Baba-Rahman-wanted-by-Chelsea
Klabu ya Chelsea ambayo imefanikiwa kumnasa Baba bado haijakata tamaa ya kusaka saini ya beki wa kiingereza anayeichezea klabu ya Everton John Stones licha ya ofa ya pound milioni 30 kukataliwa hivyo inajiandaa kutuma ofa nyingine ya pound milioni 40 ndani ya masaa 48.

Thursday, August 20, 2015


Fowadi wa Barcelona Pedro sasa atahamia Chelsea baada ya Klabu hiyo kukubali kulipa Pauni Milioni 22 kwa mkupuo kitu ambacho Manchester United waligomea kulipa.
Kwa muda mrefu iliaminika kuwa Pedro atatua Old Trafford huku kukiripotiwa kuwa tayari ameshaafikiana maslahi yake binafsi lakini kusita kwa Man United kulipa kwa mkupuo mmoja Dau ambalo Barca walikuwa wakitaka kumetoa mwanya kwa Chelsea kutumbukia na kukubali kulipa Dau hilo lote na kumnasa Staa huyo.

Man United walikuwa tayari kulipa Dau la Pauni Milioni 17.7 mbele na kisha kulipa pole pole Pauni Milioni 3.6 zikiwa nyongeza ambazo zitaendana na mafanikio atakayopata Mchezaji huyo akiwa na Man United.
Kitu hicho Barca waligomea na kutaka Fedha zote kwa mkupuo na hapo ndipo Chelsea wakawapiku Man United.
Inatarajiwa wakati wowote kuanzia sasa Pedro, mwenye Miaka 28, atapimwa Afya yake huko Stamford Bridge na kisha kusaini Mkataba.


Kiungo wa kimataifa wa Cameroon ambaye amewahi kuichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza kwa muda mrefu kabla ya kutimkia FC Barcelona ya Hispania Alex Song na msimu uliopita kuitumikia klabu ya West Ham United ya London kwa mkopo akitokea FC Barcelona amepoteza matumaini ya kuendelea na West Ham United.
Song alikuwa na matumaini ya kubakia katika kikosi hicho baada ya kuwa hana namba katika kikosi cha kwanza cha FC Barcelona ya Hispania hivyo matumaini ya kujiunga jumla na klabu hiyo yalikuwa makubwa baada ya kufanya vipimo vya Afya na kufuzu, taarifa zilizotoka August 19 ni kuwa West Ham wamesitisha mpango huo.
Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu golikipa mkongwe na mahiri Juma Kaseja kuwa bila timu na kuhusishwa kujiunga na vilabu mbalimbali hatimaye uvumi huo umemalizika August 19 baada ya kusaini mkataba wa miezi sita wa kuitumikia klabu ya Mbeya City kutoka Jijini Mbeya.
IMG-20150819-WA0008 (1)
Mkataba wa Juma Kaseja wa kujiunga na klabu ya Mbeya City umesainiwa August 19 mbele ya meneja wake mpya Athumani Tippo hivyo huo ni mwisho wa uvumi wa habari za Juma Kaseja atacheza wapi msimu ujao, taarifa hizo zinakuwa pigo kwa kocha wa Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kiwelu ambaye alikiri katika vyombo vya habari kuwa ana hitaji huduma ya Kaseja kikosini mwake.
kaseja atua mbeya city 4
Kabla ya kusaini mkataba na Mbeya City Juma Kaseja alikuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha zaidi ya miezi nane baada ya kuingia katika mgogoro wa kimkataba na iliyokuwa klabu yake ya zamani ya Yanga nakufanya kesi hiyo kutinga mahakamani.

waliotembelea blog