![](//1.bp.blogspot.com/-Kf6Dp9nzOV0/UYxS1vdihnI/AAAAAAAAJJI/2MTELq8IXbs/s000/date.png)
4:36 AM
![](//2.bp.blogspot.com/-KsISg7lKRxM/UYxS2WyOSBI/AAAAAAAAJJQ/R416Afh-K1I/s000/user.png)
Unknown
Jana
huko Parc des Princes Jijini Paris Nchini France Mabingwa wa huko Paris
St Germain waliifumua Barcelona 4-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya
Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI.
Kwenye Mechi nyingine ya Raundi hiyo Benfica iliichapa Borussian Dortmund 1-0.
Katika
Mechi ya PSG na Barca, Bao za PSG zilipigwa na Angel Di Maria, Dakika
za 18 na 55, Julian Draxler, 40', na Edinson Cavani, 71'.
PSG walitawala Mechi hii na Barca kupooza mno huku Mastaa wao Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar 'wakijificha'.
Kipigo
hiki kinaiweka Barca pagumu kufuzu kwenda Robo Fainali na wakishindwa
hilo hii itakuwa mara ya kwanza kwao kutotinga Robo Fainali katika Miaka
10.
0 maoni:
Post a Comment