Friday, July 11, 2014

Bingwa mara tatu Ujerumani na bingwa mara mbili Argentina zitagombania dola milioni 35 kwenye mechi ya fainali ya kombe la dunia Jumapili Julai tarehe 13 mjini Rio De Janeiro.
Shirikisho la kimataifa Fifa limetoa jumla ya dola milioni 576 kushindaniwa kwenye mashindano ya mwaka huu nchini Brazil.
Mshindi ataweka kibindoni dola milioni 35 na wa pili $25 milioni, wa tatu $22milioni wa nne $20 milioni.
Timu nne zilizoondolewa kwenye robo-fainali zitapokea $14 milioni kila mmoja, timu nane zilizong'olewa raundi ya pili $9 milioni na timu 16 zilizoondolewa raundi ya kwanza $8 milioni kila mmoja.
Ujerumani imefuzu kwa fainali baada ya kuiadhibu Brazil mabao 7-1 na Argentina ikaiondoa Uholanzi mabao 4-2 ya penalti mechi ya nusu-fainali. Kwa jumla timu 32 zimeshiriki mashindano ya mwaka huu kwenye mechi 64 na wachezaji 736 wakajitosa uwanjani.
Argentina ilifuzu baada ya kushinda Uholanzi
Miongoni mwa wachezaji nyota kwa upande wa Ujerumani ni mfungaji bora zaidi kwenye mashindano haya Miroslav Klose huku Argentina ikijivunia Lionel Messi mshindi wa tuzo la mchezaji bora duniani mara nne.
Hii ni mara ya tatu Ujerumani na Argentina wanakutana fainali ya kombe la dunia, mara ya kwanza ikiwa mwaka wa 1986 nchini Mexico Argentina ikashinda 3-2 kisha wakapatana tena mwaka wa 1990 nchini Italia na Ujerumani ikalipiza kisasi kwa kuinyoa Argentina bao 1-0.
Wadadisi wengi wa kandanda wanasema Ujerumani wana nafasi nzuri zaidi ya kuibuka mshindi kwani wameonyesha kiwango cha juu zaidi ya Argentina kufikia sasa.
Lakini mpira unadunda hivyo basi Argentina nao pia waeza kuibuka mshindi ikikumbukwa kwamba hamna timu ya bara Ulaya imewahi kunyakua ubingwa wa dunia mashindano haya yakifanyika Marekani Kusini.
Kwa jumla mataifa ya Marekani Kusini yameibuka mshindi mara tisa kwenye kombe la dunia na ya Ulaya mara kumi Italia na Ujerumani wakiongoza kwa kushinda mara tatu kila mmoja na Brazil ikiwa juu Marekani Kusini kwa kushinda mara tano, Argentina na Uruguay mara mbili kila mmoja.
FIFA yakatalia mbali rufaa ya Suarez
Shirikisho la soka Duniani FIFA limekatalia mbali ombi la rufaa la mchezaji wa Uruguay Luis Suarez dhidi ya marufuku yake ya mizi minne kwa kosa la kumng'ata Mlinzi wa Italia .
Katika barua kwa wanahabari FIFA ilisema kuwa imekatialia mbali ombi la Shirikisho la Soka la Uruguay la kuitaka kupunguza adhabu ya Mshambulizi huyo wa Liverpool .
Hata hivyo Suarez anauhuru wa kukata rufaa katika mahakama ya rufaa ya michezo (Court of Arbitration for Sport) iwapo hataridhika na Uamuzi huo.
Mshambulizi huyo wa Liverpool alibanduliwa nje ya kombe la dunia baada ya tukio hilo la Juni tarehe 24 na sasa anaomba msamaha ili iwe rahisi kwake angalau kujifua pamoja na wachezaji wenza huko Anfield Uingereza huku akitarajia uhamisho kuelekea Uhispania katika klabu ya Barcelona .
Papa Francis na Papa Benedict kushabikia fainali ya kombe la dunia ?
Je ushawahi kushabikia smechi ya kandanda baina ya mahasimu wawili wa jadi ?
Sasa hebu fikiria Mashabiki wa mechi ya fainali kuwa ni Viongozi wa kidini .
Taswira hiyo huenda ikakamilika siku ya jumapili Papa Francis ambaye ni Raiya wa Argentina akitizama mechi baina ya Argentina na Ujerumani na Papa mtangulizi wake Benedicto 16 raiya wa Ujerumani.
Makao makuu ya Kanisa Katoliki hata hivyo imekuwa wazi ikisema kuwa hilo huenda lisikamilike kwani papa Benedicto sio shabiki sugu ukimlinganisha na papa Francis ambaye ni shabiki sugu wa Argentina.
Msemaji wa Vatican Federico Lombardi akisema kuwa labda kadinali mkuu wa zamani wa Buenos Aires Jorge Bergoglio yaani papa Franci atatizama fainali hiyo.
Argentina na Ujerumani zilichuana katika fainali ya kombe la dunia 1986
Papa Benedict XVI, 87, anajulikana kuwa msomi na pia mwenye uraidbu wa mziki wa ala mara nyingi akipapasa roho yake kwa kucheza piano .
Wangdani wa Vatican ahata hivyo wanasema kua katika enzi zake Papa Benedict XVI alikuwa hawezi kosa matokeo ya mechi za klabu anayoishabikia ya Bayern Munich.
Gazeti moja la Italia''the Osservatore Romano'' ndilo lililotibua uvumi huu lilipochapisha habari kabla ya kuanza kwa kombe la dunia lilipobashiri kuwa Argentina itakutana na Ujerumani katika fainali ya kombe la dunia na hivyo kushuhudia mashabiki wa haiba yake , papa Benedicto wa 16 na papa Francis .

download (2) 
KATIKA fainali za mwaka 1986, Diego Maradona aliifungia Argentina au kutoa pasi za mwisho katika mabao 10 ya nchi hiyo. Mwaka huu, Messi amefunga au kutoa pasi katika mabao 8 ya Arggentina. Maradon pia alikabiliana na Ujerumani (Ujerumani Magharibi kwa wakati huo) katika mchezo wa fainali, lakini hakufunga goli katika mechi hiyo.

download 
Carlos Queiroz alijiuzulu nafasi yake ya ukocha wa timu ya taifa ya Iran baada ya nchi hiyo kutolewa hatua ya makundi katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Mtandao 0712461976 HAPA tunaangalia kwanini Asia imeshindwa kufanya vizuri katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
1.     UKOSEFU WA UONGOZI Wakati kocha wa Korea Hong Myung-bo anasafiri kwenda Uholanzi mwezi machi mwaka huu kumtembelea Park Ji-sung, hakwenda kuangalia wachezaji muhimu bali ni kumshawishi nyota huyo aachane na mpango wa kustaafu soka la kimataifa. “Timu ya vijana inahitaji wakongwe,” alisema Hong. Park alipotezea wazo lile, lakini ni ukweli kuwa Korea ilikosa wachezaji wenye uzoefu na viongozi kama yeye.  Pia  Japan haikuwa na wachezaji ambao wangepewa majukumu ya kuwaongoza vijana uwanjani katika mazingira tofauti tofauti ya mechi.
2.   MAKOSA YA MAKOCHA Alberto Zaccheroni alikuwa na maandalizi kamili yaliyochukua hadi miaka minne tangu alipokabidhiwa timu ya Japan, lakini bado kocha huyo raia wa Italia hajaweza kuonesha kiwango kizuri katika hatua ya makundi. Japan ilicheza mpira wa kawaida dhidi ya Ivory Coast na Ugiriki. Alikosolewa kwa kumuanzisha Yasuhito Endo  dhidi ya Waafrika, pia aliendelea kumuacha Yasuyuki Konno katika idara ya ulinzi wakati alishindwa kufanya kazi yake na angemtumia hata  Zaccheroni kutokana na kiwango chake kuwa kizuri kwa wakati ule.
Kocha wa Korea, Hongg, hakuwa na wachezaji wenye uzoefu, lakini alishindwa kuwatumia vijana wake katika safu ya ulinzi na hakusikiliza ushauri wa vyombo vya habari na mashabiki na kuendelea kumtumia mshambuliaji butu Park Chu-young. Carlos Queiroz alikuwa na kiwango kizuri, labda atajuta baada ya kushindwa kuonesha ubora wake na kuisaidia timu kwenye mechi dhidi ya Bosnia.

article-2688109-1F8DDD0F00000578-722_634x454 
Kwenye rada: Beki wa Atletico Madrid, Javi Manquillo anatakiwa na Arsenal.
KLABU ya Arsenal inafanya jitihada za kumsajili beki wa kulia wa Atletico Madrid , Javi Manquillo.
Washika mtutu hao wa London wanataka kumsajili beki huyo wa Hispania kwa lengo la kuongeza ushindani katika nafasi ya beki wa kulia msimu ujao.
Kama watakamilisha usajili huo, basi Manquillo atachuana katika nafasi hiyo na beki waliomsaini siku chache zilizopita, Mathieu Debuchy.
article-2688109-15AAA01D000005DC-583_634x486 
Njiani kusepa: Carl Jenkinson anaweza kuondoka Asernal na anawindwa zaidi na Newcastle.

article-2688200-1F8E156C00000578-361_634x430 
Hisia: Neymar alimwaga machozi, huku akiweka wazi kuwa alikaribia kuwa kichaa baada ya Juan Zuniga kumfanyia faulo mbaya kwenye mchezo wa robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya Colombia.
NYOTA wa Brazil, Neymar Jr amefichua siri kuwa alishindwa kuzuia machozi na alikaribia kuwa kichaa baada ya kugongwa na Juan Zuniga na kuvunjika mfupa wa uti wa mgongo.
Neymar kwa mara ya kwanza alifanya mkutano na waandishi wa habari baada ya kutoka Hospitalini ambapo anauguza majeraha yake ya mfupa wa uti wa mgongo uliovunjika kwenye mechi ya robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya Colombia.
article-2688200-1F8E0D0A00000578-115_634x432 
Machozi: Neymar alishindwa kuendelea kucheza fainali za kombe la dunia baada ya kuvunjika mfupa wa uti wa mgongo.
Pia Neymar hajakubaliana na maneno ya wakala wake aliyemuita Luiz Felipe Scolari kuwa ni kocha mbaya, mwenye majivuno na aliyepitwa na wakati.

waliotembelea blog