Tuesday, June 3, 2014


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Silas Mwakibinga akiwaonesha waandishi wa habari uthibitisho wa malipo ya shilingi milioni 400 ikiwa ni sehemu ya pili ya malipo kwa ajili ya Ligi Kuu.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Azam Media Rhys Torrington (kulia) akimkabidhi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Silas Mwakibinga nakala ya uthibitisho wa malipo ya fedha kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom.

KAMPUNI ya Azam Media imetangaza kuwa tayari imeshatuma fedha kwa Bodi ya Ligi kwa ajili ya msimu wa ligi wa Vodacom kwa mwaka 2014/ 2015.
Fedha hizo zimetolewa mapema zaidi kwa ajili ya kusaidia maandalizi mapema kwa timu kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba wa miaka mitatu ya udhamini wao katika ligi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za Azam zilizopo Tazara, Dar es salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington, alisema kuwa kampuni hiyo inavutiwa na aina nzuri ya ushirikiano kati yake na bodi ya Ligi.
Alisema kuwa kupitia bodi hiyo Azam imepiga hatua kubwa katika kufanikisha adhma yake ya kuifanya Ligi hiyo ya Vodacom kuwa ya kuvutia zaidi.
“Ligi hii tunataka kuifanya kuwa ni moja kati ya ligi zinazovutia na kuonesha ushindani barani Afrika, ingawaje ninajua kuwa kuna mengi ambayo yanatakiwa kuendelea kufanywa ili kuipa nguvu zaidi ligi hii”alisema Torrington. Alisema kuwa kwa kutambua hilo ndio maana Azam Media imehakikisha kuwa klabu zote zinapata fedha mapema ili kusaidia suala zima la maandalizi.

Akizungumzia mikakati ya baadae ya Azam Media alisema kuwa inatarajia kuanza kuonesha soka la mitaani (street soccer) mbalimbali moja kwa moja (live) itakayokuwa ikiendelea kwenye nchi za Kenya na Uganda.

Alisema kuwa kwa sasa Azam Media imeanza kujikita katika nchi za Kenya, Uganda na Malawi ambapo itakuwa ikiuza ving’amuzi vyake katika nchi hizo. Aliongeza kuwa pia katika kuhakikisha kuwa inatoa mwanya zaidi wa vipindi vizuri na vya kuvutia inaendelea na vipindi vya michezo vya Morning Trumpet, sport@8 pamoja na Kwetu House.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi, Mr Silas Mwakibinga alisema kuwa kwa hatua hiyo ya Azam ya kuhakikisha upatikanaji wa fedha hizo kwa wakati ni nzuri na itasaidia kuzipatia timu muda mzuri wa kujiandaa. Alisema kuwa bodi yake inavutiwa sio tu na utangazaji wa vipindi unaofanywa na Azam bali pia hata nia yao ya kuendeleza soka la Tanzania.

Azam Media ilisaini mkataba wa miaka mitatu na wenye thamani ya TSHS5,560,800,000 kuonesha mechi za live na za kurekodi mechi za Ligi Kuu na fedha hizo zinalipwa kwa awamu tatu.

Fainali za Kombe la Dunia ni uwanja mpana. Ni mahali ambapo vipaji na vipaji vya wanasoka duniani huonekana. Madalali wa kuvumbua na kununua wachezaji [scouts] hufurika kwenye mashindano kama haya wakijua wazi kabisa kwamba pale ndipo watakapoona “lulu” kwa ajili ya vilabu vyao. Kwa maana hiyo kuna kila aina ya harakati za kimichezo na kuonyesha na kuonyeshana vipaji. Hii sio kumaanisha kwamba wachezaji wote mahiri hapa duniani walicheza katika fainali za Kombe la Dunia.La. Wapo wasakata kabumbu kadhaa ambao hawakuwahi kugusa fainali hizi.Mfano ni George Opong Weah na watu kama kina George West nk.

Lakini wakati wengine wakionyesha vipaji ili wang’amuliwe na kubadilisha maisha yao ya kisoka,wapo wale ambao wanashuka dimbani tayari wakiwa na majina [superstars] na ambao dunia tayari inakuwa ikiwaangalia kwa makini kutaka kujua na kuona kile watakachokifanya. Kila timu huwa na mchezaji ambaye hutizamwa zaidi. Kwa umombo unaweza kumuita Key Player. Kila timu,kwa kupenda au kutopenda,huwa ina star player. Hii haimanishi kwamba katika timu hakuna wachezaji wengine wenye majina au wanaoweza pia kuwa stars.La. Ni sheria ya mmoja mmoja inayozingatiwa hapa.

Kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali wa soka,wachezaji hawa 32 [mmoja kutoka katika kila timu inayoshiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka huu] ndio watarajiwa kuchomoza zaidi huko Brazil. Mpangilio huu hapa ni kutokana na makundi ya FIFA World Cup 2014. NB: Orodha hii inaweza kubadilika kwani imeandikwa kabla timu zote hazijathibitisha wachezaji wake 23 iliyowachagua mwisho. Wengine wanaweza kuumia katika siku hizi za mwisho na hivyo kutokwenda Brazil.Zingatia.
Neymar-Brazil.
Hakuna ubishi kwamba Neymar anayechezea soka la kulipwa Barcelona nchini Spain ndio gumzo kubwa kwa timu ya Brazil. Anatarajiwa kuongoza mashambulizi ya The Kings Of Samba[Brazil]
Oribe Peralta-Mexico
Ingawa wachezaji wengine wa Mexico kama Chicharito na Giovani dos Santos wanatajwa kama ma-star,Oribe Peralta ambaye anacheza katika ligi ya nyumbani katika club ya Santos Laguna, ndiye anaaminika hivi sasa kuwa star zaidi
Luka Modric-Croatia
Hakuna shaka kwamba Luka Modric ndiye mchezaji star zaidi hivi sasa katika timu ya Croatia. Kiungo huyu ambaye hivi sasa anachezea timu ya Real Madrid nchini Spain ameonekana wazi kuwa tegemeo sio tu katika club bali nchi yake Croatia.

Charles Itandje-Cameroon
Ingawa ungetegemea mchezaji kama Samuel E’too kuendelea kuwa star na tegemeo zaidi katika timu ya Cameroon, golikipa Charles Itandje ndio tegemeo na ambaye wengi watapenda kumuona akiokoa mikwaji. Charles ambaye anachezea timu ya Konyaspor nchini Uturuki[kwa mkopo kutoka PAOK FC ya Ugiriki] aling’ara vilivyo katika mchezo dhidi ya Tunisia wakati wa kuwania nafasi ya kwenda Brazil.Google utaona alichofanya.
Diego Costa-Spain
Ingawa bado kuna utata kuhusu hali yake na kama atakuwa fit kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia huko Brazil,Diego Costa mshambuliaji mahiri wa timu ya Atletico Madrid anatarajiwa kuwa nyota wa Spain. Lakini pia huenda akawa ndiye mchezaji atakayezomewa zaidi huko Brazil kwani Diego ni mzaliwa wa Brazil na angeweza kabisa kuchezea Brazil mwaka huu kama asingeamua kuchezea Spain[pia ni raia wa Spain].Wabrazil hawajaipenda hiyo.
Arjen Robben-Holland[The Netherlands]
Robben,mshambuliaji mahiri ambaye hivi sasa anaendelea kuwika na timu ya Bayern Munich nchini Ujerumani,ndiye mchezaji ambaye ni star zaidi na ambaye ameonyesha kuwa na kile kiwango kinachoitwa “cha dunia”. Ana miaka 30 hivi sasa.
HABARI ZAIDI BOFYA LINK HIYO HAPO

Monday, June 2, 2014


Wakaazi wa Mwanza wakiwa wamefurika kwa maelfu huku wakishangilia wakati kundi la Weusi likitumbuiza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

Msanii wa Bongo flava, Ben Pol akitumbuiza maelfu ya wakazi wa Mwanza wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

Msani wa muziki wa dance, Christian Bella akikonga nyoyo za wakazi wa Mwanza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

Msanii wa bongo flava, Fid Q akizungumza na wakazi wa Mwanza wakati akitumbuiza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz wakimakinika katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rich Mavoko akipagawisha wakazi wa Mwanza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

Wakazi wa Mwanza wakiwa wamefurika kwa maelfu huku wakishangilia wakati kundi la Weusi likitumbuiza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

Msanii wa miondoko ya Bongo flava, Young Killer akimtambulisha mama yake mzazi wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

Vanessa Mdee na Fid Q wakishirikiana kutoa burudani wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

Msanii wa Bongo Flava Izzo Biznez akifanya vitu vyake wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

Sunday, June 1, 2014



All Star Club Elizabeth New Jersey Diamond akikamua licha ya show kuchelewa kuanza na wapenzi wa Diamond kushikwa na jazba wakitaka aendelee lakini ikashindika kutokana na muda wa kufunga club kufika.

AJ nae akifanya yake baada ya kupewa nafasi ya ufunguzi katika show hiyo iliyofanyika New Jersey.

AJ Ubao na Dirty Hary wakishambulia jukwaa kwenye show ya kufubgua pazia iliyoanyika New Jersey na baadae Prezidaa wa Wasafi, Diamond Plutnumz kuwapagawisha mashabiki wake wa ukanda wa pwani ya mashariki.

Ni Rais wa Wasafi akishambulia jukwaa akiwa na madancer wake kwenye show ya kukata na shoka iliyofanyika New Jersey na kuvuta mashabiki kutoka kila kona ya pwani ya mashariki ambayo ni DC, PA, NJ, NY, CT, MA na kwingineko

Diamond mwanamuziki wa kizazi kipya anayekimbiza vibaya mno kwenye anga za Bongo Flava akipagawisha mashabiki wake New Jersey nchini Marekani.

Diamond na madancer wake wakijaribu kukata kiu ya mashabiki wake wa pwani ya mashariki.

Wapenzi wa Diamond wakipagawa na show ya Diamond iliyofanyika All Star Club Elezabeth NJ.
Shabiki akidata na show ya pezidaa wa wasafi.
Shabiki akidatishwa na moja ya wimbo wa Diamond na kushindwa kujizuia kupanda jukwaani.

Wednesday, May 28, 2014



ALIEKUWA Meneja wa Southampton Mauricio Pochettino  ameteuliwa kuwa Meneja mpya wa Tottenham Hotspur kwa Mkataba wa Miaka Mitano.
Pochettino, mwenye Miaka 42, aliteuliwa kuwa Meneja wa Southampton hapo Januari 2013 alipombadili Nigel Adkins na Msimu huu amewafikisha Nafasi ya 8 kwenye Ligi Kuu England iliyomalizika Mei 11, na kabla uteuzi huu wa Leo wa kwenda Tottenham, alijiuzulu wadhifa wake wa Southampton.
Pochettino anamrithi Tim Sherwood alietimuliwa mapema Mwezi huu. 

Raia huyu wa Argentina anakuwa Meneja wa 10 wa Tottenham tangu Mwaka 2001.
Waliokuwa Wasaidizi wa Pochettino huko Southampton, Jesus Perez, aliekuwa Meneja Msaidizi, Kocha wa Timu ya Kwanza, Miguel D'Agostino, na Kocha wa Makipa, Toni Jimenez, wote wanaungana nae huko Spurs.
Roberto Soldado kuuzwa?

KUHUSU POCHETTINO:

-Kazaliwa 2 Machi 1972 huko Santa Fe, Argentina
-Alichezea Klabu za Newell's Old Boys, Espanyol, PSG na Bordeaux
-Akiwa na Espanyol alitwaa Copa del Rey mara 2: 1999/2000 na 2005/06
-Ameichezea Argentina mara 20 na kufunga Bao 2
-Aliteuliwa Meneja wa Espanyol Januari 2009.
-Aliteuliwa Meneja wa Southampton hapo Tarehe 18 Januari 2013
-Alifanikiwa kuzitwanga Manchester City, Liverpool na Chelsea kwenye Ligi


UEFA imewafungulia Mashitaka Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone na Kiungo wa Real Madrid Xabi Alonso kwa kuwatuhumu kufanya Utovu wa Nidhamu kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI iliyochezwa Jumamosi iliyopita huko Lisbon, Ureno na Real Madrid kuichapa Atletico Madrid Bao 4-1.
Wote hao wawili wameshitakiwa kwa makosa ya kuvamia Uwanja.
Mara mbili Diego Simeone aliingia Uwanjani wakati wa Dakika za Nyongeza 30 kwenda kumkabili Beki wa Real Raphael Varane na ikabidi azuiwe na Wasaidizi wake.
Pia Simeone alionyesha kukasirishwa na Refa Bjorn Kuipers wa Holland. Nae Xabi Alonso, ambae alikosa kucheza Fainali hiyo kwa sababu alikuwa Kifungoni, alionekana akikimbia nje ya Uwanja baada ya Mechi hiyo.
UEFA imetamka kuwa Kesi za wawili hao zitasikilizwa hapo Julai 17 na wakipatikana na hatia baadhi ya Adhabu zao ni kuzikosa Mechi za UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao.
Vile vile, UEFA imezifungulia Mashitaka Klabu zote mbili, Real Madrid na Atletico Madrid, kwa kuzoa Kadi za Njano 5 kila moja katika Fainali hiyo.
Kwenye Mechi hiyo, Wachezaji 7 wa Atletico na 5 wa Real walipewa Kadi za Njano.


Cardiff City imemsaini Straika wa Manchester United Federico Macheda kwa Mkataba wa Miaka Mitatu.
Macheda, mwenye Miaka 22, anakuwa Mchezaji wa 3 kusainiwa na Cardiff kwa ajili ya Msimu ujao na atahamia bila malipo kuanzia Julai 1 wakati Mkataba wake na Man United utakapoisha. 

Macheda aliwahi kufanya kazi huko Man United chini ya Bosi wa Cardiff, Ole Gunnar Solskjaer, alipokuwa Kocha wa Timu ya Rizevu.
Macheda alijiunga na Timu ya Vijana ya Man United Mwaka 2007 akitokea Lazio na kuwa Mfungaji Bora wa Timu ya Vijana ya chini ya Miaka 18 katika Msimu wake wa kwanza tu Old Trafford kwa kufunga Bao 12 katika Mechi 21.
Mwaka 2009, akiwa na Miaka 17 tu, Macheda aling’ara katika Mechi yake ya kwanza tu na Timu ya Kwanza ya Man United walipokuwa nyuma kwa Bao 2-1 na Aston Villa, Cristiano Ronaldo akasawazisha, na Macheda kupiga Bao la ushindi katika Dakika za Majeruhi na kuisaidia sana Man United kwenye mbio zao za Ubingwa Msimu huo.
Msimu huo, Macheda aliendelea kuonekana mara kadhaa kwenye Timu ya Kwanza na alifunga Bao lake la Pili kwa Man United Sekunde 45 tu baada ya kumbadili Dimitar Berbatov kwenye Mechi na Sunderland.

Msimu huo, Macheda alitunukiwa Tuzo ya Jimmy Murphy ambayo hupewa Mchezaji Bora wa Mwaka toka Chuo cha Soka cha Man United.
Lakini Msimu uliofuatia, Macheda akaanza kuzongwa na Majeruhi ya mara kwa mara na maendeleo yake kuathirika.
Misimu iliyofuatia, Macheda akawa anacheza nje ya Man United kwa Mkopo kwenye Klabu za Sampdoria, Queens Park Rangers, VfB Stuttgart, Doncaster Rovers na Birmingham City, ambako alifunga Bao 10 katika Mechi zake 18.

waliotembelea blog