Tuesday, August 5, 2014


Teaming up: Cristiano Ronaldo and James Rodriguez give the thumbs up at Real Madrid training 
Wamekutana: Cristiano Ronaldo na James Rodriguez wakitoa dole kuashiria mambo 'supa' wakati wa mazoezi ya Real Madrid.
MWANASOKA BORA wa dunia, Cristiano Ronaldo amekutana na kijana mpya wa Real Madrid James Rodriguez katika mazoezi ya klabu hiyo mjini Madrid nchini Hispania.
Rodriguez  alijiunga na mabingwa hao wa Ulaya kutokea klabu ya Monaco kwa dau la paundi milioni 60 baada ya kuonesha kiwango kikubwa katika fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu na kutwaa kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora wa mashindano.
Baada ya mapumziko akitokea kombe la dunia kuiwakilisha Colombia, nyota huyo aliripoti katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa Valdebebas HQ ambapo aliungana na wenzake.
Close ball control: Ronaldo works with the football during training at Valdebebas
Ronaldo akifanya mazoezi katika uwanja wa Valdebebas
Keep it up: Real stars (from left) Ronaldo, Karim Benzema, Rodriguez and Raphael Varane during the session
Ona kitu hicho: Nyota wa Real  (kutoka kushoto) Ronaldo, Karim Benzema, Rodriguez na Raphael Varane wakati wa mazoezi ya Real Madrid


Jan Poulsen alirithi mikoba ya Mbrazil Marcio Maximo kuifundisha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars mwaka 2010



TAIFA Stars imekuwa timu ya ‘Tia maji Tia maji’ kwa miaka mingi, lakini kwasasa kuna haja ya kuanza upya kuijenga timu hii.
Kumbukumbu: mwaka 1980 Stars ilishiriki fainali za mataifa ya Afrika zilizofanyika nchini Nigeria.
Kuanzia hapo mpaka leo hii, imekuwa ndoto ya mchana kwasababu ya mipango mibovu katika soka la Tanzania.
Mwaka 2009, Stars ilishiriki mashindano mengine makubwa ya mataifa ya Africa kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani, CHAN, nchini Ivory Coast.
Wakati inakwenda Ivory, Stars chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo ilionekana kufufuka na kulikuwa na morali kubwa kwa wachezaji, viongozi na mashabiki kwa ujumla.
Baada ya kuondoka kwa Maximo mwaka 2010, TFF ilimteua Mdenish Jan Poulsen. Mzee huyu alikuwa na mipango mizuri, lakini ilionekana kushindikana kutokana na uharaka wa Watanzania.
Ni kweli Stars ilishuka kiwango ukilinganisha na kipindi cha Maximo, lakini Jan alikuwa na mipango ya muda mrefu, jambo ambalo ni adui wa Watanzania wengi.
Njia za mkato zinapenda kweli, eti leo hii mtu anatafakari kufuzu kombe la dunia au Afcon 2015, kwa mipango ipi?
Siku moja wakati anatoa kozi kwa makocha wa Tanzania alichora mchoro katika ubao.
Wote walioenda shule wanajua mbao za kuandikia wakati walimu wanafundisha zilivyo. Rudisha kumbukumbu.
Jan aliandika  pointi A chini kabisa ya ubao na akaandika pointi B juu kabisa ya ubao.
Akasema Tanzania ipo pointi A ambapo soka la Tanzania lipo. Hicho ni kiwango cha chini kabisa, lakini soka hilo linatakiwa kufikia pointi B, ngazi au kiwango ya juu kabisa.
Mdenish huyo aliuliza swali, tunafikaje pointi B?. Akafafanua kuwa ili kufika pointi B, hapa katikati kuna kitu kinaitwa mchakato ‘Process’.
Huu mchakato unajumuisha kuandaa mipango sahihi, mfumo sahihi wa soka, hususani soka la vijana.
Jan alieleza kuwa ili kufanikiwa kufika Pointi B, lazima kuwekeza muda na fedha za kutosha kuandaa timu za vijana, miundo mbinu ya soka, kuandaa makocha wenye ueledi wa juu na kuwa na viongozi sahihi katika nafasi sahihi.
Kim Poulsen alirithi mikoba ya Mdenish mwenzake, Jan Poulsen kuinoa Taifa Stars

Wakati anayasema hayo, alionekana kugundua matatizo ya wachezaji wa Tanzania. Alipoondoka na kumuachia Kim Poulsen, mambo yalionekana kuwa poa, lakini ghafla watu wakasitisha programu za kim na kumleta Mart Nooij.
Siku Kim anaaga pala TFF, aliongea vitu vingi, lakini nilishika zaidi kitu alichosema ‘Things Takes Time’ (TTT). Hapa kocha huyu alimaanisha vitu vinahitaji muda. Soka linahitaji muda.
Lazima kuwa na uvumilivu unapojenga timu. Kwa maana yake yeye, Kim alikuwa anajenga timu na alikuwa na program ya muda mrefu hasa katika soka la vijana, lakini kutokana na uchu wa kutaka kufuzu AFCON 2015 akamtimuliwa.
Viongozi wa juu wa TFF walikaririwa mara kadhaa wakisema kwa vyovyote vile, kwa kumwaga damu uwanjani, lazima Taifa Stars iende AFCON 2015.
Tayari Kim alisema mapema kuwa malengo yake yalikuwa AFCON 2015 nchini Morocco na sio kombe la dunia 2014 au CECAFA Senior Challenge Cup 2014 nchini Kenya, lakini watu wakata mafanikio ya haraka haraka.
Mpira haulazimishwi. Lazima mipango sahihi iweke na uvumilivu uwepo.
Busara za Kim na Jan Poulsen si za kuziacha hata kidogo. Walikuwa na maana kubwa, tena ile ile aliyonayo Mart Nooij. Sema namna viongozi wanavyochukuliwa mambo kwa haraka ndio matokeo ya kule Msumbiji mwishoni mwa wiki iliyopita.
Enzi za Marcio Maximo akiifundisha Taifa Stars (2006-2010)

TFF wamekuwa wakijitahidi kuiandaa timu, kwa mfano mwaka huu waliweka kambi Botswana kuiwinda Msumbiji na kufanya mpango wa maboresho ya Taifa Stars ingawa kwa asilimia 500 ‘umefeli’.
Lakini tatizo ni lile lile na viongozi wanalijua kuwa aina ya wachezaji waliopo sasa wamekosa vitu vingi vya kimbinu na kiufundi kwasababu wengi wao walikosa misingi ya mpira enzi za utoto wao.
Nadhini ni lazima turudi nyuma na kuwekeza katika soka la vijana.
Unajua kwa mara ya kwanza nafasi nzuri zaidi ambayo Tanzania ilishika katika viwango vya FIFA? Hii ni mwaka 1965 ambapo ilishika nafasi ya 65.
Wachezaji wengi wa timu ya 1965 ndio walioipeleka Taifa Stars michuano ya mataifa ya Afrika 1980 nchini Morocco.
Asubuhi njema!


Karibuni tena Dodoma Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la kutunga Katiba ya nchi yetu. Sote tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu wetu kwa kuendelea kutupa uhai na afya hadi leo kutuwezesha kuwepo ndani ya ukumbi huu. Tupo humu ili tuitekeleze kazi waliyotukabidhi Watanzania wenzetu milioni arobaini na sita (46) ya kuwapatia Katiba mpya. Dhamana hii ni nzito na haistahili kufanyiwa ajizi.
Tunaendelea na shughuli zetu za Bunge Maalum kwa kuzingatia Kanuni ya 30 (1) inayosema
Akidi kwa kila kikao cha Bunge Maalum isipokuwa wakati wa kupitisha uamuzi wa Bunge Maalum itakuwa ni nusu ya Wajumbe wote wa Bunge Maalum“.
Nimetaarifiwa na Katibu kwamba wajumbe waliokuja Dodoma kuhudhuria ni zaidi ya robo tatu ya Wajumbe wote wa Bunge Maalum. Nawashukuruni nyote kwa kuja hapa Dodoma ili kutimiza wajibu wenu.
Kwa niaba yenu, nawashukuru Watanzania wenzetu wote ambao kwa mamilioni wamedhihirisha utashi mwema wa kisiasa kwa kuunga mkono hatua ya Bunge Maalum kuendelea na kazi zake hadi tuipate Katiba inayopendekezwa ambayo wataipigia kura ya maoni. Kipekee na kwa niaba yenu, nawashukuru kwa dhati viongozi wetu wa dini wa madhehebu yote wanaloliombea Taifa hili mafanikio Bunge Maalum, wakitanguliza utaifa pamoja na amani ya nchi na umoja ndani ya nchi na siyo ubinafsi na maslahi ya makundi.
 Kwa leo sikupenda sana kuzungumzia hoja mbali mbali zinazotawala magumzo ya mchakato wa Katiba mpya hapa nchini, magumzo yanayoendeshwa na makundi maalum kwa jazba na hata matusi. Hata hivyo nalazimika kutoa maelezo ya ufafanuzi kuhusu upotoshaji mkubwa unaoendeshwa na baadhi ya watu kuhusu Bunge Maalum. Nikiwa Mwenyekiti wenu ninao wajibu wa kuwafafanulia wananchi kuhusu uhalali wa shughuli za Bunge Maalum linaloendelea na utaratibu wa shughuli zetu.
Ni Rasimu ya Tume au la
Wapo wanaodai kuwa eti hapa Bungeni hatujadili Rasimu ya Tume. Tuhuma hii haina ukweli hata kidogo. Msingi wa majadiliano yote tangu tumeanza ni Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Katiba. Utaratibu ni kwamba pale ambapo wajumbe wanaona panafaa kurekebishwa wanafanya hivyo. Maana ya rasimu ni andiko ambalo halijajitosheleza bila kupata ithibati ya taasisi ya juu zaidi. Anayekabidhiwa rasimu anayo haki na mamlaka ya kuirekebisha. Vinginevyo kujadili rasimu hakuna sababu. Itakuwa ni jambo la ajabu na lisilo na mantiki yoyote kuwa taasisi iliyopewa mamlaka ya kujadili Rasimu ikishaijadili iiache ibaki kama ilivyokuwa wakati ilipowasilishwa!
 Je suala ni muundo wa Muungano tu?
Maudhui ya Rasimu yanajumuisha baadhi ya masuala muhimu yafuatayo:
-      Kuimarisha Muungano wetu kwa kuleta uwiano     bora zaidi wa mamlaka ya Zanzibar na Tanzania      Bara ndani ya Muungano
-      Kuimarisha haki za binadamu ili kuwawezesha      raia wa kawaida kufaidi uhuru wa demokrasia     bila ubabe na dhuluma
-      Kuzuia wachache kufuja rasilimali za taifa bila       kujali maslahi ya wengi na ya vizazi vijavyo.
-      Kujenga uwiano sahihi na wenye haki baina ya      wanawake na wanaume katika nafasi za uongozi.
-      Kubainisha hatua zenye kuleta matumaini mapya ya maendeleo kwa makundi maalum ya vijana     wakulima wadogo, wafugaji, wafanyakazi wa ngazi   za kawaida, walemavu, wafanya biashara wadogo   na wajasiriamali wengine.
-      Kuweka msingi imara wa kutungwa kwa sheria      kakamavu za kuzuia ukandamizaji wa raia,        unyonyaji, wizi wa mali ya umma, rushwa,    hujuma dhidi ya uchumi na kuzuia mapato        haramu na fedha chafu.
-      Kutambua haki za ardhi kwa wakulima, wafugaji    na wajasiriamali wengine ili kupunguza migongano na migogoro.
-      Kuweka Misingi ya utawala bora inayozingatia        uadilifu, sifa stahiki na ufanisi.
-      Kuwezesha kutungwa kwa sheria bora zaidi     zitakazosimamia chaguzi zilizo za haki na huru    zaidi pamoja na kuwepo Tume za Uchaguzi       zilizoboreshwa.
Zaidi ya hivyo, yapo mapungufu katika Rasimu iliyopo kwa kuachwa masuala ya kuwezesha Serikali za mitaa; kutoa maelekezo kuhusu masuala ya matumizi ya ardhi na rasilimali nyingine za Taifa. Nini kinatuzuia kuiboresha Rasimu kwa kuyaongeza mambo haya ndani ya Katiba kwa faida ya Taifa?
 Yote haya ni masuala muhimu ambayo yamo ndani ya rasimu na wakati wake wa kuyaweka sawa ndiyo huu. Pamoja na umuhimu wake suala la muundo wa Muungano si suala la kutulazimisha tuyaahirishe mazuri yote yaliyomo katika Rasimu tuliyopewa.
 Uhalali wa Shughuli za Bunge Maalum
Pamoja na uhalali wa kisheria wa Bunge hili Maalum kuendelea kufanya kazi zake, linao pia uhalali wa kisiasa kutokana na sifa za uwakilishi wetu na pia maudhui yaliyomo ndani ya Rasimu. Kutofautiana maoni hakuwapi hadhi tofauti baadhi ya wajumbe kujiona wao wana uhalali zaidi mbele ya wananchi kuliko wenzao. Ndiyo maana utaratibu umewekwa wa kupiga kura na wa maridhiano. Utamaduni mpya unaoanza kujengwa na baadhi ya viongozi wa jamii wa kususia mijadala halali na kwenda nje kuelezea hoja za upande mmoja hauna nafasi katika Tanzania jamii isiyotaka fujo na utengano.
 Wajumbe wa Bunge Maalum wanaoendelea na kazi mjini Dodoma ni wateule wa Rais kwa niaba ya wananchi kwa kazi ya kutunga Katiba. Kazi hii haiwezi kusitishwa kwa sababu tu wajumbe wachache wameisusia. Tutazingatia matakwa ya sheria katika kufikia hatma ya mchakato wa Katiba.
 Mabadiliko ya Kanuni
Kama nilivyoeleza hapo mwanzo, Rasimu ina jumla ya sura kumi na saba (17) zenye mambo mengi yenye maslahi kwa Watanzania wote. Kwa muda tuliopewa wa siku sitini (60) isingewezekana kuikamilisha kazi tuliyopewa ndani ya muda. Ikumbukwe kwamba kwa Kanuni zilivyo, kila sura mbili zinahitaji siku tisa kuzifanyia kazi. Kwa njia hiyo, ingetuchukua siku takriban mia moja thelathini (130) ili kuikamilisha kazi hii! Pendekezo la msingi hapa ni kwamba Kamati zetu kumi na mbili (12) zizingatie na kuzijadili sura kumi na tano (15) za Rasimu na pia zikamilishe uandishi wa sura mbili zilizojadiliwa awali na ikibidi ziongeze sura ambazo zitadhihirika kuwa ni muhimu. Naamini mtiririko huu utatuwezesha kuwa na mpangilio bora zaidi wa sura na ibara katika Katiba mpya. Tusingependa na wala isingefaa kuomba tena muda wa ziada wa kazi ya Katiba ndio maana tunafanya mabadiliko ya Kanuni. Kamati ya Uongozi iliyoketi Dar es Salaam tarehe 28 Julai 2014 imependekeza yafanywe mabadiliko ya Kanuni za Bunge Maalum kuwezesha kazi ikamilike ndani ya muda tuliopewa. Kwa hiyo nitawaomba tuyatafakari mapendekezo ya mabadiliko ya Kanuni na hatimaye kuyapitisha ili ratiba ya kazi zetu iende sawa. Nitawaomba muikubali ratiba iliyogawanywa leo na pia mkubali kuzibadilisha Kanuni kwa lengo nililolieleza hapa.
 HITIMISHO
Pamoja na maoni ya kila namna yanayoendelezwa kujadili mchakato wa Katiba nje ya Bunge hili, ni muhimu wahusika wapunguze jazba, chuki na upotoshaji. Bunge Maalum lisaidiwe kwa mawazo chanya ili limalize kazi yake.
Sisi tuliomo humu katika Bunge Maalum tuna wajibu wa kuifanya kazi yetu kwa umakini na kwa uadilifu ili kazi yetu iwe bora. Tujadiliane kwa uungwana. Tofauti za mawazo zisitufanye tuingize chuki na maneno yasiyofaa. Katika mabadiliko ya Kanuni nashukuru sasa Kiti kimepewa mamlaka ya kushughulikia utovu wa nidhamu ndani ya wakati. Lakini ninaamini haitakuwa lazima kwangu mimi au Makamu Mwenyekiti kutumia nguvu za mamlaka yetu ila tu pale itakapobidi.
 Nawatakia nyote Mkutano wenye mafanikio kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
 MUNGU IBARIKI TANZANIA!
 Samuel Sitta – MB
MWENYEKITI BUNGE MAALUM LA KATIBA

Monday, August 4, 2014


Kocha mpya wa Uholanzi Guus Hiddink amemteua Pierre van Hooijdonk kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya nchi hiyo. 
Pia Hiddink amemwambia nahodha wa timu hiyo Robin van Persie kupatana na Pierre van Hooijdonk ambaye waligombana wakati wa fainali za kombe la dunia, wakati Pierre van Hooijdonk aliposema Van Persie hafai kucheza kwenye mchezo wa mshindi wa 3 kutokana na kutokuwa na kiwango kinachostahili.





Mheshimiwa Zitto Kabwe - "#TaifaStars imecheza mechi nyingi ambazo nimehudhuria, ndani na nje ya nchi. Sijaona wachezaji wakitokwa machozi kama Jana. Ndani ya chumba cha kubadilisha nguo niliona uchungu na machozi ya vijana wetu. Kwa pamoja walikuwa wanasema 'nyumbani kama ugenini, ugenini ugenini'. Somo kubwa sana hilo."



MABINGWA wa Ulaya, Real Madrid wamemsajili mlinda mlango na shujaa wa Costa Rica katika fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil, Keylor Navas.
Navas amekubali kusaini mkataba wa miaka sita na sasa anaingia katika ushindani na kipa Iker Casillas kwasababu kuna dalili kuwa kipa mwingine Diego Lopez anasepa zake.
View image on Twitter
Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao rasmi wa klabu ya Real Madrid jana jioni inasomeka: "Real Madrid CF na Levante UD zimefikia makubaliano juu ya uhamisho wa Keylor Navas, ambaye atajifunga klabuni kwa misimu sita ijayo""Mchezaji atatambulishwa jumanne, Agosti 5, saa 7:00 mchana (saa za Hispania) kwenye uwanja wa Bernabeu, baada ya kuchukuliwa vipimo vya afya".


All smiles: Ashley Young joins team-mates Wayne Rooney and Danny Welbeck for Manchester United training
Tabasamu 'bab kubwa': Ashley Young akiungana na wachezaji wenzake Wayne Rooney na Danny Welbeck kwenye mazoezi ya Manchester United.
LOUIS van Gaal atawachana macho kwa macho wachezaji wake ambao wataachwa na Manchester United baada ya kumaliza ziara ya Marekani ambapo amewapa nafasi ya kumuonesha viwango vyao.

Anderson, Nani, Javier Hernandez, Shinji Kagawa na Marouane Fellaini ni miongoni mwa majina makubwa yaliyopo katika mstari mwekundu kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Lakini inafahamika kuwa Van Gaal  hatakuwa na huruma kabisa ingawa hajafanya maamuzi ya hadharani.
'Nitafikia maamuzi baada ya ziara hii,' alisema. Nimewapa nafasi ya kucheza wachezaji wote na najua zaidi hata kabla ya ziara.
Plenty to ponder: Louis van Gaal will tell his unwanted players that they are free to find another club
Louis van Gaal atawaambia wachezaji asiowahitaji kuwa wapo tayari kutafuta timu nyingine.

'Kwa sasa nimefikia maamuzi kidogo, lakini kwenye mpira wa miguu lazima uamue. Unatakiwa kuwapa nafasi wachezaji kufanya usajili pale unapoona hawana nafasi ya kucheza kwenye kikosi chako.
'Unatakiwa kusema mapema kwasababu ni mbali sana baada ya Agosti 31. Nitawaambia wachezaji baada ya ziara hii, lakini nitawaambia wao na sio ninyi.'
Van Gaal aliyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Miami jana kuelekea mechi ya fainali ya leo usiku ya kombe la kimataifa nchini Marekani dhidi ya mahasimu wao wakubwa England, klabu ya Liverpool.

waliotembelea blog