5:43 AM
Unknown
Wasichana
wanne wa Tanzania wakiaga kwa kupungia mikono huku wakiwa na , Bendera
ya Taifa waliyokabidhiwa na Kamishna Mkuu wa Chama cha Tanzania Girl
Guids (TGGA), Symphorosa Hangi katika hafla ya kuwaaga kwenda Uganda
ambako watakutana na wenzao 31 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati
katika mafunzo ya uongozi na utamaduni katika nchi hizo. Hafla hiyo
ilifanyika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam juzi. Kutoka
kulia ni Farida Mjoge,Elizabeth Betha, Edna Chembele na Ummy Mwabondo.
(PICHA, HABARI NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Kamishna
Mkuu wa Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), Symphorosa Hangi
(kushoto) akiwakabidhi wasichana wanne, Bendera ya Taifa katika hafla ya
kuwaaga kwenda Uganda ambako watakutana na wenzao 31 kutoka nchi za
Afrika Mashariki na Kati katika mafunzo ya uongozi na utamaduni katika
nchi hizo. Hafla hiyo ilifanyika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar
es Salaam juzi. Kutoka kulia niElizabeth Betha, Edna Chembele, Farida
Mjoge na Ummy Mwabondo.
Na Richard Mwaikenda
WASICHANA wanne wameondoka kwenda Uganda kwenye programu maalumu ya kubadilishana uzoefu wa mafunzo ya uongozi na utamaduni.
Wakifika
Uganda wataungana na wenzao 31 kutoka nchi nane za Afrika Mashariki na
Kati, ambapo watapigwa msasa wa mafunzo hadi Januari 25, mwaka huu
watakapotawanywa kwenda nchi mbalimbali.
Wasichana
hao wanachama wa Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA),waliondoka Uwanja
wa Ndege wa Kimaitafa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, juzi kwa Ndege
ya Kenya Airways, baada ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Kamishna
Mkuu wa Tgga, Symphorosa Hangi.
Wasichana
hao 35 watagawanywa katika nchi hizo nane ambapo nchini wataletwa
watatu kutoka katika baadhi ya nchi hizo, kuja kujifunza masuala ya
uongozi na utamaduni.
Akizungumza
wakati wa kuwaaga wasichana hao, Kamishna Mkuu wa Tgga, Hangi alisema
lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wasichana ili wawe viongozi
bora wa baadaye katika nchi zao ikiwemo pia kujiamini na kujithamini.
Alitaja
nchi zitakashiriki kwenye programu hiyo ambayo kwa hapa nchini ilianza
mwaka jana, kuwa ni; Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia, Rwanda, Burundi,
Zimbabwe na Afrika Kusini.
Alisema
kuwa watakapokuwa kwenye nchi hizo husika, kila mmoja ataishi maisha ya
kujitegemea kwa kwenda vijijini kuishi na wananchi na kuzungumza nao
kuhusu mambo mbalimbali ya maisha ikiwemo uongozi, utamaduni, kujiamini
na kujithamini. Gharama za kwenda katika nchi hizo hufahiliwa na Taasisi
ya FK Norway ambayo huwapatia nauli, fedha za malazi, posho na masuala
ya afya.
Alisema
kuwa watakaporejea nchini Julai mwaka huu, watapaswa kutoa mrejesho wa
waliojifunza huko, ili usaidie kuwaelimisha wasichana wengine nchini.
Kamishna akiwakabidhi nyaraka mbalimbali za kazi
Ni furaha iliyoje
Wakipiga picha na baadhi ya wafanyakazi wa TGGA
Wakipiga picha na dereva wa TGGA,Juma Rashid
Kamishna akiagana na mmoja wa wasichana hao
0 maoni:
Post a Comment